Dar es Salaam ni jiji la wanafunzi Vilaza

Dar es Salaam ni jiji la wanafunzi Vilaza

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
38,845
Reaction score
90,306
DAR ES SALAAM NI JIJI LA VILAZA.

Na, Robert Heriel.


Sijawahi kuona wanafunzi vilaza kama wa Mkoa wa Dar es salaam. Wanafunzi wa Dar es salaam ni vilaza hujapata kuona popote dunia hii. Ni vilaza ambao hawajawahi kutokea tangu kuumbwa kwa dunia. Wapende wasipende. Huo ndio ukweli. Ninyi ni Vilaza tena wa kutupa. Mnalitia taifa aibu kwa sifuri zenu.

Unajua maana ya mwanafunzi kilaza?
Ipo hivi; Kilaza ni mwanafunzi ambaye uwezo wake wa akili ni mdogo hata umuwekee mazingira wezeshi bado atabaki kuwa na uwezo mdogo.

Kwa maana hiyo na nyinginezo zinalifanya jiji la Dar es salaam kuwa jiji la Vilaza waliotukuka.

Haiwezekani jiji kubwa hapa nchini lenye miundombinu yenye unafuu bado lishindwe hata kuwa top ten ya mikoa. Mbaya zaidi ndilo linaloongoza kwa sifuri zilizotukuka. Huo ni ukilaza.
Wala hatuna muda wa kuongea maneno matamu katika hili. Yaani usome Dar es salaam bado upate sifuri wewe ni kiazi mbatata.

Dar es salaam karibu kila nyumba inaumeme. Nini kinafanya watoto wasisome mpaka wapate sifuri kama sio vichwa viazi. Iko hivi. Kama mtoto sio kiazi basi mlezi ndiye kiazi. Mtoto apate sifuri ilhali kuna umeme. Anapataje sifuri kwa mfano kama sio uzembe. Na uzembe ndio ukilaza wenyewe huo.

Watoto wanshindwa kuamka usiku wa manane kusoma? Haya hata wazazi wanashindwa kuwaamsha hao watoto kama wao wenyewe hawajitambui? Usijesema kuna kelele. Hiyo sio kweli. Mji wa Dar es salaam unaanza kupoa mida ya saa tatu usiku. Huo ni muda mzuri kwa mwanafunzi kujisomea. Akipeleka mpaka saa saba. Au alale kisha amke saa nane mpaka asubuhi kila siku kamwe hawezi kupata sifuri.

Jiji lina Tuition center kila kona. Ukigeuka huku mchikichini, huku mapambano, kule sijui nini huko. Yaani Tuition kila kona. Haya tuseme mzazi hana Pesa ya Tuition. Hivi mtoto kweli unashindwaje kuwa na marafiki wanaosoma tuition badala yake marafiki zako ni wacheza vigoma na mdundiko. Sijui Beach boy, sijui panya Road yaani utumbo utumbo tuu. Alafu unakuja kulitia aibu taifa.

Hivi unapataje sifuri kwenye jiji ambalo kila nyumba inammiliki wa Smartphone kama sio Laptop kabisa. Hivi mnashindwaje kudownload notes na material mbalimbali ya kujisomea. Matokeo yake mnatumia simu kudownlooad Video za ponograph, kuchat Whatsapp, instagram, sijui imo, na Telegram.

Yaani unaishi Dar alafu unapata sifuri wewe kama sio kichaa ni nani. Hakuna mwanafunzi mwenye akili timamu ambaye atasoma Dar apate sifuri. hata hiyo division four haiwezekani.

Haiwezekani jiji lenye chuo cha taifa, chuo kikuu cha Dar es salaam - UDSM , vyuo vingine vingi tuu kama CBE, IFM, NIT, DIT, Ardhi, Muhimbili n.k alafu bado mtu anapata zero huo si upunguani.Sisi wengine wamikoani vyuo vikuu tumeviona tulivyomaliza kidato cha sita. Tukaja mjini tukanyuka misonge tukasepa. Ninyi mmebaki kushangaana hapo kama vichaa.

Ujinga ni pamoja na kutokujua matumizi ya rasilimali. Yaani jiji lenu lina vyuo kama vyote, mnashindwa kwenda kujifunza hata kwa kaka zenu wa chuo. Mnatia aibu kwa kweli.

Jiji la Dar es Salaam ndio jiji pekee lenye vitabu, vitini, na madesa kuliko mkoa wowote hapa nchini. Lakini shangaa ndilo linaloongoza kwa sifuri nyingi ambazo ni zaidi ya mara mbili kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Iringa.

Nina uhakika jiji la Dar es salaam kama lisingekuwa na miundombinu wezeshi kama hiyo hakuna mwanafunzi ambaye angepata hata divisio four. Wote wangepata sifuri kwa sababu ni vilaza.

Jiji la Dar es Salaam hakuna changamoto ya usafiri. Kwa vile wamezoea mambo ya legelege utasikia kugombania daladala ni changamoto. Wewe ni kichaa kama utafikiri hivyo. Nenda mkoani uone wenzako wakitembea kilomita za kutosha zaidi ya masaa mawili na bado wakifika wachapwe bakora kwa kuchelewa. Wewe unatembea dakika mbili upo kwenye daladala huyo mpaka shule. Tena kwenye Daladala mnapiaga kelele wazazi wenu kwa sababu nao ni wendawazimu kama nyie. Yaani matoto yanapanda gari yanaanza kutukana, sijui hadithi ya msanii gani kafanya nini. Mara matusi kibao. Hapo kuna wazazi nao wanasikiliza kwa sababu nao ni walewale. Badala wawakanye ikiwezekana wawachape bakora za uhakika. Looh! Ndio mambo ya vilaza hayo.
Mkoani huwezi sikia ujinga ujinga kama huo. Nenda Misungwi huko, nenda muleba, nenda Rombo, Nenda Bukoba, Nenda Mbeya kama utasikia upuuzi huo.

Jiji la Dar es Salaam hakuna kazi ngumu kwa wanafunzi bado toto lipate sifuri kama sio ukilaza huo ni nini. Mkoani watu wanatoka shule wanasubiriwa na majani ya mbuzi, ng'ombe, kuni, kuchunga mifugo na kulima. Mtoto akirudi nyumbani akichelewa anakula mbata/bakora za uhakika na mzigo unamsubiria shambani. Lakini mwisho wa siku matokeo ya kidato cha nne anasimamisha msonge alafu wewe unayerudi nyumbani saa nane mchana unakalia kucheza PS, au unaenda kwenye mabanda umiza ya kina Acheche na Kimoda kuangalia Muvi unapata sifuri kwa ukilaza wako. Wewe ni kilaza na atakayekutetea ni kilaza bila kujali nafasi yake.

Huwezi ukafeli sehemu yenye shule zilizokaribu karibu.Jamani unashindwa kupata marafiki wa kitaaluma. Wenzako mkoani unakuta wilaya kata nzima kama sio wilaya shule ipo moja na bado anakupiga kipigo cha mbwa koko. Wewe bado uwe mzima kichwani.

Huwezi ukafeli ilhali kuna vipindi vya bungo kids sijui Skonga kwenye Luninga. Hivi unajua huko mikoani wenzako hivyo vipindi hawavijui kabisa kutokana na kutokuwepo na nyumba za umeme. Mfuate yule kijana wa Simiyu aliyechapa one ya Saba uone kama anajua hivyo vipindi. Usishangae kwao hakuna hata umeme. Alafu wewe unashindwa na mluga luga asiyeijua hata smartphone bado ujione kichwani zimo.

Watoto wa Dar es Salaam wanajiona wajanja lakini hakuna ujanja waliokuwa nao zaidi ya ujinga ujinga tuu. Wewe ukimuona kijana wa Dsm anaongea sana ujue kichwani hamna kitu. Usishangae kwa nini jiji hilo ni chafu kupita maelezo. Jibu ni kwa sababu ya ukilaza.

Wewee fikiria mtu anazibua chemba wakati wa mvua ikinyesha alafu yale mavi yanazagaa mtaani. Kama huo sio ukichaa ni nini.

Embu angalia mikoa inayofanya vizuri hapa nchini uone kama utaona hayo mambo ya hovyo. Embu nenda kule Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Kagera, Mbeya na Simiyu uone kama utakuta mambo hayo. Ujinga unaendana na uchafu. Ndio maana vichaa huwa ni wachafu na wanaishi kwenye majalala. Ndio sifa hiyo.

Wewe mtu mzima unapangiwa ratiba ya usafi bado ujione unaakili kweli. Kazi kusumbua viongozi.

Vitoto vya Dar es salaam ni moja ya vitoto vilivyo changanyikiwa. Yaani kitoto kidogo lakini mambo yake mazito. Unakuta kijana wa kiume katoboa pua na anasoma. Mara kanyoa kiduku, mara kabana suruali na matako kama shoga na bado kanasoma. Alafu Baba yupo, Mama yupo, Bibi yupo, Shangazi yupo, na anapewa ugali pumbavu kabisa. Alafu mtu aone nawatukana watu wa Dsm. Ninyi ni vilaza.

Ati mnasingizia maisha magumu huo ni uongo. Mngeishi huku mkoani kwa watabe. Huku maisha magumu lakini watu hawajiharibu kwa upuuzi.

Wanafunzi wa Dsm wanalala na wazungu lakini kingereza weupe yaani kapa. Mkoani watu wanalala na ng'ombe, kuku. mbuzi na kondoo chumba kimoja na bado kijana anamwaga ung'eng'e kama mzungu wa London.

Nakumbuka miaka nikiwa nasoma sekondari nilikutana na kijana maneno mengi wa Dsm. Yaani kijana anaongea yule sijapata kuona. Nikamuuliza swali dogo tuu la Biology kwamba aelezee Mechanism of Hearing. Dogo chali. Nikaona nimmalize kabisa, (physics) nikamwambia aelezee Paschal's Principle dogo jasho linamtoka. Nikasema huyu ili akiniona anisalimie kabisa nikamwambia (history) aelezee WWI. Hapa nilimuuliza swali la history ili nimpumzishe lakini kumbe hata hiyo WWI haijui. Nilishangaa akiongea habari za mieleka. Mama yangu! Nikamtemea mate usoni nikamwambia tokaa hapa! Kwa kweli aliniudhi mno. Japo tulishikana mashati lakini hatakuja kunisahau maana alibadilika na tulikutana Udsm. Alinambia dharau zangu zilimsaidia. Mate yangu yaligeuza upuuzi wake kuwa akili.

Ninachotaka kusema ni kuwa, Jiji la Dar es salaam mnatia aibu. Mbadilike. Ndio maana mnaitwa wanaume wa Dar. Yaani watu legelege.

Haiwezekani muwe na kila kitu bado mnafeli. Kama sio ukilaza huo ni nini.

Mwisho; Najua wapo wanaojitahidi hapa Dsm lakini mnamezwa na wanaoangua mayai viza. Wanawaabisha hao watu.

SIshangai kwenye media nikiona mambo ya hovyo, najua ni matokeo ya vilaza. Mtu anashabikia udaku, shilawadu, na upuuzi mwingine kama huo. Na wenye media nao kwa vile wengi wao ni vilaza wanaruhusu vipindi kuruka hewani. Kwa kweli tunahitaji mabadiliko makubwa katika jiji letu hili.

Ukiishi Dar miaka mitano mfululuzi lazima akili yako iyumbe. Hii ni kutokana na mvutano utakaoupata kutoka kwa vilaza.

Wana- Dar es salaam tubadilike kwa maana mimi mwenyewe ni mkazi wa Dsm.

Ikumbukwe kuwa; nimeitumia Dar kama kielelezo cha mikoa yenye vilaza wa kutupa. Mikoa mingine ambayo sijaitaja ambayo inamiundombinu wezeshi lakini bado inafelisha, huu ujumbe pia unawahusu.

Robert Heriel
Taiko wa Fasihi
0693322300
 
mkuu inaonekana hata dar hujawahi kufika pole sana. ila pamoja na uliyaandika dar wanafunzi wanakabiliwa na changamoto nyingi sana zinazoathiri taaluma zao, nishawahi fundisha shule moja hapa jijini kwa miaka kadhaa. ukweli ni kwamba wanafunzi wanachangamoto nyingi ikiwemo suala la kuchelewa vipindi kwa sababu ya usafiri. ingekua ushawahi kufika ningekupa mfano mmoja, imagine mtoto anakaa ilala anasoma kijichi anabadilisha gari ngapi, amekataliwa marangapi na makondakta wa magari. au mtoto anakaa tabata anasoma manzese, anabadilisha gari ngapi huyo plus foleni. atafika saaa ngp shule. alafu huo utafiti wako dar kila nyumba inaumeme sijui ulifanyia wapi mkuu. kwa shule za serikali wanafunzi wanajitahidi wenyewe kwa asilimia kubwa. kijijini unakosemea ni kweli ila walimu wanawapambania sana madogo kuwafundisha tofauti na mjini. mjini wenye fedha wengi ndo wanafaulu ila kijijini ni tofauti bro
 
Umekasirika.

Wazazi wajanja wajanja, watoto wajanja wajanja.

Kila mmoja anajitia bize for nothing.

Matokeo ndo hayo. Watakuwa mabaharia.

Kwetu mmetubania vyeo vyote ila bado taa ya Mungu inaangaza kwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mada ndefu sana hii sidhani kama wahusika watasoma yote
 
Usiwatetee. Mtoto anaamka saa moja anaenda shule gani.

Kuhusu magari usilaumu, ukiwa mwalimu nenda stend unakuta kitoto kimesimama tu magari yanapita hapandi. Kuna mida konda nafanya kuita nyie twendeni, utasikia tunangojea gari la muddi.

Kuhusu wazazi muulize mara ya mwisho kukagua madaftari au hata kufika shule kuulizia maendeleo ya mtoto ni lini.

Usitetee ujinga,
mkuu inaonekana hata dar hujawahi kufika pole sana. ila pamoja na uliyaandika dar wanafunzi wanakabiliwa na changamoto nyingi sana zinazoathiri taaluma zao, nishawahi fundisha shule moja hapa jijini kwa miaka kadhaa. ukweli ni kwamba wanafunzi wanachangamoto nyingi ikiwemo suala la kuchelewa vipindi kwa sababu ya usafiri. ingekua ushawahi kufika ningekupa mfano mmoja, imagine mtoto anakaa ilala anasoma kijichi anabadilisha gari ngapi, amekataliwa marangapi na makondakta wa magari. au mtoto anakaa tabata anasoma manzese, anabadilisha gari ngapi huyo. atafika saaa ngp shule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiwatetee. Mtoto anaamka saa moja anaenda shule gani.

Kuhusu magari usilaumu, ukiwa mwalimu nenda stend unakuta kitoto kimesimama tu magari yanapita hapandi. Kuna mida konda nafanya kuita nyie twendeni, utasikia tunangojea gari la muddi.

Kuhusu wazazi muulize mara ya mwisho kukagua madaftari au hata kufika shule kuulizia maendeleo ya mtoto ni lini.

Usitetee ujinga,

Sent using Jamii Forums mobile app
si kweli mkuu. huenda hujasoma habari yote ya mtoa mada ukasoma tena majibu yangu, ikumbukwe mtoa mada amefanya hitimisho na kusema wote. si wanafunzi wote wako hivyo. wengine wanachangamoto kubwa sana. kuna mwanafunzi aliwahi niambia mwalim m nimepangiwa chumba na baba ila hali ya kiuchumi ya nyumbani ni ngumu mno sometime anakosa hata kula. wazaz waliamua kumtafutia chumba karib na shule ili awahi kufika shule. chumba kisicho na umeme, unafikiri huyu atasoma vipi? kwahio sometime akirudi shule anaenda kuhangaika apate chochote
 
mkuu inaonekana hata dar hujawahi kufika pole sana. ila pamoja na uliyaandika dar wanafunzi wanakabiliwa na changamoto nyingi sana zinazoathiri taaluma zao, nishawahi fundisha shule moja hapa jijini kwa miaka kadhaa. ukweli ni kwamba wanafunzi wanachangamoto nyingi ikiwemo suala la kuchelewa vipindi kwa sababu ya usafiri. ingekua ushawahi kufika ningekupa mfano mmoja, imagine mtoto anakaa ilala anasoma kijichi anabadilisha gari ngapi, amekataliwa marangapi na makondakta wa magari. au mtoto anakaa tabata anasoma manzese, anabadilisha gari ngapi huyo. atafika saaa ngp shule.

Dar ni jiji ninalolielewa kuliko mji niliozaliwa(Moshi)
Ninaishi Sinza Kwaremi karibu na Shamo Hotel. Njoo hapa nikutembeze katika mji huu uone kile ninachokisema.

Sijajua ni wapi nisipopajua kwa hapa Dsm.
Huko Mbagala maeneo ambayo nimeishi ni Mtongani, hapo kuanzia kwa Chang'ombe pale DUCE, Uhasibu, kwa Azizi Ali mpaka Mbagala unapoishi napafahamu fika. Sio kwa kuhadithiwa au kupita na daladala bali kwa kutembea. Mpaka unatokea kongowe unaacha barabara ya Mkuranga unakata kushoro kuelekea Twangoma, Mwembe Mtengu mpaka unatokea Kigamboni. Bado unasema sipajui Dar?

Tena huko ni porini. Njoo hapa City Center posta, Upanga, Muhimbili, Kariakoo, Jangwani, huyu hapa mpaka magomeni, manzese, Ubungo, bado useme sipajui. Au nikupitishie Tandale mpaka sinza, kijitonyama, mwananyamala, makumbusho. Bado siijui haka kamji.
Au unataka Mwenge, Mbezi beach, Tegeta, Boko, Basi Haya, Bunju, unavuka Daraja huyo unatokea mapinga kwenye shule ya Baobao sekondari huku ni bagamoyo.

Bado Dar sipajui, Unataka njia ya Ubungo, Kimara, mbezi mwisho, Kibamba huyo unaacha Dsm unapokelewa na Kibaha.

Au ni Msasani, Masaki, na Ostabey.

Wanafunzi wa Dar ni wavivu wala hakuna kujitetea.

Hoja ya usafiri sio kweli.


Hayo mazingira nisiyoyajua ni yapi.
 
Wewe naye kilaza kama wana-dsm wenzio.

Hizo shule walizofanya vizuri wanafunzi wengi wanatoka Dar.

Shule za Dar huwa zinabakiwa na wanafunzi ambao wazazi wao ni vilaza.

Taikuni wa fasihi mbona unaniangusha?


Unforgetable

Hapa sijazungumzia waliofanya vizuri wanatoka wapi mzee Baba. Nazungumzia wanaosomea Dar. Hilo nalielewa mkuu
 
Usiwatetee. Mtoto anaamka saa moja anaenda shule gani.

Kuhusu magari usilaumu, ukiwa mwalimu nenda stend unakuta kitoto kimesimama tu magari yanapita hapandi. Kuna mida konda nafanya kuita nyie twendeni, utasikia tunangojea gari la muddi.

Kuhusu wazazi muulize mara ya mwisho kukagua madaftari au hata kufika shule kuulizia maendeleo ya mtoto ni lini.

Usitetee ujinga,

Sent using Jamii Forums mobile app

Anadhani sisi hatuishi Dar. Labda asubiri ambao hawajawahi kufika Dar
 
Back
Top Bottom