Dar es Salaam: Nyumba yapigwa mnada kwa kushindwa kulipa milioni 7

Naughty by nature

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
2,128
2,356
Dar es Salaam. Familia ya Festo Aaron, inayoishi Kimara Bonyokwa iko njia panda baada ya kukosa makazi kutokana na nyumba yao kupigwa mnada na taasisi ya Uwezo Financial Service kwa kushindwa kurejesha deni la Sh7 milioni.

Mwaka 2020 familia hiyo yenye watoto watano ilikopa Sh6 milioni katika taasisi ya Uwezo inayodaiwa kuwa na uhusiano na waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa makubaliano ya kurejesha Sh7 milioni ndani ya mwaka mmoja.

Taasisi hiyo imekuwa ikikopesha fedha hizo kwa kuzingatia sifa mbili, ambazo ni mkopaji awe muumini wa dhehebu hilo awe mwaminifu katika kutoa fungu la kumi kila mwaka.

Akizungumza na Mwananchi, Festo alisema mwaka 2020, mke wake Happy Josia alikopa kwenye taasisi hiyo Sh6 milioni lengo wakipata fedha hizo wapate mtaji wa kuanzisha biashara.

“Makubaliano yalikuwa kurejesha riba ya Sh1 milioni kwa kiasi tulichokopa, tulitakiwa kurejesha Sh7 milioni ndani ya mwaka mmoja,” alisema Festo.

Amesema fedha hizo walizielekeza kwenye biashara ya nguo na viatu katika duka waliloanzisha maeneo ya Kimara lakini hata hivyo janga la Uviko-19 lilotokea kwa mwaka huo lilisababisha biashara yao kwenda mrama.

“Tulipambana na kufanikiwa kufanya rejesho moja Sh500,000 lakini hata hivyo mambo yalizidi kwenda ovyo ndipo tulipoenda kufanya mazungumzo na taasisi kuwaeleza hali halisi na wakatuongezea muda,” amesema.

Festo amesema miezi michache baadae walipotaka kwenda kulipa deni hilo waliambiwa riba imeongezeka hadi kufikia Sh10 milioni kutoka Sh7 milioni jambo lilowashangaza na kwenda kwa wachungaji wa Kanisa hilo lakini hata hivyo hawakupata msaada.

“Hadi mwanzoni mwa mwaka huu tuliambiwa deni riba yake imefikia Sh17 milioni hivyo tulishangaa na kuwauliza imefikaje? Wakawa hawataki mazungumzo tena ndipo wakaanza kutangaza mnada nyumba yetu na wakauza kwa Sh 23milioni,” amesema.

Happy ambaye ndiye aliyekopa amesema anashangazwa na uharaka wa kuiuza nyumba hiyo.

“Tunaziomba mamlaka kuongea na taasisi hii ikubali kutuachia nyumba yetu na iridhie kurejesha deni la msingi la Sh7 milioni tulilokopa ili tuendelee na maisha,”amesema.

Mwananchi, lilizungumza na Mchungaji wa kiongozi wa Kanisa la TAG Kimara, Ruth Temu amesema taarifa za familia hiyo kukutana na kadhia hiyo alishazipata na ana mpango wa kwenda kuzungumza nao.

“Siwezi kusaidia chochote kuhusu hili sakata japo taasisi iliyokopesha naijua lakini masharti waliyokubaliana siyajui kwa hiyo siwezi kuwasaidia chochote,” amesema Temu.

Alipotafutwa ofisa mikopo wa taasisi ya Uwezo, Patro Mwashambwa alikiri kuidai familia hiyo huku akieleza suala la nyumba ya familia hiyo kupigwa mnada haihusiki kwani iliyofanya hivyo ni kampuni za ufilisi iliyopewa jukumu hilo na Mahakama.

“Siwezi kueleza sana, tunawadai na nyumba yao kupigwa mnada imefanywa na taasisi ya ufisili waliopewa jukumu hilo na Mahakama kupata fedha za kulipa deni hili,” amesema.

Naye Ofisa kutoka taasisi ya Ngomeni iliyopewa jukumu la kupiga mnada nyumba hiyo, Kristian Samweli amesema walitekeleza amri ya mahakama baada ya mdaiwa kushindwa kulipa deni analodaiwa.

“Sisi tumeuza na tulifuata taaratibu zote zinazotakiwa ikiwepo kumpatia notisi ya kumtaka alipe lakini alishindwa, pia tuliwafahamisha viongozi wa Serikali za mitaa, juu ya kusudio la kuuza nyumba hiyo, kimsingi tuliiuza kwa Sh23 milioni baada ya kufuata utaratibu” amesema
 
Dar es Salaam. Familia ya Festo Aaron, inayoishi Kimara Bonyokwa iko njia panda baada ya kukosa makazi kutokana na nyumba yao kupigwa mnada na taasisi ya Uwezo Financial Service kwa kushindwa kurejesha deni la Sh7 m
Mkuu hivi huyu Festo ana undugu na Festo ndugage the disgrace cabinet minister?

Kwasababu majina yao ya kwanza yanafanana.
 
Tukiwaambia Riba haifai mnatuona ss washamba halafu ni kanisa na waumini wake yaani ndo uone sasa jinsi Wagalatia walivokua hawana huruma na waumini wao

Laiti hii ingetokea kwa Waislamu comments zingekua zishafika 1000 uko ila kwasababu nyani haoni.

Basi wacha wamalizane wenyewe
 
Back
Top Bottom