Dar: Mtoto wa miaka 17 ampiga risasi mtoto mwenzake na kumsababishia kifo

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Hii ni habari mbaya sana maana ni ngumu kuiamini.

----
Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Ilala linamshikilia Juma Shamata kwa kushindwa kuhifadhi eneo salama bastola yake, hali iliyosababisha mtoto wake wa miaka 17 kuitumia kwa kumpiga risasi mtoto mwenzie Ikhissan Abdilahi (10) na kumsababishia kifo.

Jeshi hilo pia linamshikilia mtoto huyo wa kidato cha tatu kwa tuhuma za mauaji.

Tukio hilo lilitokea Aprili 2 katika mtaa wa Viwege kata ya Pugu nyumbani kwa Shamata ambako Ikhissan alikwenda kucheza.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya Ikhissan kuingia kwenye nyumba hiyo walisikia kishindo na punde mtoto aliyefanya tukio hilo alitoka akiwa amembeba na kumrejesha nyumbani kwao akieleza kuwa amepigwa na shoti ya umeme.

Shangazi wa marehemu aitwaye Aisha Hussen alisema; “Nilikuwa nimekaa kwenye kibaraza hapa nje, Ikhissan alikuwa anaendesha baiskeli, alipofika pale (kwenye nyumba aliyopigwa risasi) akaingia ndani, baada ya muda mfupi tukasikia mlio mkali, lakini hakuna aliyehisi kwamba inaweza kuwa risasi.

“Ghafla akatokea mtoto wa nyumba ile akiwa amembeba Ikhissan na kumleta hapa nje ya geti akamuacha akisema kwamba amepigwa na shoti ya umeme, nilimkimbilia nikamchukua kumuingiza ndani kwa ajili ya huduma ya kwanza maana alikuwa akivuja damu,” alisema Aisha.

Baada ya kumchunguza kwa dakika kadhaa waligundua kuwa alikuwa na tundu kifuani ambalo lilitokeza upande wa pili ndipo walipomuwahisha hospitali ambako waliarifiwa kuwa ameshafariki dunia.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala, Moses Fundi alisema yupo mtoto aliyekuwa anacheza na mwenzake kisha kumjeruhi na risasi iliyopelekea kupoteza maisha.

Kamanda Fundi alisema jeshi hilo linamshikilia mwanafunzi huyo na baba yake kwaajili ya mahojiano ili kujua ukweli wa tukio hilo.

Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa kulikuwa na uzembe katika uhifadhi wa silaha hiyo, jambo lililosababisha mtoto kuifikia.

Alisema kuwa silaha haiwezi kuhifadhiwa sehemu kama juu ya kabati, kama mtu anamiliki silaha utaratibu wa kuhifadhi unafahamika, ikiwamo kuifungia kwenye sanduku la chuma.

“Tumegundua silaha inamilikiwa kihalali, lakini inawezekana kuna uzembe katika utunzaji wa silaha hiyo, kama mtoto anaweza kuichukua ina maana hata mwizi angekuja angeweza kuichukua,” alisema kamanda Fundi.
 
huyu dogo atakuja kuwa jambazi akiachwa mtaani huwezi mpiga risasi bado ukapata ujasiri wa kumbeba na kudanganya kapigwa na shoti ya umeme

kweli 17 ni umri wa mtoto ila kwa matendo haya huyu anajua alichokuwa anafanya wamlambe mvua za kutosha
 
Duh huyu dogo ni jasiri na ana roho ngumu, unampiga mtoto mwenzio risasi na unambeba kumpeleka kwao na unadanganya amepigwa na shoti😪 kwanza miaka 17 huyu si anajitambua kabisa sheria ifate mkondo wake tu .

basi wazazi wenye silaha tunzeni vizuri silaha zenu ili kuepusha madhara kama haya. R.I.P mtoto
 
huyu dogo atakuja kuwa jambazi akiachwa mtaani huwezi mpiga risasi bado ukapata ujasiri wa kumbeba na kudanganya kapigwa na shoti ya umeme

kweli 17 ni umri wa mtoto ila kwa matendo haya huyu anajua alichokuwa anafanya wamlambe mvua za kutosha
Mimi mwenyewe amenishangaza.
 
huyu dogo atakuja kuwa jambazi akiachwa mtaani huwezi mpiga risasi bado ukapata ujasiri wa kumbeba na kudanganya kapigwa na shoti ya umeme

kweli 17 ni umri wa mtoto ila kwa matendo haya huyu anajua alichokuwa anafanya wamlambe mvua za kutosha
Miaka 17 -18 ni umri wa A level
kwa wakina junia (junior) miaka 17 iyo huku kijijini ndo anamaliza la 7 pia watanzania wengi huanza shule na miaka 7 humaliza na 13-14 na kidato cha 4 humaliza na 17-18 (wengi sana )
 
Hata majambazi hawana ujasiri huo wa kujeruhi na kumbeba majeruhi mpaka kwao na kupindisha stori. Huyu ni zaidi ya jambazi.
 
Back
Top Bottom