Dar: Polisi wakamata kiwanda cha kutengeneza noti bandia huko Chanika, Ving'ora vyapigwa Marufuku

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,981
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA MITAMBO YA KUTENGENEZEA NOTI BANDIA, WATUHUMIWA 4 NA NOTI BANDIA ZA MATAIFA MBALIMBALI.
1576751011449.png


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Benki kuu ya Tanzania (BOT), mnamo tarehe 15.12.2019 majira ya saa kumi na nusu jioni huko maeneo ya Chanika Zingiziwa Mkoa wa Kipolisi Ilala tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa aitwaye MASUMBUKO PAULO, mkazi wa Chanika, uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini mtandao mzima au washirika wake. akiwa mtuhumiwa alikamatwa akimiliki kiwanda cha kutengenezea noti bandia za Tanzania na mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Marekani (USD), Demokrasia ya Congo (DRC Francs), Msumbiji (Meticais), Malawi, Zambia (Kwacha), Botswana (Botswana pula BWP) na Kenya(Ksh).

Noti bandia walizokutwa nazo ni kama ifuatavyo;

(1) Noti bandia 10357 za Tsh 10,000/= sawa na Tsh 103,570,000 kama zingekuwa halali.

(2) Noti bandia 534 za Tsh 2,000 sawa na Tsh 106,800/= kama zingekuwa halali.

(3) Noti bandia 9000 za Tsh 5,000 sawa na Tsh 45,000,000/= kama zingekuwa halali.

(4) Noti bandia 823 za Tsh 10,000 sawa na Tsh 8,230,000/=kama zingekuwa halali.

(5) Noti bandia USD 133,048 za kimarekani sawa na Tsh 304,679,920 kwa rate ya 2290 ya kubadilisha fedha kama zingekuwa halali.

(6) Noti bandia 16,523 za Msumbiji (Melticais) zenye thamani ya Melticais 13,011,500 kama zingekuwa halali.

(7) Noti bandia 2270 za DRC (francs) zenye thamani ya kwacha 7,592,000 kama zingekuwa halali.

(8) Noti bandia 1 ya shilingi ya Kenya yenye thamani ya Ksh 200 kama ingekuwa halali.

(9) Noti bandia 1 ya Kwacha 500 ya Malawi

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama tunaendelea na msako mkali ili kutokomeza uhalifu huu mbaya ambao unaathiri uchumi wa nchi.
Watuhumiwa wanaendelewa kuhojiwa na kuandaliwa mashtaka na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali na utaratibu utakapokamilika watapelekwa mahakamani.

JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU UTUMIAJI HOLELA WA VING’ORA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limebaini kuwa ving’ora vinatumika katika magari na pikipiki barabarani kinyume cha sheria ya usalama barabarani.

Ifahamike kuwa ving’ora vinapaswa kutumika katika magari au pikipiki zinazoongoza misafara ya viongozi (Oficial Motorcades) ni kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani sura ya 168 ya mwaka 1973 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 kifungu cha 39 B(I) na (2) kinafafanua juu ya matrumizi ya ishara ikiwepo ving’ora na vimulimuli.
kifungu cha 54(1), (2), (3), (4) na (5) vinaeleza mazingira, matumizi ya vimulimuli na ving’ora na wanaoruhusiwa kufunga ving’ora, vimulimuli na kuvitumia kutoa ishara za tahadhari na watumiaji wengine kupaswa kuwapisha au kuwapa kipaumbele.

Wanaoruhusiwa kutumia ving’ora na vimulimuli kwa mujibu wa sheria hiyo ni magari ya dharura ambayo ni ya polisi,majeshi ya ulinzi,zimamoto na uokoaji, magari ya kubeba wagonjwa na magari mengine au matela ambayo yamepata kibali kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi na kutangazwa kwenye gazeti la serikali.

Kutokana na kukiukwa kwa matumizi ya ving’ora jeshi la Polisi linapiga marufuku kwa wamiliki wa magari na pikipiki kwani imekuwa kero na kuwachanganya madereva na watumiaji wengine wa barabara kushindwa kubainisha upi msafara wa viongozi na mgari ya dharura.

Aidha jeshi la Polisi kuanzia leo litayakamata magari na pikipiki zinazotumia ving’ora kinyume cha sheria kupitia tarifa hii waliofunga vingo’ora wanatakiwa kuviondoa haraka iwezekavyo watii sheria bila shuruti.

TAHADHARI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR ES SALAAM.
Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linapenda kutoa tahadhari kwa wakazi wa jiji la Dsm wote kuwa makini kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepukana na majanga yanayoweza kuepukika.

Hivyo wananchi wote wanatakiwa kuwa makini na watoto wadogo wanaohitaji uangalizi wa karibu, pia kujiepusha kupita kwenye maji ya mito midogomidogo au madimbwi ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wao.

LAZARO B. MAMBOSASA – SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
17.12.2019
 
mambo ya police kupiga marufuku ni ya kishamba sana... viongozi wapige marufuku then police wasimamie.... hii nchi inaendeshwa kirai na si military regime..et police imepiga marufuku kama nani wanapiga marufuku? viongozi kemeeni hzo mambo.
 
Nilitegema kukuta habari hii kwa kina hapa JF maana ITV wameionyesa kwa kimafumbo....kumbe hata hapa hivohivo, ila anagalau hapa wameweka jina la mtuhumiwa na kiasi cha fedha...ITV hata vifaa vya kutengeneza fedha wamevionyesha kidogo tu!
 
1576691010920.png


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Benki kuu ya Tanzania linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumiliki mitambo ya kutengeneza noti bandia na kukutwa na fedha bandia za Tanzania na mataifa mengine zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Mia Sita.


Akizungumza Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa onyo kwa wote wanaojihusisha na biashara hiyo kwani wanahujumu uchumi wa nchi na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

"Alikuwa anaendesha kiwanda mtaangalia mitambo ntawaonyesha mitambo ambayo iliendelea kutumika wakati wa kutengenezea pesa hizo haramu, ukiangalia amejificha pembezoni kabisa anaelewa Operasheni za katikati ya Jiji zinavyoendelea," alisema Mambosasa.
 
Back
Top Bottom