Upelelezi kesi aliyekuwa mkurugenzi TPA wakamilika

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,370
8,107
Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA), Madeni Kipande na wenzake umedai kuwa upelelezi umekamilika na wapo kwenye hatua ya kuwasilisha nyaraka katika Mahakama Kuu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh4.2 bilioni.

Wakili wa Serikali, Mosie Kaima alidai mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Kisitu, Ramadhani Rugemarila kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake umekamilika.

"Upelelezi umekamilika tupo kwenye hatua ya kuwasilisha nyaraka Mahakama Kuu, hivyo tunaiomba mahakama hii ipange tarehe nyingine kwa ajili kutajwa," alidai Kaima.

Baada ya maelezo hayo hakimu Rugemarila aliahirisha shauri hilo Machi 27, 2023 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Mbali na Kipande washtakiwa wengine ni Peter Gawile (58) Ofisa Rasilimali Watu wa TPA, Casmily Lujegi (65) Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi wa TPA, Mashaka Kisanta (59) Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi na Kilian Chale (51) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Mkazi wa Mbezi Makabe.

Inadaiwa kati ya Oktoba Mosi, 2014 na Oktoba Mosi 2020 jijini Dar es Salaam, walikula njama na kuisababishia TPA hasara ya Sh4.2 bilioni.

Inadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2015 hadi Februari 17, 2015 washtakiwa wakiwa maofisa wa TPA, walitumia madaraka yao vibaya kwa kutangaza zabuni namba AE/016/2014-15/CTB/G/39 kwa nia ya kujipatia dola za Marekani 1,857,908.04 .

Kati ya Oktoba Mosi 2014 na Oktoba Mosi, 2020 maeneo ya TPA na maeneo mengine ya Dar es Salaam, washitakiwa kwa makusudi walitangaza zabuni ya Enterprises Planning Resources (ERP).

Inadaiwa walitangaza zabuni hiyo, bila kupata kibali cha bodi ya zabuni ya mamlaka hiyo na kushindwa kufuata kanuni za zabuni hivyo kutoa malipo ya awali ya asilimia 40 bila idhini ya bodi hiyo jambo lililosababisha TPA hasara ya Dola za Marekani milioni 1.8 sawa na zaidi ya Sh4.2 bilioni.

MWANANCHI
 
Eeh! Kumbe inawezekana mbona upelelezi umechukua miaka mingi hivyo?
 
Mbona watu wengine wamepiga hela nyingi sana zaidi ya hizo lakini wapo nje wanakula bata tu.
 
Back
Top Bottom