MaIsha ya dar vs mikoani

chamaclotus

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
971
1,969
Kwema wakuu,
Hasa kwetu sisi vijana ambao bado tunatafuta, we unaona wapi bora kati ya dar es salaam na mikoani.
Karibu
 
Kwa mtu asiyekuwa na mtaji Shamba Kunamfaa kwani Kuna fulsa nyingi za kuanza nazo.

Kwa mwenye mtaji Dar panamfaa kukuza mtaji wake kwa haraka.

Yote hayo yanatemea hiari ya mtu.
Kuna wengine hawezi kuishi Shamba au Mjini katika na kufanya harakati zao.
Kuna watu wa Mjini tu.
 
Kilimo gani hicho kisichohitaji mtaji? Ambacho asie na mtaji anaweza akafanya?
 
Kilimo gani hicho kisichohitaji mtaji? Ambacho asie na mtaji anaweza akafanya?
Mi sijataja kilimo.
Nimezungumzia fulsa za kuanza nazo bila mtaji Mkubwa

Kuna kuvuna Asali bure msituni na kuiuza.
Kuna kufanya uvuvi hasa kwenye vyanzo vya maji kama Mito, Maziwa nk.
Kuna kuuza mkaa, miti ipo ya Bure.
Kuna uwindaji wanyama Nk.

Kilimo, kuna baadhi ya maeneo Yana mvua za kutosha na hayahitaji mbolea za kununua kukuzia mazao.
Mfano maeneo ya, Idodoma, Itipi, Malolo, Nziha, Kilosa na Ifakara Mkoa wa Morogoro
 
Kuhusu kuvuna asali siwezi kuzungumzia maana sijui lolote,ila hayo mengine yaliyobaki yanahitaji mtaji,tena mtaji wa uhakika maana unaweza usipate matokeo kwa wakati na mda mwingine hasara kabisa
 
Kwema wakuu,
Hasa kwetu sisi vijana ambao bado tunatafuta, we unaona wapi bora kati ya dar es salaam na mikoani.
Karibu
Mkuu nimefika Dar mwaka jana mwishoni! Ukweli usemwe, hapa sitoki, nastaafia hapa hapa hata iweje! Dar fursa kibao ni wewe tu!! Nilikuwaga sijui kama Dar wanafakamia hivyo kuku wa kisasa! Niikuwaga sijui kama nyama ya ng'ombe Dar inauzwa 10k kwa kilo tena ile ya daraja la chini kabisa!!
 
Back
Top Bottom