Madame B
JF-Expert Member
- Apr 9, 2012
- 31,841
- 37,579
Kuna mwaka fulani nilipanga chumba Mbagala.Hata ukiwa na mshahara mdogo dar unaishi
...Dar kuishi ni kwa ku2mia akili tu
Asubuhi:Mihogo ya 500 na maji ya kandoro au ya bombs 50
Mchana:unaenda maeneo ya karibu na chuo wali wa buku shazii au kutokana na jinsi ulivyoshiba asubh kwa ile mihogo ya 500 iliyoliwa Saa 5 unaweza ukapiga pass ndefu
Jioni:unaweza piga chapati au ugali na dagaa maximum 1000 au 1500 au ukala vichwa vya kuku na miguu yake ..... usiku mwema kimya unapita nao!yani kwa Siku unaweza tumia 2500 tu.....I Love Dar na nimepamiss naamn nitarudi tu....
Aisee....kweli Dar ni kitonga.
Asubuhi napiga zangu skonzi 3 sh 300 na chai sh 100
Mchana napiga ugali 500 na utumbo wa kuku wa 300 na maji ya kunywa glasi 100
Usiku naenda pale stand Rangi tatu napiga wali harage na samaki kwa 1500 na maji ya uhai ya 500
Nikifika kitandani napiga hesabu jumla nimetumia sh 3300/=
Asubuhi Aluta Continua.
Siku nikipewa ofa naagiza kuku nusu, nusu nakula, nusu nafunga....naenda kuunga mchuzi nyumbani wa mchana na usiku.
Afu ndo mtu ananiambia nihame Dar.
Tutabanana hapahapa.
We ukila kuku nusu...nami nikila miguu na vichwa, wote tumemla kuku.
Ladha ileile.