Dar: Mkuu wa Mkoa, Amos Makala aagiza Mabasi yote kushushia abiria Stand ya Mbezi

Ni upumbavu haswaa...hawa maRC na UDC wanatuonaje! Kwanini wanapenda kuwatesa wananchi!.. wao wana maV8 na isitoshe wanatumia usafiri wa angani....kwanini wanatusumbua lakini!....Msafiri anatoka Mwanza anashukia mbezi, alafu anafikiria usafiri wa kutoka mbezi adi mjini, na haoo una watoto, mizigo na kama umepanga kufikia hotel ndio akili inachoka haswaaaaaaaaa......ni kutesana tu hakuna kingine.

Naomba serikali iliangalie upya swala hili, ikiwezekana abiria washushiwe mjini/Urafiki atleast...mfano; abiria wa kutoka kanda ya ziwa musoma, mwanza, Shinyanga na kahama bus linawasili saa 5 usiku, alafu ukifika stand utafute tena usafiri wa kukupeleka adi mjini jamani!!!!!, hamuoni ni mateso haya!...na isitoshe kuna gharama tena za usafiri ....aisee treni ya umeme ikamilike haraka, otherwise tutaendelea kuteseka.
 
Au kwa mfano nimetoka Arusha na BM kufika Mbezi kituoni limeshusha abiria na likitoka hapo linaelekea kwenye ofisi zao zilizopo Shekilango,nami naishi Manzese.
Je hawaruhisiwi kuja kunishusha Shekilango?.
Ni lazima nishukie Mbezi?.
Kateleza
 
Nimekosa cha kusema. Mheshimiwa Rais ikikupendeza tizama hizi kauli ...zinaleta shida katika jamii. Sambamba na hilo hiyo stendi inaitwa Magufuli,....hivyo kuto-recognized hiyo stendi kwa jina hilo kulikofanywa na RC si sawa hata kidogo. Ifike mahala tuweke tofauti zetu pembeni tufanye kazi kwa maendeleo ya Taifa hili
 
Mkuu
Ili Stand ya mabasi iwe karibu na kila mkazi wa Dsm...ilitakiwa ijengwe wapi?
Shida siyo stendi kujengwa Mbezi, shida ni hiyo amri ya RC. Kwani wangeruhusu mabasi kushusha hapo stendi halafu wakaendelea na safari mpaka kwenye vituo vyao ili kuwapa nafasi abiria wakachagua wanapotaka kushuka ingepunguza nini?
 
Mkuu

Hajateleza ni makusudi na ndio aina yake ya mawasiliano na umma (rejea akiwa Mbeya alitoa tamko watu wakaanza kuzomea lakini hakuona aibu)

Leo amesahau jinsi alivyokuwa akiigiza kubebwa na pikipiki wakati akitembela wapiga kura huko Mvomero miaka hiyo kabla hawajamtema.

(Shida mwana malevya)
 
Nimekosa cha kusema. Mheshimiwa Rais ikikupendeza tizama hizi kauli ...zinaleta shida katika jamii. Sambamba na hilo hiyo stendi inaitwa Magufuli,....hivyo kuto-recognized hiyo stendi kwa jina hilo kulikofanywa na RC si sawa hata kidogo. Ifike mahala tuweke tofauti zetu pembeni tufanye kazi kwa maendeleo ya Taifa hili
Huyo RC aondoshwe haraka sana Dar maana amewadhalilisha kwa makusudi wana Darisalama na wageni wote wanaoingia jijini humo. Pili ameonesha chuki za dhahiri kutotamka stendi ya Magufuli na kuiita stendi ya Mbezi....kwa chuki hizo watumiaji wake amewamwagia upupu-washawasha na akili zitakapowakaa sawa atajilaumu mwenyewe kuchokoa pweza wakati hafahamu namna ya kumwandaa aliwe
 
Kuna viongozi wajinga sana, hawawazi kuturahisishia maisha bali kutukandamiza, yaani gar inakwenda Shekilango na mi nnaenda Manzese lkn eti unilazimishe nishuke Mbezi? Hawa viongozi huwa wanawaza kwakutumia kitu gani? Kwanini watulazimishe kuteseka
 
Kama ishu ni wahamiaji haramu, amri/agizo hilo liwe kwa mabasi yanayosafirisha abiria nje ya nchi kwasababu ndani ya mipaka ya JMT hatuna wahamiaji haramu.

Na pia sidhani kama kuna route za daladala za moja kwa moja kutoka maeneo yote ya daressalaam kwenda mbezi mwisho. Huu ni usumbufu.

Au lengo ni kuwafurahisha hao mamalishe na wamachinga waliopo hapo stendi?
na bado inaweza kufanyika kwa usahihi kwa kuweka some rules wakati wa kukata ticket
 
Shida siyo stendi kujengwa Mbezi, shida ni hiyo amri ya RC. Kwani wangeruhusu mabasi kushusha hapo stendi halafu wakaendelea na safari mpaka kwenye vituo vyao ili kuwapa nafasi abiria wakachagua wanapotaka kushuka ingepunguza nini?
Stendi kuu ibaki hiyo ya Magufuli Mbezi Louis lakini zijengwe zingine huko Mbagala na Tegeta/Boko au Bunju
 
Nimesikiliza taarifa ya habari ya saa mbili usiku anasema mabasi yote ya kutoka mkoani yapitie kituo cha mbezi. Ila hajasema yaishie mbezi kituoni. Inaonekana kuna mabasi ambayo yalikuwa hayapiti kwenye kituo cha mbezi.
 
Kuna viongozi wajinga sana, hawawazi kuturahisishia maisha bali kutukandamiza, yaani gar inakwenda Shekilango na mi nnaenda Manzese lkn eti unilazimishe nishuke Mbezi? Hawa viongozi huwa wanawaza kwakutumia kitu gani? Kwanini watulazimishe kuteseka
Inawezekana kashinikizwa na wamiliki wa daladala, bajaji na bodaboda kwamba wanakosa abiria wa uhakika yanapowasili mabasi kituoni hapo.
 
Asema utaratibu wa Sasa ni rahisi ata kusafirisha wahamihaji haramu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha kuanzia Sasa Mabasi yote yanashusha na kupakia abiria kwenye kituo kikuu Cha Mabasi Cha Mbezi Louis.

RC Makalla amesema hayo wakati alipotembelea kituo hicho na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za Wafanyabiashara kituoni hapo.

Amesema Serikali inatambua kituo kimoja pekee Cha Mabasi ambacho ni Mbezi na uwekezaji uliofanyika ni mkubwa hivyo hakuna maana Kama kila mmiliki wa mabasi atakuwa na kituo chake kupakia na kushusha abiria.

Aidha RC Makalla ameelekeza uongozi wa Stendi hiyo kuweka utaratibu wa baadhi ya Mabasi kushusha abiria kwenye eneo la kulaza magari ambapo kuna Banda la Mamalishe ili kuchochea biashara.

Kuhusu changamoto ndogondogo zilizojitokeza kituoni hapo, RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Halmashauri ya Ubungo na kituo kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Mhe.Makalla pia ameelekeza Wafanyabiashara kituoni hapo wapangwe Katika utaratibu mzuri na bora kuendana na hadhi ya kituo.

Wakati huohuo RC Makalla ametembelea Soko la Machinga lililopo pembezoni mwa Stendi hiyo na kutaka Wafanyabiashara wote wahamishiwe sokoni hapo na uchunguzi ufanyike kwa wale waliopatiwa vibanda kwa upendeleo na kujuana ambapo Wafanyabiashara hao wamesema wapo tayari kuhamia sokoni apo na wamechoka kufanya biashara barabarani.

Amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuweka utaratibu wa Daladala kushusha abiria sokoni apo ili kuchagiza biashara.
View attachment 1846949View attachment 1846950View attachment 1846951View attachment 1846952View attachment 1846954
Huu utaratibu wa viongozi kutoa matamko yasiyozingatia sheria unaturudisha nyuma sana!

Mnaalika wawekezaji waje kuwekeza Tanzania halafu viongozi hawafuati sheria wala consistency kwenye taratibu. Mambo haya ya kishambakishamba mnatakiwa kiyaacha.

Mwekezaji kama DarLux amewekeza pesa zake nyingi kutengeneza terminal yake baada ya kupata vibali vyote ghafula mkuu wa mkoa anatoa amri ya ajabuajabu. Mambo ya namna hii hayakubaliki kwenye jamii ya watu wastaarabu. Viongozi badirikeni. Mantuangusha sana.
 
Vipi k
Asema utaratibu wa Sasa ni rahisi ata kusafirisha wahamihaji haramu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha kuanzia Sasa Mabasi yote yanashusha na kupakia abiria kwenye kituo kikuu Cha Mabasi Cha Mbezi Louis.

RC Makalla amesema hayo wakati alipotembelea kituo hicho na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za Wafanyabiashara kituoni hapo.

Amesema Serikali inatambua kituo kimoja pekee Cha Mabasi ambacho ni Mbezi na uwekezaji uliofanyika ni mkubwa hivyo hakuna maana Kama kila mmiliki wa mabasi atakuwa na kituo chake kupakia na kushusha abiria.

Aidha RC Makalla ameelekeza uongozi wa Stendi hiyo kuweka utaratibu wa baadhi ya Mabasi kushusha abiria kwenye eneo la kulaza magari ambapo kuna Banda la Mamalishe ili kuchochea biashara.

Kuhusu changamoto ndogondogo zilizojitokeza kituoni hapo, RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Halmashauri ya Ubungo na kituo kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Mhe.Makalla pia ameelekeza Wafanyabiashara kituoni hapo wapangwe Katika utaratibu mzuri na bora kuendana na hadhi ya kituo.

Wakati huohuo RC Makalla ametembelea Soko la Machinga lililopo pembezoni mwa Stendi hiyo na kutaka Wafanyabiashara wote wahamishiwe sokoni hapo na uchunguzi ufanyike kwa wale waliopatiwa vibanda kwa upendeleo na kujuana ambapo Wafanyabiashara hao wamesema wapo tayari kuhamia sokoni apo na wamechoka kufanya biashara barabarani.

Amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuweka utaratibu wa Daladala kushusha abiria sokoni apo ili kuchagiza biashara.
View attachment 1846949View attachment 1846950View attachment 1846951View attachment 1846952View attachment 1846954
Vipi kuhusu sisi wa Gongo la Mboto na chanika,yaani Tilisho ituache huko Mbezi,wakati inatufikisha mpaka huku.

Hapo umechemka,fanyeni marekebisho yatakayo vuta wawekezaji kuingiza mabasi hapo.kumbuka hawa watu wamekopa hayo mabasi yanatakiwa yarudishe na waweze kunua mengine.Pale wanapopaki ndiyo panapofaa nyie nendeni mkakusanye ushuru wenu hapo hapo ila msiwazue.anzeni na wamachinga kwanza,ambao hata hawalipi chochote serikalini
 
Ila huyu makala ni empty kiasi hichi nilijuaga jiwe kamuonea kumbe ni problem creator badala ya solver loh, hawa wateule wa mama awaangalie performance Yao huyu makala ame create usumbufu kwa kukurupuka
 
Nimesikiliza taarifa ya habari ya saa mbili usiku anasema mabasi yote ya kutoka mkoani yapitie kituo cha mbezi. Ila hajasema yaishie mbezi kituoni. Inaonekana kuna mabasi ambayo yalikuwa hayapiti kwenye kituo cha mbezi.
Kituo cha Mbezi ni kipi?

Kituo cha Mbezi mwisho ni cha daladala lakini cha mabasi ya mikoani na nje ya nchi ni cha Magufuli, kwanini mnakwepa kutaja hivyo?

Laana itawatafuna......ilimtaka hivi

"Madamu mmeamua kukiita kituo hicho kwa jina langu, basi ni sharti kitoe huduma inayonufaisha watu wa chini, mkiianza kuwanyanysa sitakubali"

Kwa sasa hayupo, lakini ujasiri uliopandwa kwa wana Darisalama, kauli iliyotamkwa sio ya kiuongozi ila ina ishara za chuki binafsi
 
Back
Top Bottom