Dar: Hospitali ya Dar Group inanuka kinyesi kila sehemu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Salaam Wakuu,

Usalama wa wagonjwa hatarini katika hospitali ya Dar Group iliyopo Tazara Jijini Dar es Salaam.

Mazingira yote ya hospitali yananuka kinyesi kutokana na kutozibuliwa Kwa chemba za kuhifadhia maji taka.

Wagonjwa Wengine wanashindwa kuvumilia na kuondoka kwenda kwenye hospitali nyingine.

Uongozi wa Hospital unadai kwamba tatizo watalifanyia kazi.

Wafanyakazi wa hospitali pia wanasema hali zao ziko hatarini kutokana na kufanya kazi katika mazingira magumu na yasiyo salama Kwa afya zao.

Hospitali ya Dar Group ilizinduliwa mwaka 1971 na baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere
 
Back
Top Bottom