Dar es Salaam Mpya: NSSF kuanzisha miradi mikubwa jijini; Mwisho wa malori kuingia jijini wawadia

naogopa pale wateja wa nssf watakapoanza kukosa mafao yao sababu tu mtu mmoja anaitwa dau anatafuta umaarufu at their expense..i hope he knows what he is doing
 
Dr. Dau kwa nini usianze kufukuza mzee mmoja mpuuzi, mtukana watu, mpenda rushwa wa pale Ubungo ana kisahara na ana asili ya Musoma! I hate that stupid man. Anatukata na kufokea watu kama . . . . . Aaargh!!
 
Jinsi Dr. Dau asivyopenda rushwa.....nashangaa yule mzee amewezaje kudumu pale....au ndo mtaalamu wake? mana ameshafikishiwa malalamiko kuhusu huyu mzee zaidi ya 1,000
 
naogopa pale wateja wa nssf watakapoanza kukosa mafao yao sababu tu mtu mmoja anaitwa dau anatafuta umaarufu at their expense..i hope he knows what he is doing

Hivi ile working doc ya SSRA in the name of investment guidelines kwa social sec funds bado inafanya kazi au haijaanza kutumika rasmi?

Hizi investment je zina baraka za SSRA?

Hivi mwisho wa siku mfuko ukishindwa kulipa anayeshitakiwa ni SSRA au mfuko? Kama ni mfuko kazi ya SSRA ni nini?

Naomba mnielimishe wana bodi.

Queen Esther
 
Hivi hii NSSF wanachama wake wako DSM tu! Daraja la Kigamboni DSM, Nyumba za bei nafuu DSM, Reli DSM, Bandari kavu DSM Ooops Kisarawe? Je wanachama wa mikoa mingine hutataki hizo nyumba za bei nafuu?

Halafu nani amempatia mamlaka hayo ya kutumia pesa zetu atakavyo? Wanachama tunachotaka ni kuboresha formulae ya kukokotoa mafao ya uzeeni yafanane fanane na ya PSPF.

Sijui hili suala tunaweza kuli solve vipi kwenye katiba mpya? Mkurugenzi wa NSSF na mifuko mingine ya jamii achaguliwe na wanachama wenyewe badala ya kuteuliwa na RAIS ambaye yeye ni mwanachama wa PSPF.

Hivi hela zetu (NSSF) tulizotumia kujenga UDOM serikali imeshaanza kuturudishia?, Maana report ya CAG ya 20012 inaonesha Serikali imeshindwa kurudisha hiyo pesa na mifuko hiyo (NSSF, PPF) iko taabani kifedha na ndiyo ulikuwa mwanzo wa muswaada ule wa kuzuia FAO LA KUJITOA.

Kama ni hivyo kwanini Dr. Dau aendelea kuifadhili serikali ambayo it is a bad DEBTOR. Huyu Dr. Dau kwanini anajipendekeza sana kwa serikali at the expense ya michango ya wanachama?
 
Hivi wadau kwa kutumia akili ya kawaida ni kweli uwepo wa bandari na shughuli ndiyo chanzo kimojawapo kinachohusika na msongamano Dar??? bandari inatumia njia zipi kwa ajili ya shughuli zake??? Hizo fedha kwanini zisitumike angalau kuhamishia baadhi ya ofisi za serikali kwenda Dodoma?? Tutatapanya fedha nyingi sana kwenye ujenzi wa njia za juu. .... mabasi ya kwenda kasi.....na siasa nyinginezo za ujenzi lakini mwisho wa siku tutajikuta tunaongeza matatizo mengine......
 
Kupunguza mrundikano bandarini na foleni, mbona jibu ni rahisi. Vitengo vya bandarini na TRA vifanye kazi hadi usiku. Malori yaanza kusafiri kuingia mjini na kutoka bandarini kuanzia saa nne usiku. Mbona hiyo ni rahisi sana. Taa za barabarani ndizo ziongoze magari, traffic police washughulike na wanaotanua na kutoheshimu taa.
 
Mpango wa Dr Dau ni mzuri lkn wasiwasi wangu ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi? au ni kujinyakulia Prime Area kiujanjaujanja? kwanini asikae na wataalam wa ujenzi tukajenga reli za kisasa toka Kongowe - Posta, posta bunju na kibaha - posta kwa kuanzia ili tuone mradi utakavyofanya kazi na sio kwenda kuvunja nyumba za watu wa Manzese na Vingunguti kwa njia ya dhuluma suluhisho ni RELI SERA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA ILIWAPA WATU ELIMU YA KUJILETEA MAENDELEO WENYEWE WATU WAKAJENGA VIPI LEO WAONDOLEWE?

DR DAU NA SERIKALI WAENDE LILONGWE WAJIFUNZE JIJI LILE LILIVYOPANGWA NA KUENDELEZWA WAACHE UJANJA UJANJA, KAZI YA SERIKALI NI KUJENGA HOSPITAL, SHULE VYUO, VITUO VYA POLISI NA FIRE NA MIUNDOMBINU NA SIO KUTUMIA SHIRIKA LA NSSF KUWATOA WATU KTK SEHEMU ZAO ZA ASILI,

WHO BEHIND OF THIS CURTAIN? DR. DAU
 
Wao kila kitu kimepitwa na wakati,mbona CCM imepitwa na wakati hawaibomoi na kuijenga kisasa?.

kwa hili mkuu itakuwa baadae sana kwani wote hao wanafanya kwa ajili ya CCM mkuu isingekuwa hivyo mbona tushakizika..
 
Jinsi Dr. Dau asivyopenda rushwa.....nashangaa yule mzee amewezaje kudumu pale....au ndo mtaalamu wake? mana ameshafikishiwa malalamiko kuhusu huyu mzee zaidi ya 1,000

dah! Nadhani kuna kitu na dr. Dau sababu mama Musika (manager wa Ubungo) ni mtiifu na mpenda haki. Lenyewe linapinga hadi maamuzi ya Manager wake. Kuna kitu hapo, ngoja tutafute namba yake ya simu tufanye tracking
 
Hivi hii NSSF wanachama wake wako DSM tu! Daraja la Kigamboni DSM, Nyumba za bei nafuu DSM, Reli DSM, Bandari kavu DSM Ooops Kisarawe? Je wanachama wa mikoa mingine hutataki hizo nyumba za bei nafuu?

Halafu nani amempatia mamlaka hayo ya kutumia pesa zetu atakavyo? Wanachama tunachotaka ni kuboresha formulae ya kukokotoa mafao ya uzeeni yafanane fanane na ya PSPF.

Sijui hili suala tunaweza kuli solve vipi kwenye katiba mpya? Mkurugenzi wa NSSF na mifuko mingine ya jamii achaguliwe na wanachama wenyewe badala ya kuteuliwa na RAIS ambaye yeye ni mwanachama wa PSPF.

Hivi hela zetu (NSSF) tulizotumia kujenga UDOM serikali imeshaanza kuturudishia?, Maana report ya CAG ya 20012 inaonesha Serikali imeshindwa kurudisha hiyo pesa na mifuko hiyo (NSSF, PPF) iko taabani kifedha na ndiyo ulikuwa mwanzo wa muswaada ule wa kuzuia FAO LA KUJITOA.

Kama ni hivyo kwanini Dr. Dau aendelea kuifadhili serikali ambayo it is a bad DEBTOR. Huyu Dr. Dau kwanini anajipendekeza sana kwa serikali at the expense ya michango ya wanachama?

Dar! Dar! Dar! Dar! Why not Kigoma?
 
onyo! alimradi tu kusiwe na sura ya kisiasa au ni upigaji wa hela za uchaguzi 2015
 
sijui lakini.....
Nakupongeza sana Dr. Dau kwa maono yako na uongozi wa NSSF. Udhubutu wenu unatia hamasa, lakini pia nakumbuka nilipata kusoma gazeti nililonukuu ukilalama kuhu malipo kutoka serikalini zaidi ya bilion300 ambazo serikali haijalipa. Hizi ni hela za watanzania, sio za serikali wala zako au hata wafanayakazi wengine wa NSSF. Ni miliki ya wanachama. Kwa kuzingatia hayo, ebu tazama hoja zangu binafsi.
1. Je recorvery status imefikia wapi?
2. Uwekezaji katika bandari nauunga mkono, ila najua kisarawe hamna barabara madhubuti ya kuelekea mikoa mingine ya tanznia. Je katika hilo mnasemaje?
3. Naelewa kuna mizigo mingi inayoshushwa bandarini ya dar ambayo utumika hapa dar. Barabara ya kwenda kisarawe ilivyo kwasasa imeshaelemewa, je mnampango gani kuhusu miundo mbinu hasa kwa magari ya kurudisha mizigo jijini?
4. Mheshimiwa naomba utueleze mpango wa kujenga reli na kuimalisha usafiri wa treni katika jiji la dar na majiji mengine imeishia wapi. Tulisikia ahadi nyingi waktai wa uchaguzi na hizo ahadi zikasaidia kuongeza idadi ya kula kwa baadhi ya wagombea. Je huu mpango mpya ni wa ukweli au ni mipango ya kuleta episode mpya kama njia ya kuwafumba macho watz?
 
Nakumbuka hata John S Malecela akiwa madarakani ashawahi kusema kabla hajaondoka madarakani, Dar es Salaam itakuwa na mtandao wa treni za mjini
 
Back
Top Bottom