Dar inawapotezea watu muda

Dar inawapotezea watu muda

Mi sikatai matokeo ya huo utafiti wa NBS , maisha ya mkoani yanaeza kweli kuwa magumu, lkn mkoani ni rahisi sana kutoka kimaisha kuliko hapo dar , Nina ushahidi wa hilo, Nimezaliwa dar nimesoma na kukulia hapo, miaka mitatu hii ya mwisho ndipo nilipopiga U turn kutafuta fursa mkoani, naujutia sana muda niliopoteza hapo dar
Na mimi nimezaliwa Dar, nimekulia Dar+ughaibuni nasisitiza Dar kuna fursa nyingi kuliko mkoa wowote nachelea kusema kuna fursa kuliko hata ughaibuni kama utarumia uliyojifunza nje.
 
Afadhali mkoani unaweza kutafuta sehemu ukakaa ukapata ka upepo na joto lake lina muda na muda sio wakati wote km Dar
Dar ina joto wakati wote? Si kweli,joto ni kuanzia December hadi mwezi wa pili au tatu baada ya hapo zinaanza mvua ambazo zinapunguza sana joto, then mwezi wa sita mpaka hivi sasa ninapoandika hamna joto unless umeamua tu kupotosha.
 
Hivi mkoani hakuna kula kuvaa kuumwa?na mkoani si unaweza kuwa unatumia zaid ya nauli hiyo kwa boda boda au Bajaj?au mkoani kibarua huyo huyo badala ya kulipwa elf 8 atalipwa elf 18?
Hao wanajitoa ufahami. Takeimu zinaonesha mikoani ndio kuna dhiki na Dar ndio ina unafuu wa maisha. Hizi nyingine ni porojo tu.
 
Maoni yangu

Dar Ni vigumu kujenga nyumba kuliko mkoani
Lakini dar Ni rahisi kupata hela kuliko mikoani
Hii ina uhalisia, Dar kipato ni kikubwa ila pia gharama za maisha zipo juu sana. Mkoani kipato hafifu ila gharama za maisha zipo chini pia! Ukiwa na mshahara wa kawaida tu mf: 750k ukaweza kumiliki miradi mbali mbali mkoani unatoboa chapu sana kuliko ukiwa dar.

Bongo pagumu sana kwa wale wasio na mitaji mikubwa maana gharama huzidi kipato matokeo yake unajikuta unatelezea hapo hapo(sliding) husogei mbele labda upige dili za hela chafu, wanaofaidi ni wale waliowekeza mamilioni.
 
Dar inataka hisabati wenye uwezo wa kukokotoa milinganyo ndio hawa mnaowasifu...wenye uwezo kinyume chake wanakimbia au kupaponda...binadamu yeyote anaetumia akili yake vizuri,alimradi ana siha njema anao uwezo wa kuishi mahali popote ambapo binadamu wengine wanaishi.
 
nyinyi ni waoga wa maisha, maisha popote, kama umeamua kurudisha mpira kwa kipa ni mpango wako kivyako vyako, wengine tumetusua na tunaendelea kutusua hapa hapa bongo daslamu

Maisha popote kaishi chooni au kafungue bucha la kitimoto kwa msikiti...



Wakati mwingine maisha ni chaguzi zinazoendan na mazingira lakin si popote...
 
Mwana F.A aliimba usije mjini,tafuta huo wimbo uusikilize utapata funzo
 
Uko jumla jumla sana MKUU.Maisha ni popote akili yako tu.
 
Na mimi nimezaliwa Dar, nimekulia Dar+ughaibuni nasisitiza Dar kuna fursa nyingi kuliko mkoa wowote nachelea kusema kuna fursa kuliko hata ughaibuni kama utarumia uliyojifunza nje.
Doh naona hata hatuelewani umeng'ang'ania dar tu kuna maisha mazuri, mada haikuwa dar na mkoani wapi kuna maisha mazuri, mada inasema dar na mkoani wapi ni rahisi kufanikiwa kimaisha ,
Typical mindset ya watu wa dar , hatukubali kuonekana tumeshindwa hata kidogo especially unapofanya argument na mtu unayedhani ni wakuja !!!
Naona mada ya chini hapo unampinga kwa nguvu zote mdau aliyesema kuwa dar kuna joto ,
 
Back
Top Bottom