Daraja la Kigamboni ni White Elephant Project, Hatulihitaji!

Daraja la Kigamboni ni White Elephant Project, Hatulihitaji!

Tufanye kahesabu kadooogo. 200,000,000,000 /500,000=400,000 Nadhani ni mradi fair tu ukizingatia na uwekezaji unaoendelea kigamboni sh laki nne kwa kila mwananchi inalipika kwa maisha ya daraja husika ie lifespan.
 
Mleta mada acha ubinafsi mbaya kiasi hiki, ungekuwa unakaa kigamboni ungetamani ile njia ifunguliwe hata kesho ili kuondosha adha ya usafiri kwa sisi wananchi tunaokaa kigamboni na vitongoji vyake na maeneo ya mbagala. Daraja lile litasaidia kupunguza foleni kwa njia zote mbili za kilwa road na pale kivukoni kwenda kigamboni. Binafsi naipongeza serikali na wabia wake kama nssf katika kuja na mradi huu mkubwa na wenye malengo mahsusi kwetu sisi wana kigamboni na njia ya kilwa road.
Nikushauri tuu mtoa uzi kwamba tatizo la foleni ya dar siyo kuleta DART tuu, ni pamoja na kuimarisha njia za mitaani ili kupunguza foleni kwenye njia kuu. ukiangalia tabia ya foleni za dar utaona foleni zipo kwenye makutano ya barabara kuu kama pale ubungo, tazara, chang'ombe, magomeni, moroko, mgulani, kwa aziziali, mtongani na njia ya kilwa road, mbezi ya kimara, vingunguti na makutano katika njia ya pugu nk. Kama njia za mtaani zikiboreshwa na zikapitika kiasi cha kwamba mtu anayekaa kimara aweze kwenda gongolamboto pasi na kwenda mpaka ubungo, buguruni, tazara ndio ashike njia ya pugu ilihali zipo njia za mkato ila tuu hazipitiki kwa ubovu. Njia hizi zikiboreshwa foleni ya dar itapungua kwa kiasi kikubwa.
kitu kingine ni kujenga flyovers kwenye makutano ya barabara kuu mambo hayo yakitendeka foleni itapungua sana hapa dar

Sina kinyongo na wakazi wa Kigamboni ila tatizo liko kwenye gharama ya Ujenzi wa hili Daraja ikilinganishwa na faida itakayopatikana kutokana na utumiaji wake, Je ni asilimia ngapi wa wakazi wa DSM watalitumia? Kwa maana jibu la hili swali ndiyo lilipaswa lihalalishe ujenzi wake!

Na sasa kwa kuwa wewe mwenyewe umefafanua hivyo kuhusu tatizo la foleni, ni kipi kingepaswa kianze je Daraja la Kigamboni au kujengwa na kuboreshwa kwanza kwa hizo barabara ulizozitaja?
 
Oh My God! Siwezi hata kufikiri kwamba kuna kiumbe anaye weza kuja na hoja kama hii. It's a total embassment. I thought hii forum ni ya Great Thinkers. What a waste of time!
Think about congestion ya traffic in the inner city. Think about mafuta yanayo potea bure kwenye hizo foleni, think about kuboresha sehemu zingine za jiji, think about maendeleo ya satellite cities, etc. Halafu eti unasemaje???

Mimi siyo Great thinker na wala sijawahi na sitowahi kujitambulisha hivyo ila kama wewe unaona unastahili kuitwa hivyo hiyo ni juu yako!

Haya niambie hili daraja litapunguza msongamano wa kiasi gani kwenye huu Mji? Ni asilimia ngapi ya wakazi wa Dar watalitumia kila siku kwenda na kurudi kazini ikilinganishwa na gharama iliyotumiwa kulijenga?
[/QUOTE]
yaani mpaka hapo hujaelewa tu? Kama unajitambua kuwa wewe siyo great thinker ni vema ukakaa kimya. Achana na kuanzisha mada wakati uwezo wako ni Kiduchu.

unataka akwambie nini wakati hata mada yako haioneshi ubaya ni upi? unaishia kukosoa bila kutoa ufafanuzi. Kwa heri
 
Dah! Hakika wewe unazidi kuonesha upuuzi wako. Labda nikueleze ni kwamba NSSF ni mfuko wa hifadhi ya jamii. Ni taasisi ambayo watu binafsi, mashirika ya umma na hata taasisi za serikali huitumia kwa ajili ya kuweka fedha zao ambazo huitwa mafao. Yapo mafao ya uzeeni, ulemavu, uzazi nk. Kwa kuwa fedha hizo ni nyingi, taasisi hiyo imekuwa ikijihusisha na uwekezaji kwenye miradi mbalimbali. Kwa maana hiyo, taasisi hiyo inafanya biashara kama wanavyofanya watu binafsi na wanatumia fedha za wanachama wao kama mtaji na dhamana katika biashara zao. Wanajenga majengo makubwa ya kibiashara, kuna mkakati pia wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme na kuiuzia TANESCO na huo mradi wa daraja la Kigamboni.

Kama hujui ni vema ukauliza ili ufahamushwe. Hivyo NSSF wanapowekeza kwenye miradi miradi hiyo si ya serikali. Ni mali ya NSSF
Waache kiherehere cha kupeleka pua zao kunusa wasivyostahili,wanajifanya wawekezaji na kuanza kupiga danadana wanachama wanaotaka mafao wakati hela hakuna wameinvest kwenye real estate ambayo inachukua more than 10 years to break even.
 
Daraja la kigamboni litasaidia ,ila manufaa yake yatakua partial tu(hapo ndio inaingia ishu ya why spend a lot of money )Kama watu wa dar hamtaki foleni inabidi kujengwe flyovers kwenye major junctions zote ,hapo sasa ndio manufaa ya matumizi ua hizo 200bn yatakapoonekana yana uzito.
 
Tufanye kahesabu kadooogo. 200,000,000,000 /500,000=400,000 Nadhani ni mradi fair tu ukizingatia na uwekezaji unaoendelea kigamboni sh laki nne kwa kila mwananchi inalipika kwa maisha ya daraja husika ie lifespan.

Hayo mahesabu yako yanasema nini? Ningekuomba ufanunue kama ukiweza kwa maana hesabu bila ya maelezo inabakia kuwa kama namba tu ambazo hazidasii sana!
 
Watu wanaobeza hili daraja itakua si watu ambao wamewahi kufika kigamboni na kuona usumbufu wa pale hasa kwa wenye magari
 
Gharama za daraja
Hayo mahesabu yako yanasema nini? Ningekuomba ufanunue kama ukiweza kwa maana hesabu bila ya maelezo inabakia kuwa kama namba tu ambazo hazidasii sana!
according to jamaa hapo juu ni 200bn ,idadi ya wakazi km 500,000 hivi kwa hiyo ukikokotoa naona kwa maisha ya daraja ni mradi ambao ni endelevu ukizingatia uwekezaji wa unaotaka kufanyika kigamboni pia nadhani watu wameangalia zaidi miaka ijayo na sio matumizi ya leo tu.
 
Oh My God! Siwezi hata kufikiri kwamba kuna kiumbe anaye weza kuja na hoja kama hii. It's a total embassment. I thought hii forum ni ya Great Thinkers. What a waste of time!

Think about congestion ya traffic in the inner city. Think about mafuta yanayo potea bure kwenye hizo foleni, think about kuboresha sehemu zingine za jiji, think about maendeleo ya satellite cities, etc. Halafu eti unasemaje???

Huku nadhani tumevamiwa na Akina kibajaj.
 
Mimi siyo Great thinker na wala sijawahi na sitowahi kujitambulisha hivyo ila kama wewe unaona unastahili kuitwa hivyo hiyo ni juu yako!

Haya niambie hili daraja litapunguza msongamano wa kiasi gani kwenye huu Mji? Ni asilimia ngapi ya wakazi wa Dar watalitumia kila siku kwenda na kurudi kazini ikilinganishwa na gharama iliyotumiwa kulijenga?
Hivi Watanzania tuna matatizo gani wajameni ?hivi mtu Kama huyu tumuweke fungu gani?[/QUOTE]

Daraja la kigamboni halikujengwa kwaajili ya kupunguza msongamano wa magari bali kuwezesha watu kuvuka kwa urahisi kwenda kigamboni na pia kuendeleza upande huo wa jiji la Dar.
 
Hoja yako imeegemea zaidi kukosoa zaidi ya kujenga ndo maana unasema halihitajiki daraja la kigamboni. Itakuwa ngumu kwa unaemkosoa kukusikiliza sababu ni kama vile una chuki au vivu mbaya. Watu wa aina yako ukipotezwa usijemlaumu yeyote maana hizi si zama zile. Kiongozi wetu ameonyesha njia na nia thabiti na tunamsupport bila kujali kama tulimkataa au la kwenye sanduku la kura maana sisi wananchi matakwa yetu ni maendeleo bila kujali ni chama au itikadi gani inaongoza nchi.

Mimi siko huko kwenye siasa bali niko kwenye kuangalia kama hili daraja lina manufaa ukilingansha na fedha zilizotumika!
 
Mimi siyo Great thinker na wala sijawahi na sitowahi kujitambulisha hivyo ila kama wewe unaona unastahili kuitwa hivyo hiyo ni juu yako!

Haya niambie hili daraja litapunguza msongamano wa kiasi gani kwenye huu Mji? Ni asilimia ngapi ya wakazi wa Dar watalitumia kila siku kwenda na kurudi kazini ikilinganishwa na gharama iliyotumiwa kulijenga?
yaani mpaka hapo hujaelewa tu? Kama unajitambua kuwa wewe siyo great thinker ni vema ukakaa kimya. Achana na kuanzisha mada wakati uwezo wako ni Kiduchu.

unataka akwambie nini wakati hata mada yako haioneshi ubaya ni upi? unaishia kukosoa bila kutoa ufafanuzi. Kwa heri[/QUOTE]

Kwani kulikuwa na ulazima gani wa wewe kuchangia mada yangu ambayo haieleweki?
 
Barbarosa

Wengi humu na dhani hawajaelewa hoja iliyopo mezani..
Mimi kwa maoni yangu hili daraja Lingekuja pale tuu Jiji litakapoweza kutatua tatizo la msongamano hasa kwenye makutano makuu,
hilo lingewezekana kwa kufungua barabara za michepuko ambazo kwa sasa ni mbovu kutupa, Lingine tungewekeza kwenye flyovers na Lamwisho huu mradi wa DART utasaidia sana kuondoa foleni ndani ya CBD..

Kihualisia hili daraja halitakua na effect yeyote kwenye kuondoa foleni ukizingatia Hatahao wakazi waKigamboni watavuka nakuja kukwama kwenye Foleni..
 
Unapoteza muda bure. Daraja linafunguliwa mwezi Machi wewe unajifanya kupinga sasa! Kichekesho kweli
 
Barbarosa

Wengi humu na dhani hawajaelewa hoja iliyopo mezani..
Mimi kwa maoni yangu hili daraja Lingekuja pale tuu Jiji litakapoweza kutatua tatizo la msongamano hasa kwenye makutano makuu,
hilo lingewezekana kwa kufungua barabara za michepuko ambazo kwa sasa ni mbovu kutupa, Lingine tungewekeza kwenye flyovers na Lamwisho huu mradi wa DART utasaidia sana kuondoa foleni ndani ya CBD..

Kihualisia hili daraja halitakua na effect yeyote kwenye kuondoa foleni ukizingatia Hatahao wakazi waKigamboni watavuka nakuja kukwama kwenye Foleni..

Msaidie Barbarosa kwamba unapokuja na challenge katika jambo kubwa kama hilo angalau jaza tafiti zako au mawazo ya ufafanuzi kwamba halina msaada kwa sababu hii na hii. yeye anaishia kuwaambia watu daraja halitakuwa na msaada kwa lipi? hakuna majibu.

Mawazo yako yako sawa lakini kumbuka mji wa Dar unapanuka sana kuelekea Kigamboni na maeneo mengine. Pia kumbuka plan ya kuujenga mji wa Kigamboni. Daraja la Kigamboni ni hatua mojawapo ya kuupanua mji wa Dar.maendeleo yote yanaenda kwa phase. huwezi subiri mlundikano ndio ufikirie kuweka miundombinu. mpango wa Fly overs, DART na upanuzi wa barabara zingine za ndani na nje ya Mji yote iende kwa wakati mmoja.

walioapanga bado wako Sahihi kabisa
 
Ngoja watanzania wenye uchungu na nchi yao waje. Naona mleta mada unawatania.
 
Oh My God! Siwezi hata kufikiri kwamba kuna kiumbe anaye weza kuja na hoja kama hii. It's a total embassment. I thought hii forum ni ya Great Thinkers. What a waste of time!

Think about congestion ya traffic in the inner city. Think about mafuta yanayo potea bure kwenye hizo foleni, think about kuboresha sehemu zingine za jiji, think about maendeleo ya satellite cities, etc. Halafu eti unasemaje???

wewe ndio huna unachoelewa, kiuchumi daraja la kigamboni sio kipaumbele chetu kabisa ni ujenzi wa sifa tu, kigamboni ina watu wangapi? na hata wao watu wakija mjini bado njia za mjini hazijaboreshhwa so foleni iko pale pale, kigamboni bridge is a white elephant project, period
 
watu wa kigamboni p
Hivi Watanzania tuna matatizo gani wajameni ?hivi mtu Kama huyu tumuweke fungu gani?

Daraja la kigamboni halikujengwa kwaajili ya kupunguza msongamano wa magari bali kuwezesha watu kuvuka kwa urahisi kwenda kigamboni na pia kuendeleza upande huo wa jiji la Dar.[/QUOTE]
watu wa kigamboni pigeni mbizi acheni mbwembwe za daraja
 
gharama inayotumika kujenga DART ilitosha kabisa kuweka mfumo wa METRO kwa sababu METRO nyingi duniani nchi zilizoendelea hazihitaji kuwavunjia watu majumba yao wala kulipa watu,zinapita juu ya barabara zetu tu ,hakuna njia rahisi ya usafiri kama TRAIN metro hizi nyingine zote porojo tu
Mkuu, labda tueleweshane, ni mji gani mkubwa duniani ambao unaufahamu ambao uko kando ya bahari kama Dar es Salaam wenye metro? Nafikiri tabia ya nchi, udongo na miamba una nafasi kubwa sana katika hilo la kujenga metro. Halafu huo umeme wa kuendesha hayo ma train hatunao bado. Labda unachosema wewe ni kwamba tuanze kwa kuangalia upper stream devlelopmental investments?
 
Back
Top Bottom