Dar: Hussein Ramadhani akamatwa kwa kujifanya Askari Polisi. Na Maila Majula akamatwa kwa kudanganya kaibiwa gari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Dar-es-salaam 15/02/2022
JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM
LIMEMKAMATA MTU MMOJA KWA KUJIFANYA ASKARI POLISI

Tukio hilo limetokea tarehe 09.02.2022 majira ya saa sita na nusu mchana huko maeneo ya Vingunvguti Mtakuja ambapo alikamatwa Hussein Ramadhani, miaka 30, Mzaramo na mkazi wa Sinza akiwa amevaa sare za za Jeshi la Polisi (Jungle Green) akijifanya Askari Polisi na kukamata watu ovyo huku wakati mwingine akijihusisha na matendo ya unyang`anyi wa kutumia nguvu akiwa amevaa sare hizo.

Upekuzi zadi ulimkuta akiwa na vifaa vimgine kama Buti za Jeshi la Polisi, kadi za Benki NMB na CRDB, kadi ya Mpiga kura na kadi za NSSF zenye jina la Florence Victor Kiondo ambazo zinachunguzwa jinsi alivyozipata na kuhusishwa na tukio la kihalifu. Hata hivyo kumbu kumbu zinaonesha mtuhumiwa huyo alishawahi kufungwa kwa makosa mbalimbali na taratibu za kisheria zina fanyika ili kumfikisha tena Mahakamani.

Mtuhumiwa alishawahi kufungwa jela miaka 4 CC no 138/2018 kwa kosa la Kujeruhi akatumikia kifungo katika Magereza ya Mkuza Kibaha, Rwanda

Mbeya na kumalizia kifungo Gereza la Kitai Mbinga Mkoani Ruvuma. Pia alishawahi kuhukumiwa kifungo nje miezi 6 na Mahakama ya Mwanzo Buguruni CC NO 893/2021 tarehe 19/08/2021 kwa kosa la wizi

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam litaendelea kufuatilia watu mbalimbali wanaojifanya watumishi wa mamlaka za Serikali na kuwabughudhi raia wakati wao si mamlaka hizo husika

Katika hatua nyingine , Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam eneo la Kariakoo Mtaa wa Msimbazi na Livingstone limemkamata Maila Majula, Mjita, Mkristo, miaka 29, Biashara, mkazi wa Makongo juu kwa kutoa taarifa za uongo katika kituo cha Polisi Msimbazi za kuibiwa Gari lake namba T.303 DPS aina ya Toyota IST rangi ya Bluu.

Uchunguzi umebaini kuwa mtuhumiwa alipewa T.shs Milioni kumi na kaka yake ili akaziweke Benki matokeo yake akazitunia kwa matumizi yake binafsi na kuamua kutengeneza tukio la kufkikirika kuwa pesa ile na gari viliibwa wakati yeye aliposhuka kwa muda na aliporudi hakukuta gari iliyokuwa na pesa .

Baada ya kumtilia mashaka mtoa taarifa ilibainika kuwa taarifa hizo ni za uongo, na ilibainika gari hilo alikuwa amelificha maeneo ya Tabata kwa Swai ambako lilipatikana kabla ya kwenda kituoni kutoa taarfa za kuibiwa kwa Gari hilo.

Tarifa nyingine ya uongo ilitokea tarehe 10.02.2022 majira ya saa majira ya saa tisa Alasiri ambapo alikamatwa Mohamed Bakari Kisungura, Mndengeleko, miaka 37, Mkazi wa Kisemvule kwa kutoa taarifa za uongo katika kituo cha Polisi Msimbazi kwamba eneo la mataa Mkunguni alivamiwa na watu wawili waliokuwa na Pikipiki na kumtishia kwa silaha aina ya Bastola na kumpora pesa kiasi cha T.shs 37,000,000/= ambazo alipatiwa na mwajiri wake Bariki Ngairo, Mkinga, Mkristo, Biashara, miaka 42, mkazi wa
Kitunda ili azipeleke Benki ya NMB tawi la Kongo.

Upelezi ulifanywa na kubaini kuwa hakukuwa na tukio la kutishiwa kwa Silaha ,ndipo ikabainika kuwa mtu huyo alikutana na watu wawili benki kati yao mmoja wao ni jinsia ya kike ambao walijifanya kuwa ni wageni na walihita ji kubadilisha fedha za kigeni hivyo walimshawishi na kutoka nao nje ya Benki hiyo na kuingia mtaa wa Mkunguni wakiwa njiani walimpatia mfuko wa khaki uliokuwa na karatasi zilizotengenezwa kwa mfumo wa fedha za kigeni (USD) ili akazibadilishe kwa hela za kigeni na kukabidhi mfuko wa fedha uliokuwa na pesa taslim Tshs. 37,000,000/= ,Alivyobaini ameibiwa kiutapeli akaamua kutengeneza tukio la kufikirika la unyanganyi wa kutumia silaha

Mafanikio ya Oparesheni balimbali
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam llinaendelea na Oparesheni, Doria na misako ili wananchi waendelee kuwa salama na watuhumiwa mbalimbali wamekamatwa akiwemo Zulfa Ramadhani, miaka 20 , Mzaramo na wenzake 75 wakiwa na madawa ya kulevya kete 15 Heroine, Bhangi Puli 396 , Kete 1380 na Misokoto ya bangi 1200

Pia wamekamatwa Watuhumiwa 9 wa wizi wa pikipiki huku pikipiki nane zilizokuwa zimeibwa maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es salaam zikiwa zimepatikana

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa katika hatua nyingine kumkamata Dotto Japhari, miaka 39, Mpogolo, Mkazi wa Tabata Kimanga na wenzake 12 wakiwa na mali za wizi TV Flatscreen tatu zenye ukubwa tofauti Deki 2 mbili , Friji ndogo 1, Generator 2, Ving`amuzi 5 vya AZAM, pia wamekutwa na Grender 3 za kutobolea ukuta,vifaa mbalimbali vya kuvunjia , spika 10 za Subwoofer, mabegi madogo manne ya wizi. Jeshi linanawaomba wananhi waendelee kutoa taarifa ili lichukue hatua za kisheria za kuzuia vitendo vya kihalifu

Muliro J MULIRO– ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
 
Ukute na wao polisi wametengeneza haya matukio ya kufikirika ili tusahau yaliyopita (LINDI, MASOKO KUUNGUA NA MAUAJI KILA KUKICHA)
 
Ila wenye pesa wana moyo.

Bosi unamtuma mtu akupelekee benk pesa zako shilingi milion 37.

Na mwingine nae kamtuma mtu ampelekee benk shilingi milion 10
Mkuu inawezekana tena sana, nilishawahi fanya kazi sahemu nilikua napewa hadi 30m nipeleke bank. Ni uaminifu tu
 
Sasa polisi mbona wanashindwa kutimiza jukumu lao kwa mtuhumiwa wa 37m kwanini wameshindwa au kuendelea kuwatafuta hao waliomtapeli Mana mpaka kutangaza inamaanisha Mambo yameisha katika uchunguzi, hapo naona polisi wameamua kuhamisha goli Ila mechi bado
 
hajakosea maana binafsi nikiona mtu amevaa hizo sale mi namuona ni mwizi tu kama wezi wengine ...

laptop yangu,simu na hela zangu niliibiwa na watu waliovaa hizo sale tena nikawekwa na seli kabisa wiki nzima so hakuna jipya hapo
 
Tangu nianze kusoma habari za police, hii leo imekuwa ndefu zaidi.
Polisi wanaweza sema tu jamaa kwa kupenda pesa ni balaa
 
Back
Top Bottom