BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili watumishi 16 wakiwemo wahasibu wa Jiji la Dar es Salaam umedai upelelezi umekamilika wanaandaa taarifa kwa ajili ya kuituma Mahakama Kuu.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 143 likiwemo la kuisababishia hasara jiji hilo zaidi ya Sh8.9 bilioni.
Wakili Serikali, Pendo Temu alidai mbele ya Hakimu Mkazi kisutu Pamela Mazengo wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo wanaandaa taarifa kwa ajili ya kuituma mahakama kuu hivyo ameiomba mahakama hiyo ipange tarehe ya kutajwa.
"Upelelezi umekamilika wapo kwenye mchakato wa kuandaa taarifa kwa ajili ya kuituma Mahakama Kuu," amedai Temu.
Washtakiwa hao ni Tulusubya Kamalamo, James Bangi ambao ni wahazini, Mohamed Khars, Abdallah Mlwale na Deogratias Lutatuza na Alinanuswe Mwakasumbe ni wahasibu pamoja na Judica Ngowo ambaye ni karani wa fedha.
Wengine ni Febronia Nagwa, Glory Eugen, Said Bakari, Josephine Sandewa, Dorica Gwihala, Jesca Lugonzibwa, Patrick Chibwana ambao ni wahasibu, Patrick Chubwana Ofisa Afya , Ally Baruan meneja na Khalid Nyakamande Afisa mtendaji wa mtaa.
Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Julai Mosi, 2019 na Juni 30, 2021 jijini Dar es Salaam washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji wa fedha na kujipatia kiasi cha Sh8.9 bilioni mali ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 11, 2023 kwa ajili ya kutajwa.
MWANANCHI