DAR iko overrated, Majority ya watu wanaishi maisha ya ovyo sana

Mimi mwenyewe nipo Singida lakini kila nikipata pesa naenda kutumia Dar zikiisha narudi zangu kuja kula ugali na ndalu Dar ukiwa na pesa raha sana huku mkoani ni mwendo wa kupauka tu saa moja usiku giza tororo kama tupo kwenye mahandaki
Haaahaaa!! Saa Moja tu giza tororo. Yaani mikoani unakuta Binadamu na Kuku muda wao wa kuingia ndani ni Mmoja
 
Suluhusho la slums sio demolition, bali ni mipango miji, hii attitude ya bomoa bomoa inarudisha sana maendeleo ni vile hatujui tu .
Bila mipango miji hata Dodoma nayo itakuja bomoa bomoa , mji mdogo kabisa tayari kuna ujenzi holela usiopangiliwa , Mkonze njia ya kwenda Iringa kwa mfano tayari ina slums, radius ya 10km tu kutoka city centre.
SLUMS ni ishara ya kuwapo watu wa kipato cha chini katika jiji. Tukikataa slums zisiwepo labda tupandishe hadhi ya eneo. Kusiwe na genge na bei Za bidhaa ziwe juu zaidi. Slums zenye we zitakimbia expensiveness
 
Ndugu yangu wale wenzetu ex ni jadi yao lakini kwa sisi waafrica wengi wanafanya kutafuta ridhiki tena cha kusikitisha kabisa mfano dar wanawake wengi dar wanauza ili walishe familia zao.
Hizi sio kesi za Dar!. Hizi ni kesi za urbanization.. Mana miji yote dunia I Zina experience hiyo. Mbona USA na Japan watu Wana cheza ex kwenye public train
 
Ndugu yangu wale wenzetu ex ni jadi yao lakini kwa sisi waafrica wengi wanafanya kutafuta ridhiki tena cha kusikitisha kabisa mfano dar wanawake wengi dar wanauza ili walishe familia zao.
Watu wa hivyo hata maerkeni wapo. Minority groups ndio shughuli zao. Hiv unajua marekani ukiwa sehm ya minority unapata tabu kama uko ng'wanza au ushirombo tu
 
Dar hakuna joto kwa wenye uwezo, Dar hakuna kugombania daladala kwa wenye uwezo, wikiendi yote hii ndefu ya pasaka, kuna watu hawajatoka majumbani mwao, ni mwendo wa kiyoyozi, DSTV, na kutafakari afanye nini na atoke na mchongo gani baada ya Pasaka. Hata wakitoka ni mwendo wa kula bata tu, hiyo habari ya joto haipo. Unapolalamika na kukimbia Dar eti maisha magumu sio sahihi.

Nchi nyingi za Ulaya wakati wa msimu wa kipupwe (Winter) baridi ni kali sana, unaweza hata kupoteza maisha kwa baridi, lakini watu hawakimbii miji yao kwasababu ya baridi..... WANAPAMBANA, wanafanya kazi kwa bidii, kila nyumba inawekwa mfumo wa joto ambapo ukiwa ndani mwako baridi haikusumbui, lakini lazima ulipie gharama za kudumisha mifumo hiyo ya joto majumbani.

Dar sio tatizo, bali tatizo ni mzunguko wenu wa kipato..... tafuteni fedha, Dar haina shida.
 
Dar watu hawashibi, vijana wengi ni madarali, Mji umejaa Machawa kibao na Midananda,
Dar ndo kuna uchawi kushinda ata Mikoani watu wanapigana Miba balaah.
 
Mfalme anakula Bata na Kukimbizana na sungura huku anaowatawala hoi
a-london-slum-family-with-all-their-possessions-in-the-street-following-eviction.jpg

Aisee kumbe sio kwetu tu
 
Lakini bado tu sisi tunafeli hatuna mipangilio ya miji yetu, unaongeleaje suala la slums sehemu kama manzese, buguruni?.
Watu wa hivyo hata maerkeni wapo. Minority groups ndio shughuli zao. Hiv unajua marekani ukiwa sehm ya minority unapata tabu kama uko ng'wanza au ushirombo tu
 
Mkuu mifano mibaya yote ni mbagaraa😔😂🤣🤓
Hawa wa tabata Bima na goba wanadai kwao sio slums achana nao. Wanajua wanatudanganya wakati
Lakini bado tu sisi tunafeli hatuna mipangilio ya miji yetu, unaongeleaje suala la slums sehemu kama manzese, buguruni?.
SLUMS ni tatizo Kwa model ya city standard za ulaya. Tunafananisha miji yetu na yao. Miji yao inatumika kama picha ya kujenga miji yetu huku tu nasahau historia zetu, uchumi wetu na tamaduni za muafrika. Slums huwezi kuziondoa kirahis kama unavyotaka na kupanga.
slums ni kesi ya watu wa chini mjini.. Ukiqeza kukontro watu wa Hali ya chini wasiishi mjini slums hutaziona
 
Vijana wengi na watu wa mikoani, na pengine kwa kukosa Exposure hudhani Watu wanaoishi Dar wanafaidi sana pengine kwa Maisha mazuri, hali ya hewa nzuri na pesa za kukidhi kila mahitaji Yao.

Lakini asilimia kubwa ya watu Dar es salaam wanaishi mazingira magumu sana, Chumba kimoja kilichojaa ndoo na madumu ya maji, joto zaidi ya Nyuzi joto 30, Kulala na watoto chumba kimoja, Mvua zikinyesha maji yanavujia ndani pengine na Kusomba Nyumba kabisa.

Wakazi wengi wa Dar es salaam wanafanya shughuli zao zaidi ya km 10 kutoka kwenye makazi yao, na utakuta anauza utumbo wa kuku au anaenda kuuza bidhaa za Muhindi k.koo.

Kero haiishii tu kwenye Makazi. Mtu ataamka saa 10 alfajiri na atapanda daladala iliyojaa kama wako Jehanamu, kama ulinyoosha shati lako basi tegemea ukishuka litakuwa limesagwa kama ulikuwa unapigana. Mateso yako pale pale wakati wa kwenda na kurudi kazini.

Mara nyingi watu hawa huhangaikia kipato cha kati ya elfu 10 hadi elfu 30 kwa siku (ukiachilia Mbali ambao wameajiriwa na kufanya biashara ambao hawa ni tabaka la kati).

Kwa kuwa Dar ina shughuli nyingi za kujipatia hivi vipato vidogo vidogo, bado vipato hivi havitoshi kumfanya mtu akaishi maisha ya ahueni kwa maana ya kujenga Nyumba yake mwenyewe ambayo ina viwango na ubora mkubwa kama mikoani.

Kwahiyo pesa nyingi wanayopata vijana huishia kununua I phone na TV kubwa kuweka kwenye magheto yao ya chumba kimoja.

Kikubwa ukiwa na Maarifa na ubunifu katika utafutaji unaweza kupata mafanikio zaidi ukiwa mikoani zaidi hata ya Dar wanakokimbilia vijana.

Wanawake wa Dar ni waswahili na wanavaa mawigi ya rangi rangi, kope ndefu bandia, Matapeli wa Mapenzi, Wanashindana na Mashosti zao kuhakikisha wanahongwa zaidi kuliko rafiki zao na IQ zao ni ndogo.

Hiyo ndiyo Dar es salaam ambayo wakazi wake hujaa dharau wanapoenda Mikoani wakati hawana kitu.

Samwaleku.
Ni kweli 89%
 
Iondoe Japan hapo mzee hakuna slum kule .hata Brazil na India ni baadhi ya miji
Japan wako smart kuliko hata hao wazungu wenyewe wa ulaya. Hao jamaa hawana slum na labda hadi mwisho wa Dunia hawawezi kuwa na slums.
Wao wako wengi tu mjini Tokyo na sio kwamba wako na slums. Never.
 
Japan wako smart kuliko hata hao wazungu wenyewe wa ulaya. Hao jamaa hawana slum na labda hadi mwisho wa Dunia hawawezi kuwa na slums.
Wao wako wengi tu mjini Tokyo na sio kwamba wako na slums. Never.
Sawa kabisa
 
Ulitakiwa ukitoka hapo mpeleke oysterba,masaki,mbezi beach them mdump mtaa wa congo
Watu wengi wanaoiponda Dar wana ndugu masikini, hivyo wanafikia sehemu duni, zisizo na miundombinu

Mbezi Beach, Mikocheni B, Masaki, O'Bay, Mindu, Muhimbili, Kijichi, Magomeni ya Upande wa KKOO

Hizo ni chache
 
Nakubishia mpaka kesho mfano hapa Mwanza nyumba ni kali kuliko hata hupo Dar!
Mfano huku Ilemela kuna nyumba kali kuzidi hata kinyerezi wewe unaleta ngonjera!
Tukubali tu Dar ni ya wachache wengi mahayawani!
Kha hebu onesha huo ukali wa nyumba
 
Wanaposema dar hakuna maskini wamejumlisha na pato la bakhresa na mo na matajiri wengineo...ila ukiniuliza mi binafsi kwa hali hali halisi ninayoiona dar maskini wanaweza kufika hadi 70% ya wakazi wa dar, wananchi wengi wa dar wanaishi maisha magumu mno.
Kwamba zaidi ya watu 3.5mil wana maisha magumu?
 
Back
Top Bottom