DAR: TANESCO mnachotufanyia mtatuunguzia vitu

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Sijui kuna tatizo gani, lakini leo Ijumaa Septemba 8, 2023, huku ninakoishi maeneo ya Kilungule A, Kimara, Dar es Salaam, umeme umekatika zaidi ya mara nane.

Tangu asubuhi Tanesco wanafanya zoezi la kukata na kuwasha umeme, sijui wana mpango wa kutuunguzia vitu vyetu ambavyo tumenunua kwa kukopa.

Kama kuna tatizo tuambiwe lakini hili la umeme unakatika, unakaa nusu saa au dakika kumi unarudi, kisha baada ya saa tatu au nne unakatika tena, si sawa.

Hebu fikiria, kama usiku huu pekee kuanzia saa 1 hadi saa 3, umeme umekatika mara tatu na kurudi si chini ya dakika kumi.

Pia, soma Kero: TANESCO Mtwara wanakata kata umeme ovyo!
 
TANESCO wapumbavu Mbezi mwisho wamekata toka saa 11 jioni mpaka mda hawajarudisha pumbavu zao
 
TANESCO wapumbavu Mbezi mwisho wamekata toka saa 11 jioni mpaka mda hawajarudisha pumbavu zao
bora huko mkuu ni masaa tu... Shinyanga ni siku 3 mpaka 4... Au wanakata saa 3 asubuh wanawasha saa 7 usiku... Wenye biashara zinazotegemea umeme tutashika majembe mwezi wa 9 huu...
 
Back
Top Bottom