Dar: Matukio na yanayojiri jijini...

wewe na wa kule kwenye box au mikoani? Hiyo ndo Dar Mkuu ila inaonyesha unapenda sana starehe bahati nzuri unaenda na my wife wako that's good
 
 
 
lory lna kondakta Wajameni?.....

Nimemuita kondakta. Au huku mnawaitaje wale wanaowasaidia madereva? turn boy? Katika magari ya abiria kule South wanaitwa "Transport Officer" ukibainika kumuita kondakta unaweza kujikuta matatizoni.
 
Dah! Huu ni utalii wa ndani...! BTW! Mbona TMK tu? Au ndiyo kwetu Mbagala?
Harbor View Hotel, chumba cha kulala "standard room ni USD 178, exchange rate ya hotel ni USD 1=THS 1600, usiku unaoitwa "night sea food platter", nimekaribishwa......ati mhudumu hii ni ghorofa ya ngapi vile, nane au tisa?...sahani kubwa kabisa inaletwa ina crabs, prawns, huyu samaki mwingine simjui,ebo mbona tena kuna kuku? kwani na yeye ni wa baharini?....namvumilia, Pembeni kuna BBQ, nakaribishwa na wasabi, ile inayoliwa na sushi(wali na row fish ya kijapan). Hapa napata mashaka kidogo, kwanini wasiniletee "tartar sauce" kwa ajili ya samaki badala ya wasabi? Elimu ya kula sina ila kwa mbali nafikiri watu wa mahoteli mtanisaidia.Nilifurahia kuyaona maji karibu, meli zile palee ingawa ilikuwa ni usiku. Bei ya stangdard room haikuniridhisha, nimewaandikia comments zangu..sijui siku hizi kama masanduku ya maoni yanafanya kazi, labda enzi zile. nitarudi tena hapo kabla ya kuondoka. Nimebakiza siku tano tu hapa Dar.
 
wewe na wa kule kwenye box au mikoani? Hiyo ndo Dar Mkuu ila inaonyesha unapenda sana starehe bahati nzuri unaenda na my wife wako that's good
Mkuu umenifurahisha sana, nimepata msamiati mpya,,,kumbe mikoani panaitwa kwenye box?..nimeipenda hii ingawa inadhalilisha kidogo!!....kilichonifanya niache kufanya kazi kule Kuwait ni joto ingawa malipo yao hayakuwa mabaya, hapa napo kuna joto, mimi nimezoea baridi...naoga mara 3 hadi nne kwa siku kabla ya kulala. suti za nini hapa, t-shirt na jeans...kujiachia nako ruksa...SABAYI tukutane Billicanas leo jioni, sipajui ila wife yeye kwao ni hapa hapa, ni mwenyeji sana kabla hatujaoana alinicheka eti sijawahi kufika Dar.......ila hayo maisha ndivyo yalivyo.
 
safi sana nimeipenda
Nawasha TV, napata midundo ya " Country Music". Huyu anayeimba ni Trisha Yearwood..."she is in love with the boy"......unajirudia rudia "she gonna marry that boy some day" nakaza macho kujua ni Channel gani..................SIBUKA TV.
Nimelipenda hili jina na natamani kuona SIBUKA inafika mbali kimafanikio, sikuwahi kujua kama kuna kitu kama hiki.
 

I'm too old for bilicanas mkuu,Just have funy usimsahau mamsap tu usije jikuta kwa wa haya
 
I'm too old for bilicanas mkuu,Just have funy usimsahau mamsap tu usije jikuta kwa wa haya
Hapana mkuu, siwezi msahau hata kidogo anajua kuitumia nafasi yake vizuri, na lazima nimheshimu sana....na popote niendapo niko na mashemeji zangu wawili, wananipenda sana, wife kanikumbusha IFM wakati. wakati anasoma hapa ndio nilikuwa nafanya bidii kumpata. Mdogo wake wa kiume niko naye, naye anasoma hapa, huyu ndiye best yangu na sidhani kama ataruhusu kuona dada yake akitendwa (ingawa sina matukio ya tabia za namna hiyo), Pia tuko na "family friend" Khadija a.k.a Mzanzibar, huoni hata kama mtu ana tabia zake bado hapa kawekwa kati mkuu.....Nashukuru sana kwa Kampani yenu Mkuu SABAYI, hata kama hatuonani.
 
sabasita .. kwa mujibu wa maelezo yake ... hii itakuwa ya Dar Mbele kidogo ya Temeke Hospitali kwenye kona ya Temeke Sudani ... wenyewe vijana wanapaita "Kwa Timbwa"
Ni Kweli mkuu, si mbali sana na Hospitali ya TEMEKE ingawa mimi mwenyewe ukiniambia niende tena maeneo hayo inabidi kwanza nifike pale hospitali au kituo cha polisi Chang'ombe au kanisa la wasabato TEMEKE...nakumbuka hoteli yenyewe ina rangi ya njano na maandishi yako kwa pale juu kabisa. Ni kama ghorofa nne au tano sikumbuki vizuri.
 
hii ya huko mbezi haina vituko hivyo thats why nilistuka nikataka kujua huo mtaa wa sudan ni upi
Asante mkuu, ila huko Mbezi nitaenda tu kama utaratibu wa "utalii wangu wa ndani ya Dar" kabla sijaondoka....lakini mbona najitahidi namna hii na bado silimalizi hili jiji?
 
Iron Lady, ni kweli na ndio maana nafanya bidii kwani nina muda mchache hapa.....niacheni tu nifurahi..niongeze siku za kuishi.
We Iron Lady, si umwakilishe Lady mwenzako? WiseLady kwa kumpatia Mwita Maranya namba zangu za kiganjani..........basi kama unaona uvivu natoa tangazo;

Tangazo: Tangazo: Tangazo:

This is very special for WiseLady...I mean the Original WiseLady, for easing my trip from J,burg to Dar,. Also by enabling to meet Mwita Maranya, the Comrade, by teleconversation.....big mwanajamii!!

Someone told me by being in Dar, I will be ending up into "No long at Ease" I say shame on him.I am on my bliss!!!
 
Thanda, pleasure is all mine. Kama Mwita Maranya amekualika kwake mabwepande usije kuthubutu tafadhali,otherwise enjoy your stay
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…