Dar: Simba 0 - 1 Yanga, Ngao ya hisani | Benjamin Mkapa

Insigne

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
3,642
2,000
Asalaam Aleykum Dar es Salaam
Asalaam Aleykum Tanzania
Asalaam Aleykum Afrika Mashariki na kati
Asalaam Aleykum Afrika kwa jumla.

Ni katika Derby ya kariakoo Simba na Yanga watani wa jadi hawa ni leo hii ya tar. 25.9.2021 majira ya saa 11:00 jioni nyasi za uwanja wa Mkapa zitashuhudia mpambano mkali kati ya wababe hao wa Tanzania na Afrika Mashariki na kati ni mchezo wa ngao ya hisani na ikiwa na maana ya ufunguzi rasmi wa mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara katika msimu wa 2021/2022.

Tangu kuanzishwa kwa kombe la ngao ya jamii 2010, Simba wana rekodi ya kuchukua kombe hilo mara 6 ambapo walichukua mwaka 2011,2012,2017,2018,2019 na 2020 ikiwa wamechukua kombe hilo mara 4 mfululizo, je wataweza kuendeleza ubabe wao katika kombe hilo la ufunguzi wa ligi.

Yanga pia wana rekodi ya kuchukua kombe hilo mara 5 ambapo wamechukua mwaka 2010, 2013, 2014, 2015, 2016 ikiwa pia wana hiyo rekodi ya kuchukua mara nne mfulilizo kabla ya simba kuiweka.

Vikosi vyote viwili vya simba na Yanga vikiwa na sura mpya katika timu zao kwa upande wa Yanga kuna Makambo, Aucho Khalid, fiston Mayele, djuma Shaaban, djigui Diarra, Moloko na wengine wengi

Pia simba kuna Sakho, kanoute, Banda, Duncan Nyoni, kibu deniss na wengine wengi.

Niko hapa kukuletea matangazo ya moja kwa moja kutoka uwanja wa Taifa katika mtanangane huu wa kibabe sana, nani kuibuka mshindi katika mechi hii?, tusubiri tuone

Ahsante sana wananchi tuliokuwa pamoja kuanzia mwanzo hadi mwisho wa matangazo haya ya moja kwa moja

Tukutane wakati mwingine tena

Asalaam Aleykum

===========

Simba Vs Yanga.JPG

Simba Vs Yanga

00' Mpira umeanza uwanja wa Benjamini Mkapa na Yanga wanapata kona ya mapema kabisa

01' Mugalu anapiga shuti kali kutoka nje ya 18' lakini linapaa juu

03' Kibwana Shomari anawekwa chini na Shomari Kapombe, mpira wa adhabu unakosa faida kwa Yanga

04' Yanga wanapiga pasi safi kuelekea lango la Simba, Pachal Wawa anatibua mpango wao

07' Simba wanapata kona ya kwanza, zinatokea piga nikupige langoni mwa Yanga bila goli

09' Wawa analamba kadi ya njano kwa kumuweka chini Fisto Mayele, mpira wa faulo unaishia mikononi mwa Aishi Manula

11' ⚽ Goaaaaaal, Fisto Mayele anaindikia Yanga bao la kwanza kwa kutandika mkwaju mkwali na kumshinda Aishi Manula

Fisto Mayele Goal Yanga Vs Simba.JPG

Fisto Mayele akishangilia bao la kuongoza kwa Yanga dhidi ya Simba

14' Hassan Dilunga anaachia mkwaju mkali kuelekea lango la Yanga lakini unaishia kwenye nyavu za pembeni

18' Yanga wanapata kona, inaishia mikononi kwa Aishi Manula

32' Bangala anaachia mkwaju mkali kuelekea Simba lakini unapaa juuu

46' Shomari Kapombe anapewa kadi ya njano

45+2' Mpira unaenda mapumziko, Simba 0-1 Yanga

=======

45' Mpira unarejea kutoka mapumziko, Simba inaongeza mshambuliaji kwa kuingia John Bocco nafasi ya Hassan Dilunga anaeenda bench

48' Chriss Mugalu anapata nafasi nzuri kusawazisha, anapiga nje ya lango, Simba 0-1 Yanga

57' Simba wanafanya shambulizi, Mugalu anaukosa na Diarra anasimama imara kuuweka mpira kwenye himaya yake

58' Bangala anapewa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Kanoute

61' Mabadiliko, Yacouba anaingia kuchukua nafasi ya Farid Mussa

62' Peter Banda anaingia kwa upande wa Simba

65' Thadeo Lwanga anapewa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Feisal Salum

69' Makambo anaingia kuchukua nafasi ya Fisto Mayele

70' Feisal Salum anamjaribu Aishi Manula kutoka nje ya 18' na Aishi Manula anasimama imara kuupangua

72' Mpira wa burudani unachezwa uwanja wa Taifa na timu zote zinashambuliana kwa zamu

76' Diarra yuko chini akigaagaa baada ya kichwa kugonga mlingoti akijaribu kuufata mpira

Simba Vs Yanga.JPG

Feisal Salum akiwa kwenye msitu wa wachezaji wa Simba

86' Mwenda anaingia kuchukua nafasi ya mohammed Hussein Tshabalala

88' Bwalya anapiga mkwaju wa faulo na Diarra anafanikiwa kuupangua

90+1 🟥Thadeo Lwanga anapewa kadi ya pili ya njano baada ya kumzuia Feisal Salum

90+3' Yacouba anapewa kadi ya njano

90+4' Kipyenga kinapulizwa kuashiria mwisho wa mchezo, Simba 0-1 Yanga

Yanga inashinda mechi ya ngao ya Jamii kwa kuitandika Simba SC bao 0-1 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Simba Vs Yanga.JPG

Yanga wakishangilia kutwaa ngao ya jamii dhidi ya Simba​
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom