Kesi ya Ubakaji Temeke: Mtoto atoa ushahidi jinsi Ostadhi Shabani alivyomuingizia dudu la kukojolea kwenye bibi yake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
MWANAFUNZI wa Darasa la tatu mwenye umri wa miaka tisa( jina linahifadhiwa), amedai amekuwa akibakwa na mwalimu wa madrasa mara nyingi baada ya mafunzo ya dini.

Amedai amekuwa akiingizwa dudu lake la kukojolea kwenye uchi wake wa kukojolea (kwa bibi) na mwalimu huyo kisha anampatia biskuti ili asije kusema.

Shahidi huyo ambaye anasoma shule ya msingi Uwanja wa Ndege, Dar es Salaam, alidai hayo katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke, mbele ya Hakimu Mkazi Anna Mpessa, wakati akitoa ushahidi wa kesi ya ubakaji inayomkabili Shaban Hamid(22).

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Cecilia Mkonongo, Shahidi huyo alidai baada ya kutoka shuleni saa nane mchana anakwenda nyumbani anakula chakula kisha anakwenda madrasa na mtoto wa shangazi yake ambaye anasoma chekechea.

Shahidi huyo alidai wakifika chuo cha dini wanafundishwa na hostazi Shabani wakiwa na watoto wengine ambapo baada ya mafundisho anawaambia watoto wengine waondoke wabaki yeye na mwenzake kwa ajili ya kukusanya mikeka.

" Hostazi Shabani anatufundisha sisi na watoto wengine alafu baadaye anatwambie tubaki mimi na mwenzangu tukusanye mikeka kisha ananibaka wakati huo mwenzangu anakuwa pembeni akinimaliza nae anambaka. Anakuwa ananivua nguo yangu namwambia sitaki sitaki làkini ananivua hadi chupi mpaka chini naye anavua suruali yake pamoja na boksa kisha ananiambia nilale chini alafu yeye analala juu yangu," alidai.

" Baada ya kusikia mama anaongea na shangazi kuhusu habari za ubakaji ndipo namimi nikamwambia kwamba Hostazi uwa anatubaka mimi na mwenzangu," alidai.

Shahidi huyo alidai baada ya kumwambia mama yake alimchukua na kumpeleka hospitalini kisha walimpima.

Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wa kesi hiyo, Hakimu Anna alisema hati ya kumkamata mshitakiwa imetolewa baada ya kuruka dhamana ambapo kesi hiyo ilisikilizwa pasipokuwepo mshitakiwa.

Mshitakiwa inadaiwa alitenda kosa hilo kati ya Desemba mwaka 2019 na Februari mwaka jana eneo la Yombo Lumo, Dar es Salaam ambapo alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka tisa( jina linahifadhiwa)

Hakimu Anna iliahirishwa hadi Mei 11
 
Huu utaratibu wa hizi madrasa uangaliwe upya ubakaji wa watoto umezidi sana huyu mhusika lazima ale mvua ya 30

Lakini tatizo litabaki palepale lazima mbinu mpya za ufundishaji madrasa zibuniwe ili kukomesha hili tatizo kama pawepo wasimamizi wengine wa jinsi zote, mwisho wa kutoka watoto iwe saa 12, na wachukuliwe na walezi wao mikeka akusanye mwl wao nk
 
Back
Top Bottom