Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,915
- 30,259
Wengi wetu tumekulia Dar es Salaam na tumeuona unazi wa Simba na Yanga ulivyokuwa.
Nakumbuka siku kama ya leo ambayo sasa tunaita Dar es Salaam Derby ukipenda Kariakoo Derby ilivyokuwa.
Nakumbuka pale mnadani Mafia na Msimbazi vile vitezo vilivyokuwa vinamwaga moshi wa ubani toka asubuhi.
Wakati ule Yanga wako Sukuma na Sunderland yaani Simba wako Congo.
Vilabu viko jirani kwa mwendo na mbio zetu za kitoto dakika kumi zilitosha kufika Yanga kuangalia kuna nini na ukarejea Sunderland kutazama hali ya hewa. Uwanja ulikuwa Ilala Stadium.
Watangazaji wa TBC wana kijibanda kidogo juu tuu ya jukwaa la watazamaji.
Dar es Salaam ilikuwa ndogo sana.
Milango ya kuingia uwanjani midogo sana inaruhusu kuingia mtu mmoja mmoja na wachanaji tiketi unawaona hapo.
Wauza soda za Portelo kutoka kiwanda cha Abdulrasul wanazunguka uwanjani na Cocacola pia walikuwa wanashusha makreti kwa makreti ya mbao nyuma ya uwanja.
Kuna vijana wakiuza soda hizo kwa kamisheni. Nakumbuka gari la soda za Cocacola la Mzee Maukwe.
Navikumbuka vyumba vya wachezaji...vyumba vidogo sana.
Minazi mingi ilikuwa imezunguka uwanja na kuna waliopanda minazi hii kuangalia mpira.
Hali imebadilika sana.
Kuna maendeleo makubwa katika soka.
Unazi pia umechukua sura tofauti kabisa.
Leo sihitaji kupiga zile mbio kwenda club au kupita mnadani kupata, "mood," ya "game."
Simu yangu janja inanitosha kabisa kusikiliza na kuona watani wanavyotupiana makombora na kwa kweli inaongeza ladha ya mchezo.
Hakika tumetoka mbali toka enzi za akina Mnuwili, Ugundo (Dr. William), Ayub Kiguru, Bin Dossi, Jumanne Kisukari...Allah awarehemu...viongozi kama Shebe, Kitwana Ibrahim...muhimu sana TFA itengeneze Ukumbi wa Historia ya Mpira na historia ya Wanazi wa Simba na Yanga.
Hii ni historia ya pekee kabisa.
Leo tuko kwenye "electronic tickets," na mpira uko kwenye TV na hii imetuletea wapenzi wa soka wa kwenye makochi majumbani, Uingereza wanawaita, "arm chair supporters," na wanajaribu kuwatoa vitini kuwaleta uwanjani.
Club zinataka kuongeza ''gate collection.''
Vilabu hivi Simba na Yanga vina historia kubwa sawasawa na mji wake wa Dar es Salaam.
Timu iliyoshinda Gossage Cup 1949 picha hii walipiga Ilala Stadium.