Daraja la Kigamboni ni White Elephant Project, Hatulihitaji!

Daraja la Kigamboni ni White Elephant Project, Hatulihitaji!

mtoa mada musimlaumu coz yeye ndie msomi wa kwanza wa ukoo na kijijini kwao,hivyo hawezi kuona umuhimu wa daraja la kigamboni km vile mwenyekiti wa kijiji chake asivyoweza kuona umuhimu wa daraja hilo.
Bila shaka mtoa mada ameliona daraja kwenye picha au through TV,
 
Duh! Hata kama ni upinzani basi wa kwako umepindukia. Kwanza utambue kuwa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa kiasi kikubwa unatekelezwa na NSSF. Kwa maana hiyo ni kwamba ni mradi wa Taasisi Binafsi kwa kushirikiana na Serikali kupitia PPP. Ujenzi wa daraja hilo ni kama Ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Ubungo hadi Chalinze. Huwezi kumpangia mtu mradi ambao anataka kuwekeza.

By the way, wanaojua umuhimu wa daraja la Kigamboni ni wakazi wa Kigamboni. Wewe Mburula ambaye upo hapo Arusha Mjini utajuaje adha ya usafiri wanayokumbana nao wakazi wa Kigamboni?
Oh yes wakazi wa Kigamboni ambao ni milioni ngapi vile?????
 
Oh My God! Siwezi hata kufikiri kwamba kuna kiumbe anaye weza kuja na hoja kama hii. It's a total embassment. I thought hii forum ni ya Great Thinkers. What a waste of time!

Think about congestion ya traffic in the inner city. Think about mafuta yanayo potea bure kwenye hizo foleni, think about kuboresha sehemu zingine za jiji, think about maendeleo ya satellite cities, etc. Halafu eti unasemaje???
watu wa namna hiyo wapo tena wengi sana, na unaweza kukuta ana elimu nzuri sana, ila ana fikra za zamani sana, watu wanajaribu kupunguza msongamano watu wengine wanamawazo mfu.
 
Naona wakazi wa Kigamboni mmeungana kuleta mashambulizi. Hoja ya mdau ni mgawanyo wa fedha za miradi utakaowafikia watu wengi zaidi. Kwamba zimetumika fedha nyingi kujenga hilo daraja kwenda huko (Which might be good), lakini wakazi wengi wa jiji wametelekezwa na wengine wachache (Kimara/Mbezi) kuletewa mradi wa kipuuzi sana (DART) ...

Sasa tukiwa hatujapona majeraha sisi wakazi wa Mbagala, Gongo la Mboto, Tegeta nk, tunaotumia barabara korofi kama ya Mandela, Kilwa nk tunaambiwa kuna daraja lingine litakalotumia mabilioni, eti litajengwa kutoka Posta, Salenda mpaka coco beach; Unadhani tunafurahia au ku enjoy?! Tuache ubinafsi nyie watu.
 
Sina kinyongo na wakazi wa Kigamboni ila tatizo liko kwenye gharama ya Ujenzi wa hili Daraja ikilinganishwa na faida itakayopatikana kutokana na utumiaji wake, Je ni asilimia ngapi wa wakazi wa DSM watalitumia? Kwa maana jibu la hili swali ndiyo lilipaswa lihalalishe ujenzi wake!

Na sasa kwa kuwa wewe mwenyewe umefafanua hivyo kuhusu tatizo la foleni, ni kipi kingepaswa kianze je Daraja la Kigamboni au kujengwa na kuboreshwa kwanza kwa hizo barabara ulizozitaja?
Kimsingi unatakiwa kuelewa kigamboni ni sehemu inayokuwa kwa kasi, kuna kiwanda cha cement, kuna beach nzuri kwa ajili ya utalii, kuna miradi ya nyumba za makazi ambazo zipo chini ya Nssf, nhc , utumishi n.k , hii miradi ili iende vizuri kwakuwa ni ya kisasa inatakiwa iende sambamba na miundo mbinu ya kisasa, hayo maeneo unayopendekeza yaendelezwe ni sawa lakini kumbuka hayo maeneo hayana nafasi na ukuaji wake ni kidogo sana ukizangatia plan ilikuwa mbovu miaka ya hapo zamani..pia kumbuka huku wakazi wanaongezeka kila leo ni sehemu potential sana kwa uwekezaji , kuna vyuo vinafunguliwa na vingine vipo tayari vinafanya kazi kama mw.nyerere wanafunzi wanatoka maeneo mbali mbali uwepo wa daraja utawapunguzia adha ya usafiri kwa watakao kuwa karibu na upande wa daraja haitawalazimu watu wajekubanana kwenye foleni pale ferry..pia kuna usafirishaji wa cement kutoka kigamboni kwenda maeneo mbali mbali ikiwemo hapa dar na nje ya dar..nadhani unaijua cement ya NYATI inatoka kigamboni kaka na imani utakuwa umenielewa..na mawazo uliyoyatoa ni mazuri lakini unafanya maendeleo kwenye maeneo yenye nafasi kwanza ya jufanya hayo maendeleo..
 
Mtoa mada unakaa mkoa gani? Ninauhakika huijui kigamboni naomba ukatemee uangalie mji hasa weekend halafu rudi town kupitia ferry au Kongowe ndiyo utajua umuhimu wa hilo daraja.
 
Daraja likikamilika fedha za kigeni zitaongezeka kwenye mzunguko sababu watalii wataongezeka maeneo wa kigamboni.
Hata baada ya miaka 20 daraja litakuwepo, sioni hasara hapo.
 
Daraja likikamilika fedha za kigeni zitaongezeka kwenye mzunguko sababu watalii wataongezeka maeneo wa kigamboni.
Hata baada ya miaka 20 daraja litakuwepo, sioni hasara hapo.

Watalii waongezeke kwa sababu ya daraja? Endelea kuota, na ninakuhakikishai tena likikamilka na kuanza kutumika bado vivuko vitakuwa vinajaa na bado kivuko kitabakia kuwa ni usafiri Mkuu wa wakazi wengi wa Kigamboni na siyo hilo daraja, muda utaleta majibu yote, sana sana watumizi wakubwa wa hilo daraja watakuwa watu wachache ambao wanamagari na wanataka kwenda kipepeo beach sasa ingawaje ndiyo ni muhimu lkn kuwekeza bilioni 200 kwenye nchi masikini kama hii yetu kujenga daraja kwa ajili tu ya watu kwenda beach ni dhambi kwa Mungu!
 
Oh My God! Siwezi hata kufikiri kwamba kuna kiumbe anaye weza kuja na hoja kama hii. It's a total embassment. I thought hii forum ni ya Great Thinkers. What a waste of time!
Think about congestion ya traffic in the inner city. Think about mafuta yanayo potea bure kwenye hizo foleni, think about kuboresha sehemu zingine za jiji, think about maendeleo ya satellite cities, etc. Halafu eti unasemaje???

Mimi siyo Great thinker na wala sijawahi na sitowahi kujitambulisha hivyo ila kama wewe unaona unastahili kuitwa hivyo hiyo ni juu yako!

Haya niambie hili daraja litapunguza msongamano wa kiasi gani kwenye huu Mji? Ni asilimia ngapi ya wakazi wa Dar watalitumia kila siku kwenda na kurudi kazini ikilinganishwa na gharama iliyotumiwa kulijenga?
[/QUOTE]
Daraja litaleta foleni moja kubwa ambayo haijawahi kutokea hii ni kutokana na kuwa na foleni Sugu ya miaka yote pale kilwa road, sasa gari za temeke zikiongezeka na Kigamboni pale bondeni kwanye matanki ya mafuta kutakuwa na msongamano wa Hatari. Hilo daraja bado halijasaidia kupunguza Tatizo la msongamano wa Magari bali litazidisha majanga.
 
Daraja likikamilika fedha za kigeni zitaongezeka kwenye mzunguko sababu watalii wataongezeka maeneo wa kigamboni.
Hata baada ya miaka 20 daraja litakuwepo, sioni hasara hapo.
Watapitia wapi? Foleni itazidi mara dufu kwani barabara ya kilwa road pale bondeni itapanuliwa?
 
K
Watalii waongezeke kwa sababu ya daraja? Endelea kuota, na ninakuhakikishai tena likikamilka na kuanza kutumika bado vivuko vitakuwa vinajaa na bado kivuko kitabakia kuwa ni usafiri Mkuu wa wakazi wengi wa Kigamboni na siyo hilo daraja, muda utaleta majibu yote, sana sana watumizi wakubwa wa hilo daraja watakuwa watu wachache ambao wanamagari na wanataka kwenda kipepeo beach sasa ingawaje ndiyo ni muhimu lkn kuwekeza bilioni 200 kwenye nchi masikini kama hii yetu kujenga daraja kwa ajili tu ya watu kwenda beach ni dhambi kwa Mungu!
we daraja Asubuhi na jioni kutakuwa na foleni ya Hatari kuliko popote jijini, Tambueni kuwa kabla ya daraja barabara ya kilwa road huwa ni kero kwa foleni tena kwa Magari ya temeke pekee, sasa jiulize hizo gari za Kigamboni zikiongezeka juu yake foleni itakuaje?
 
Mleta mada bilioni 200 za nssf zinakuuma nini? Kama hasara si yao?
Kama vipi omba wakupe ukurugenzi mkuu uwapangie jinsi ya kuwekeza.
 
Kwa kifupi daraja ni kitu kizuri lakini litaongeza kero ya foleni maana Magari ya Kigamboni yakikutana na Magari ya temeke barabara ya kilwa road itakuwa na foleni mbaya kuliko zote jijini Dsm, ni vyema wapanue barabara kuwepo na daraja lingine pale bondeni kwanye zile tenk za mafuta kidogo itaweza kusaidia kupunguza kero kubwa ya foleni zisizokwisha.
 
M
Mimi siko huko kwenye siasa bali niko kwenye kuangalia kama hili daraja lina manufaa ukilingansha na fedha zilizotumika!
Pesa imeliwa kama iliwavyo kwenye miladi yote Tanzania na Majipu yamo endapo Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikalini atathubutu kuwabeep, Manufaa yatakuwepo kidogo tena kwa waende kwa miguu, baiskel, pikipiki lakini watumiaji wa magari watakumbana na foleni kubwa pindi wakivuka daraja kuja posta na huenda ikawa ni kero kubwa kuliko zote Nchi hii.
 
hawa ndio wasomi wetu waliozuia ujenzi wa barabara ya lindi to kibiti kwa kisingizio kua barabara ile haina cha kubeba
 
Ni juu ya mamlaka za kiserikali kigamboni kutumia fursa ya daraja hilo.....kwa mfano michezo,starehe,utalii n.k
Fursa ipi? Gari zikitoka Kigamboni zitakutana na foleni kubwa ya kilwa road.
 
hawa ndio wasomi wetu waliozuia ujenzi wa barabara ya lindi to kibiti kwa kisingizio kua barabara ile haina cha kubeba
Tanzania kila jambo linawezekana, sasa utashuhudia foleni mbaya kuliko zote jijini na huenda wengi wakaendelea kutumia kivuko zaidi maana wakivuka wanaingia town moja kwa moja pasipokuwa na foleni kubwa sana.
 
Nyie watu wagumu sana kuwaelewa, mnasema kuna watu wachache, sasa hiyo foleni mbaya sijui ni ya mbuzi?!!
 
Mleta uzi naona hujafanya uchunguzi wa kutosha ili kujua Ni miradi gani inafanywa na Serikali. Kwa taarifa yako DART wana awamu Tano za miradi kama huo unaokwisha. Awamu ya pili ni Tegeta Posta, ya tatu ni Mwenge Kurasini kupitia ubungo na tazara, ya nne ni Posta Gongo la Mboto. Hivyo usijali mambo yanakuja taratibu si mpaka ushuhudie.
 
Back
Top Bottom