Dar: Watu wanne wa familia moja wafariki baada ya kuvuta hewa chafu ya jenereta

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Muliro.jpg


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la vifo vya watu wanne wa familia moja ambao wamepoteza maisha baada ya kuvuta hewa chafu ya moshi kutoka kwenye jenereta walilowasha ndani ya nyumba na baadae kulala

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema tukio hilo lililotokea tarehe 19. 04. 2023 maeneo ya Chang’ombe, Temeke, Jijini Dar es salaam.

Inaelezwa kuwasiku moja kabla Saa 4:00 Usiku watu hao waliwasha jenereta baada ya umeme kuzimika na kuliweka ndani ya nyumba.

Kamanda Muliro amesema Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watu hao walipoteza maisha baada ya kuvuta hewa inayodaiwa kuwa ni hewa chafu ya moshi iliyokuwa inatoka kwenye jenereta baada ya kuwashwa.

Waliopoteza maisha ni Kazija Mohamed (21), Munir Ibrahim (7), Munira Ibrahim (6) Muyyat Ibrahim (3).

Mume na mke ambao ni Ibrahim Juma (28) na Aisha Ayubu (29) wote wakazi wa Kilimahewa, Chang’ombe hali zao sio nzuri na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kwa kushirikiana na mamlaka zingine.

---

Pia soma - Tukio la ndugu wa Familia kufariki kwa moshi wa jenereta, ndugu adai marehemu walipigwa kabla ya vifo vyao
 
Watu wengi wanajua kuvuta hewa chafu ni ushuzi, harufu ya kinyesi au uvundo na uozo fulani kumbe hewa chafu ni hewa safi inapokosekana na hewa chafu kama kuungua kwa mkaa ndani ya chumba kidogo hufanya mzunguko wa hewa safi kuingi na mtu kuishia kuishia kuvuta hewa iliyochafuka kwa carbonmonoxide na kuishia kupoteza maisha. Kuungua mkaa ndani ya nyumba hukuu madidirisha na milango ikiwa imefungwa ni hatari sana
 
Back
Top Bottom