Wakazi wa Kigamboni watalipia daraja la Mwalimu Nyerere mpaka lini?

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
Kwa sababu za kijografia , Wilaya hii imekuwa na changamoto ya kufikika kwa urahisi na hivyo kwa miaka mingi wakazi wake wamekuwa wakitumia huduma ya kivuko cha ferry au kutumia njia ya Barabara ya Kongowe, njia ambazo zimekuwa na shida kwa wakazi.

Ujenzi huu ulianza ramsi Februari 2012 chini ya kampuni za China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company huku mbunifu wake ikiwa kampuni ya Arab Consulting Engineers. Kigamboni Bridge - Wikipedia

Mradi wa daraja la Nyerere lenye urefu wa mita 680, upana wa mita 32 ulizinduliwa na na kuanza kutumika rasmi tarehe 19 Aprili 2016 ambapo inakadiriwa kutumia kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 300 ,mradi unaomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania ( 40%) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF (60%). https://www.eatv.tv/news/current-affairs/gharama-daraja-la-kigamboni-zaongezeka-maradufu

Wazo la kujenga daraja la Nyerere lilionekana kuwa mkombozi kwa Wilaya hii katika Nyanja za kuboresha huduma, kupanua uchumi na kusogeza karibu huduma za kijamii na kupunguza gharama za maisha, badala yake imekuwa kero na mzigo kwa raia kutokana na tozo zake kuwa juu sana ambapo kwa wastani wa mtumiaji wa gari ndogo anakadiriwa kulipa kiasi cha Tsh. 3000 kwa siku , Tsh. 90,000 kwa mwezi, Tsh. 1,080,000 kwa mwaka, ambayo ni sawa na Tsh. Milioni 5 na laki nne kwa miaka mitano (5).

Taarifa iliyotolewa miaka mitano iliyopita na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara ilieleza kuwa Shirika limekusanya Sh. bilioni sita za tozo ya kivuko kwa miezi nane, kuanzia mwezi Mei 2016, hadi januari 2017, sawa na Tsh. 750M kwa mwezi. Daraja la Kigamboni laingiza bilioni 6 – Dar24

Aidha , Prof. Kahyarara alisema gharama za uendeshaji wa daraja hilo katika kipindi hicho ni jumla ya Sh. milioni 800 tu na kuongeza kuwa NSSF imemudu kuvuka lengo kwa wastani wa asilimia 20 kutokana na kutumia waajiriwa wake badala ya Wakala iliwa ni wastani wa Sh. Milioni 100 kwa mwezi. http://dar24.com/daraja-la-kigamboni-laingiza-bilioni-6/

Kwa mujibu wa takwimu hizi za miaka mitano iliyopita, ukitilia maanani kwamba Idadi ya watu imeongezeka , sambamba na Idadi ya magari kwa wastani daraja la Nyerere litakuwa limeingiza kiasi cha Tsh. Bilioni 9 kwa mwaka. Hivyo itakapofikia mwishoni mwa mwaka 2021, Mradi huu utakuwa umeingiza mapato ya kiasi cha Tsh Bilioni 54 toka kuanzishwa kwake. (2016-2021) huku matumizi yake yakiwa takribani Bilioni 7.2 kwa kipindi chote.

Kutokana na hali hii, na kwa kuwa mradi una uhai ( life span) ya miaka mia mbili 200, ni wazi kabisa Serikali na NSSF wapo katika nafasi nzuri ya kutengeneza faida bila kuwaumiza wakazi wa kigamboni na wananchi wengine wanaotumia daraja hilo.

Hivyo basi ni muda muafaka kwa Serikali na NSSF kukaa pamoja na kupitia viwango vya tozo vilivyopo na kuvishusha ili kuleta ahueni kwa Watanzania ambao wengi wao ni wanachama wa mifuko hii ambapo fedha zao zimetumika katika Uwekezaji, wengi ni walipa kodi wa Serikali na hivyo kustahili huduma kama wakazi wengine wanaoishi katika maeneno yenye madaraja na vivuko.

Fly overs zinatumika na watu wote bila malipo ya ziada, Madaraja ya Mikoani yanatumika bila tozo au masharti kwa watumiaji, kwa nini Kigamboni? Je Serikali haioni kwamba ni muda muafaka kupunguza tozo hizi ?


 
Bahati mbaya Wahusika wakuu ambao wangekujibia Maswali yako haya vyema kabisa hawako tena duniani na kwa Kupendana Kwao hata Vifo vyao navyo vilikuwa vya Kufuatana pia.
 
Kigamboni daraja lilijengwa kwa hela za wachangiaji wa nssf.. na ndio mradi pekee wa nssf unaoleta hela.. mingine mingi ya kifisadi.

Sasa nssf hawawez kukubali kuachia hela za darajani maana ndizo wanazitegemea kulipa mafao wastaafu
 
Kigamboni daraja lilijengwa kwa hela za wachangiaji wa nssf.. na ndio mradi pekee wa nssf unaoleta hela.. mingine mingi ya kifisadi.

Sasa nssf hawawez kukubali kuachia hela za darajani maana ndizo wanazitegemea kulipa mafao wastaafu
Hayo mafao wataanza kupewa robo kuanzia mwaka kesho
 
Tatizo la ujenzi wa hili daraja ni kuwa nssf ilitumia fedha za wastaafu hivyo lazima wazifidie. Ndiyo maana wanakusanya wenyewe fedha getini. Limegharimu fedha nyingi hivyo tutalipa mpaka tukome.
 
Tatizo la ujenzi wa hili daraja ni kuwa nssf ilitumia fedha za wastaafu hivyo lazima wazifidie. Ndiyo maana wanakusanya wenyewe fedha getini. Limegharimu fedha nyingi hivyo tutalipa mpaka tukome.
tayari tushakoma, watufungulie sasa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom