Daraja la Kigamboni lakusanya bilioni 83 tangu kufunguliwa 2016. Makusanyo yafikia 1.3B kwa mwezi

Bongo, sehemu serikali inatoza tozo wakikuambia kwa siku wanakusanya fedha milioni moja, inabidi uzidishe hicho kiasi mara mbili kisha ujumlishe na robo yake ili upate makusanyo halisi.
Na ndio uhalisia, mapato ya hilo daraja ni makubwa kutokana na movement ya magari iliyopo. Malori tu yanayopita kwenda kupakia mafuta yanaingiza hela nyingi sana.
 
Milioni 40 kwa magari yenye uzito mdogo kabisa ni 1500

40,000,000/1500=2,666

Hizo ni trips 2666 ambapo kama mtu anaishi Kigamboni anaenda na kurudi. Wastani wa magari yasiyozidi 1300 kwa siku, punguza na mabasi ambayo yanapita hapo siku nzima kwa kurudia rudia..

Nadhani inawezekana..
Mkuu hesabu za wapi hizo umepiga?
 
Gharama za ujenzi ni bilioni 200 plus ..
Kama limeingiza bilioni 83 ina maana nssf wanadai kama bilioni 120
Serikali ilipe deni ...hayo makusanyo yaende kwenye manispaa ya Kigamboni...
Kwamba wao walichangia kitu gani?

Kwamba hizo hela zisirudi na faida?

Kwamba hujui maana ya uwekezaji?
 
Daraja la Kigamboni ambalo linaunganisha mji wa Kigamboni limekusanya bilioni 83 kama tozo za kuvuka daraja kwa miaka saba iliyopita.Daraja la Kigamboni lilijengwa kwa gharama ya $ 135 bilioni(337.5 bilioni)na kuwa la aina yake Afrika Mashariki.

Daraja la Nyerere ni mradi wa pamoja kati ya Serikali na NSSF. Mkurugenzi wa NSSF, Masha Mshomba amesema kwasasa daraja hilo linakusanya wastani wa bilioni 1.2-1.3 ambayo ni kama milioni 41 kwa siku.

Pamoja na ombi la kujirudiarudia la mbunge wa Kigamboni kuomba wananchi wapite bure, jambo hilo liligonga mwamba baada ya Rais Samia kusema limejengwa kwa mkopo na lazima urejeshwe.
Unaijua usd 135 billions ndugu mtoa mada?
 
Back
Top Bottom