Kupinga Daraja la Kigamboni kunatokana na mtu kutofahamu tabu na adha ya foleni wakati wa kusubiri kivuko, muda unaotumika ni mrefu na hiyo huwa kwa mtu anaetoka mjini kwenda Kigamboni na vice versa. Kigamboni kuna mahoteli, airstrips na recreation sites ambazo zinavutia wageni na wenyeji lakini ambao wanakatishwa tamaa kuzifikia kutokana na usumbufu wakati wa kuvuka.
Wakazi wengi wa Dar es salaam wanamiliki maeneo wanayoshindwa kuyaendeleza kutokana na ugumu wa kuyafikia na wengine wanashindwa kuanzisha makazi katika maeneo wanayomiliki kwa kuwa shughuli zao ziko center na kufika huko kwa wakati kunakwamishwa na foleni ya kupanda kivuko.
Kigamboni ni wilaya mpya ambayo inatarajiwa kuwa jiji jipya la kisasa, shughuli zote za kuliendeleza na kulikuza jiji na kufikia viwango vinavyotarajiwa, itahitaji mfumo mwanana wa usafirishaji wa vifaa na watu watakaoshiriki katika mchakato mzima wa kulijenga jiji hilo na daraja ni suluhisho muafaka wa kuyafanya yote hayo yawe rahisi.
Ukiachana na mradi wa mji mpya, tayari Kigamboni kuna miradi mingi mikubwa ya makazi mapya ya kisasa ambayo yanatarajiwa kuaccommodate maelfu ya wazalendo na wageni. Mifano mizuri ni: Dege eco Village, Avic Town, Mradi wa Nssf Mwongozo, Mradi wa Nssf Kibada, Mradi wa Nssf Tuangoma na midogo ya makazi Mwasonga ambayo iko katika maeneo matatu katika kijiji hicho.
Hivi kweli bado Daraja lisiwe na maana? Inaingia akilini kweli? Tafiti kabla ya kuzungumza.