Dar: Sakata la kuibwa mtoto Hospitali ya Temeke

Life.co.tz

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
639
368
Husika na kichwa cha Habari hapo juu.. Leo ktk kupindi cha Pb cha Clouds Fm,palikuwepo na wageni.

Mama Aliedai kujifungua mapacha mwishowe kaambulia kupewa moja wakike baada ya vigisuvigisu nyingi.

Binti huyo aliongozana kwenda hapo Clouds Fm akiwa na Huyo mtoto wake mdogo,Mama yake mzazi(Bibi ya Kitoto) pamoja na Msemaji wa Familia.

Story niya kusisimuha haswa. Na kwamaelezo ya Binti yaonyesha alikuwa na Mimba ya mapacha kwani Ultra Sound alizofanyiwa zaidi ya mara 4 zinaonyesha ni Mapacha.

Mchezo mchafu umekuja anzia Temeke Hospital ambapo aliambiwa aende kwa uchunguzi zaidi ndipo ilipobainika Ujauzito ni wa Mapacha unamiezi 9 na mtoto moja amekaa vibaya hivyo afanyiwe.

Kiufupi baada ya oparesheni Mama mzazi kakabidhiwa mtoto moja wa kike.Bwana na Mama aliejifungua washaripoti mpaka kwa Naibu Waziri.

Tume imeundwa tatizo Wahanga watukio hawajaonana na tume hiyo...pia wanasikia tume imesha maliza kazi.

Na wamesikia baadhi ya vielelezo na picha mbalimbali za Ultra Sound toka Hosptal tangia huki mwanzo havionekani.

KWA JINSI NILIVYOISIKILIZA STORI NIKIJARIBU KUUNGA DOT.HII SKENDO SOON UKWELI UTAPATIKA NA NI YAKIIBUKA MTANIELEWA[/....Nawakilisha..
 
nimeisikia asubuhi kutka clouds lakini sikujua ni mkasa gani, nilidhani ni wa zamani, kumbe ni siku za karibuni, nimesikiliza maneno yote ya yule dada aliyekumbwa na hili tukio kamtaja dr. Elisha,
 
Husika na kichwa cha Habari hapo juu.. Leo ktk kupindi cha Pb cha Clouds Fm,palikuwepo na wageni.
Mama Aliedai kujifungua mapacha mwishowe kaambulia kupewa moja wakike baada ya vigisuvigisu nyingi..
Binti huyo aliongozana kwenda hapo Clouds Fm akiwa na Huyo mtoto wake mdogo,Mama yake mzazi(Bibi ya Kitoto) pamoja na Msemaji wa Familia...
Story niya kusisimuha haswa.. Na kwamaelezo ya Binti yaonyesha alikuwa na Mimba ya mapacha kwani Ultra Sound alizofanyiwa zaidi ya mara 4 zinaonyesha ni Mapacha...
Mchezo mchafu umekuja anzia Temeke Hospital ambapo aliambiwa aende kwa uchunguzi zaidi....ndipo ilipobainika Ujauzito ni wa Mapacha..unamiezi 9...na mtoto moja amekaa vibaya hivyo afanyiwe. ..
Kiufupi baada ya oparesheni Mama mzazi kakabidhiwa mtoto moja wa kike...
Bwana na Mama aliejifungua washaripoti mpaka kwa Naibu Waziri...
Tume imeundwa tatizo Wahanga watukio hawajaonana na tume hiyo...pia wanasikia tume imesha maliza kazi...
Na wamesikia baadhi ya vielelezo na picha mbalimbali za Ultra Sound toka Hosptal tangia huki mwanzo havionekani....
KWA JINSI NILIVYOISIKILIZA STORI NIKIJARIBU KUUNGA DOT....HII SKENDO SOON UKWELI UTAPATIKA NA NI YAKIIBUKA MTANIELEWA[/....Nawakilisha..
nadhani soon milard ayo ataiweka
 
Dr. Wa kike aliye mfanyia operation Dada huyo anasiri fulani kutokana na mazingira, maneno, mshiriki wake mgeni ktk chumba cha upaasuaji. ingefaa achunguzwe kwa makini sana atatoa utata!
 
Inauma sana kutojua mwanao halipo
Sio kutojua mkuu, kujua kuwa hapo ulipo mwanao watu walisha mchemsha kwenye chungu mpaka mafuta yakaja juu, wakachukua kwenda kuwauzia wazee wa mafuta ya upako, halafu supu wakanywa, na halafu mifupa wakaanika na kuisaga kwa ajili ya wazee wa hirizi za utajiri,
 
Ultrasound is operator dependent
Ok nilikuwa cjui hilo....
Ajabu nikwamba wakati wa oparesheni hawakumpiga ile sindano ya Nusu Kaputi..
So mpaka wanawatoa Watoto alikuwa anawasikia..Dr Moja akasema ""heee Tupo Tuwiliii""
Mama Mzazi akasikia Dr Mwanamke anasema 'acha kelele endelea na kazi'''
Ndipo alipochomwa nusu kaputi....
Kuja kushtuka kakaBidhiwa mtoto moja.
 
Waungwana mmenifungua akili. Lakini ultrasound haiwezi kukosea? Uko hivi: make wangu pia aliandikiwa na daktari kuwa ana mapacha (kadi hadi leo ipo). Alipopasuliwa nilipewa mtoto mmoja. Kisha nikaambiwa aloandika hakupima vizuri. Ndo maana nauliza mashine hii haiwezi kukosea? Naomba nijifunze.
 
Waungwana mmenifungua akili. Lakini ultrasound haiwezi kukosea? Uko hivi: make wangu pia aliandikiwa na daktari kuwa ana mapacha (kadi hadi leo ipo). Alipopasuliwa nilipewa mtoto mmoja. Kisha nikaambiwa aloandika hakupima vizuri. Ndo maana nauliza mashine hii haiwezi kukosea? Naomba nijifunze.

Ukipiga ultra sound huwezi kukosea. Miguu inaonaka minne, vuchwa viwili, wanaona mpaka jinsia zao ukitaka wanakwambia ni wa kike au wa kiume. Kwa ufupi kusema ultra sound imekosea tena baada ya kupigwa kwa kurudia mara nne sio sahihi. Napata picha hii issue aishikie Mheshimiwa Rais wetu kuna moto utawaka hapo.........maana naona hawa wengine kama wana kigugumizi hivi........
 
Waungwana mmenifungua akili. Lakini ultrasound haiwezi kukosea? Uko hivi: make wangu pia aliandikiwa na daktari kuwa ana mapacha (kadi hadi leo ipo). Alipopasuliwa nilipewa mtoto mmoja. Kisha nikaambiwa aloandika hakupima vizuri. Ndo maana nauliza mashine hii haiwezi kukosea? Naomba nijifunze.
Ultrasound inategemeana na anayeioperate ana uzoefu kiasi gani, maana wanaweza wakapima kitu tumbani watatu tofauti kila mmoja akawa na majibu yake ndio maana inahitaji operator mzoefu sio anayejifunza

Kwa hiyo huyo mama kusema alicheck ultrasound akaambiwa ana mapacha sio kigezo tena mara nyingi siku hizi wanacheck ultrasound kwenye vizahanati vya private ambavyo vingi vyake havina wataalamu wa kutumia Mashine vzr wao wanaangalia hela tu

Niko kwenye medical field kwa miaka 5, wakinamama kadhaa walishawahi kuja wakisema wameambiwa zahanati wana mapacha lakini ukipima unakuta mmoja Hata kwa wale ambao tunaowafanyia operation ( ceaserian section) unakuta mtoto mmoja

Pointi yake angesema amewaona wote wametolewa after operation hapo yungemuelewa maana mara nyingi wanapewa dawa ya usingizi ya spine ambapo unaweza kuongea nae na anaona kila kitu
 
Waungwana mmenifungua akili. Lakini ultrasound haiwezi kukosea? Uko hivi: make wangu pia aliandikiwa na daktari kuwa ana mapacha (kadi hadi leo ipo). Alipopasuliwa nilipewa mtoto mmoja. Kisha nikaambiwa aloandika hakupima vizuri. Ndo maana nauliza mashine hii haiwezi kukosea? Naomba nijifunze.
Nawewe walikufanyia mchezo mchafu....uyo dada alipima utrasound zaidi ya mara moja na zote zikaonyesha ni mapacha
 
Acheni udaku tafuteni ukweli
....

ULTRA SOUND YAWEZA KUKOSEA.

PACHA MMOJA AWEZA KUFIA TUMBONI NA KUNYONYWA HUMO HUMO NDANI YA TUMBO

MAMA MJA MZITO AWEZA KUWA NA KICHAA CHA UJAUZITO

N.K
Hao clouds ni vilaza tu ..
yuko daktari MD wanashindwa kumuuliza juu ya kurusha stories za namna hiyo....kama mtoto kaibiwa hiyo ni jinai na sehemu ya kisheria ni kwenda polisi sio clouds.

Tuache Udaku...Taifa limeathiriwa na Udaku
 
Back
Top Bottom