Dar inawapotezea watu muda

Hahahahah, kuna uhalisia lakini?
 
Gari zuri lipo arusha wewe,,,dar hakuna magari

Ww tako husifananishe dar na arusha maisha yako yote
Arusha mjin unazunguka na miguu umemaliza uonao mji
Ivi nyinyi watu warusha mnajifananishaje na dar ata iyo mwanza hafikii ndio unafananisha na dar
Nyinyi saizi yenu mbeya
 
Kuna msemo huwa unatumika sana kwenye makasino makubwa makubwa kuwaasa wacheza kamari wao "Winners knows when to stop "
Inatumika kuelezea wacheza kamari kuwa ukiliwa sana kwenye game basis ujue na kuacha usilazimishe sana mpaka unafilisika kabisa

Hii ndo philosophy yangu kuhusiana na dar !, yes kuna fursa ..sawa , kuna maisha mazuri na hufuma nzuri kwa karibu kila kitu...sawa , kuna idea nyingi sana hapo ...sawa , lakini si kwa kila mtu, jaribu maisha dar na ku hustle hapo , ikishindikana toka na idea za hapo njoo mkoani ! Implement idea za dar , kunauwezekano makubwa wa kufanikiwa
 
We hapo Dar uko rank gani mkuu?
 
At least umeliweka vzr mkuu...kwahy bottom line kwanza ni lazima ifike Dar upambane ukiwin umewin ukishindwa, implement fikra za hustle za kiDar mkoani.
Ni kweli Dar isn't for everybody!
 
Hizo ni story tu kuna madogo walimaliza pale ifm wakawa wanapeana story za fursa za kutengeneza bisi kilichowapata wanajua wenyewe tena hesabu yao wao ilikua buku 10 tu kwa siku.
Hahahahah nimecheka kimumbwaa man. Yani kila nikisoma hio sentensi dah! Ni shida!!! Wabongo tunapendaga kupeana ma hope sana ya mafanikio ya muda mfupi! Ha ha ha ha, same story za mayai ya kware mara forex manina. Jana nilikuwa namsikia mtumishi mmoja wa Nabii Bushiri akitoa 1 na 2 jinsi forex ilivyomfanya vibaya. Anadai amekula hasara ya zaidi ya dolla elfu 10 ikiwa hajafanikiwa. Ni kupiga na kupigwa tu. ha ha!!!
 
15,000 per day kwa dar na 15,000 per day ya huko katavi/bariadi/mtwara/lindi/ ni mbingu na ardhi,cheki yo' facts again boss.
Huko mtwara napata 15,000 baada ya kupiga mishe gani?Huwezi amini vijana wengi kwa siku wanaingiza kati ya buku 3 hadi 5.ukipata 10,000 siku hiyo ni ya furaha balaa,ama la hiyo buku teni umepiga kazi ya kibabe balaa.Vijana wengi Dar wanapiga kazi ya udalali hiyo ndo wanapata pesa ya bure.Ila kwa kupiga kazi yaani mpka upate teni umechoka haswa.kazi ya kupata 5000 unapewa buku au buku 2.sasa kupata msimbazi ni noma sana kwa Dar na majiji mengine.Ukija kijijini kupata pesa ni kwa msimu.msimu wa mavuno sasa kama huna akiba ya kutosha ni noma.pia kijijini madili ya daiwaka hakuna au ni adimu balaa.ukijiajili pia ni changamoto sana.Enzi za Jk mtu unaweza kumsaidia kazi ndogo sana akakupa hata jero.saiz nani awezaye.?saiz vijana kama Dar na maeneo mengine ya miji akipata buku anawaza kwenda kubeti.mtu anakuwa na mikeka hata mitatu.mmoja unatiki analamba 25000 mingine miwili inachanika.Hivyo ndivyo wanaendesha maisha yao.Maeneo mengi ya mjini vijana saiz kazi yao kubwa ni kubeti.Hakuna ajira wala madili,madili ukipata ni ya jasho na damu.
 
Kwahiyo tunaoishi Dom tumepotea njia?
Mkuu kama umehamishiwa Dodoma kwa mshahara wako ule ule ambapo sasa unatakiwa kuendesha familia mbili (Dodoma na Dar) maana najua huwezi kuhama na mke wako ndani ya mwezi moja na kama ulikuwa na kimradi Dar angalau ka kuingiza kipato cha laki 5 kwa mwezi, ukweli mchungu ni kuwa umepotea na unapoteza muda. Sorry.
 
Halafu ni swala ambalo halipingiki,kati ya kumi kwa dar waliofanikiwa na wana story nzuri ni mmoja maajabu wakizid hapo
 
Waulize wenzio waliohamia dodoma wanavyolia Lia. Dar kufanikiwa ni rahisi kuliko kufeli.
Ngumu,kufanikiwa kwa fursa zipi mkuu....usidanganywe na mafanikio ya ujanja ujanja...maana mtu anayeishi dar hata wakijaga mikoani yaani unaona macho juu juu,tunamuambia tuliza mpira chini anza upya hujachelewa
 
Ni kweli asilimia mia kamili!
 
Bado una mawazo ya kazamani,hivyo vitu vinakusaidia nini kwenye maisha yako ya kubabaisha...leo wanaowekeza pale city centre na kko angalia vizuri mitaji wameitafuta mkoani ambako unakubeza...nyinyi ndio kazi kusifia mshikaji amenunua gari kali,au kupiga picha magari na nyumba za watu,ukiona mtu wa mkoani anasifia kitu ujue on the progress kununua yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…