Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,473
- 13,624
Kaka Dar inakua usizichukulie hizo sababu zako za mwaka 2016 kuwa ndizo zitakuwa sababu za mwaka 2046, kuna maisha baada ya mimi na wewe kuondoka duniani. Wazungu wanaendelea kwa sababu wanao uwezo mkubwa wa kujifunza kutazama miaka mingi ijayo.Kwanza hakuna mahali niliposema kwamba hilo daraja halina mahitaji, najua kwamba linahitajika na watu wanaokwenda kipepepo wkend au kuangalia wanyama Dar zoo n.k ila hizo sababu ni ndogo sana ukilinganisha na mahitaji mengine ambayo hizi bilioni 200 zingeweza kufanya kama hizi hele zingeingizwa kwenye kupunguza msongamano ingetoa tofauti kubwa sana, sasa hivi tunavyoongea NSSF inashida ya fedha kwa sababu ya mradi kama huu, sasa kwa nini tufilishi shirika lenye kuweka akiba zetu za uzeeni kwa kuwekeza kwenye mradi ambao unafaidisha watu chini ya asilimia 5% ?
Na hapo ndipo Kipaumbele kinapokuwa na umuhimu, sababu kubwa ya kujengwa hilo daraja kama nilivyosema haina uhusiano wowote ule na manufaa ka Wananchi bali ni prestige project kwamba tuweze kupiga picha na kusema Dar tuna Daraja lkn siyo kumwezesha Mtz kiuchumi na hili litaonekana wazi daraja litakapofunguliwa utakuwa shahidi kama kweli vivuko vitapungukiwa na watu na ninaweza kukuhakikishia asilimia 90% ya wanaotumia vivuko wataendela kutumia hivi vivuko hata baada ya daraja kufunguliwa na watakao litumia niwachache ambao wanakwenda wk end kipepeo beach au kukagua mashamba yao, sasa dola 200 bilioni kutumika kufanya uwekazaji kama huu kwenye nchi ambayo ukifungua tu mlango umaskini umekuzunguka kila mahali na wali hata haujui uanzie wapi ni kutokuwa na uwezo wa kupanga vizuri!