Derby ya Kariakoo inapoteza mvuto

ngara23

JF-Expert Member
Aug 31, 2019
2,417
5,294
Kesho Tanga kuna mchezo wa watani jadi Simba dhidi ya Yanga lakini naona huu mchezo umedorora hamna shamra shamra na mtaani watu hawazungumzii hili tukio kubwa la kimichezo la kesho

TFF imeweka kiingilio elfu 30 lakini nina wasiwasi kama uwanja utajaa kutokana na derby kukosa mvuto

Sababu kubwa nadhani kwakuwa hizi team zinakutana mara nyingi kwa msimu kuliko timu zingine, kwaku TFF wameona ndo gap la kupiga wasijue kuwa kukutana mara nyingi watu wanazoea na baadae wanauchukulia mchezo huu kama mechi zingine

Siku hizi sioni watu wakipata msisimko hadi kuzimia uwanjani kama zamani

Derby ya kariakoo ikiendelea kufulia ni wasaa wa kuhamia mashemeji derby pale Nairobi ndo itakuwa derby bora ukanda wete CECAFA

TFF msipende kuzitumia hizi timu kupiga hela na mkapoteza ladha ya Derby.

Itawachukua miaka kuifufua tena.
 
Wabongo mnazingua kwa Ujuaji usio na msingi.
Kuna namna nyingi za kuonesha una " akili " au " Upeo" tofauti na hii ya kukosoa kila kitu.
1. Simba na Yanga ni timu kama timu Zingine.

2. Kanuni za Ligi kuu zinafahamika.
Bingwa wa FA na Bingwa wa Ligi watacheza Mechi ya Ngao ya hisani kuashiria kuanza kwa ligi ( saiv kanuni imerekebishwa zimekuwa team nne badala ya 2).

3. Haijalishi ni team gani zimechukua kombe na kushika nafasi za juu Ngao ya jamii lazima ifanyike.

4. Uwezo wa uwanja wa mkwakwani ni Mdogo, ukiweka kiingilio Kidogo unaweza sababisha Vurugu. Weka kiingilio kikubwa kupunguza watu.
 
1)Simba na Yanga zinawaza kimataifa

2) somo la takwimu sio la kila mtu.

Inatakiwa uje na uchambuzi ukizingatia kuwa hiyo mechi imeshtukiza tofauti na zile ambazo zinafahamika mwezi kabla kwamba Yanga vs Simba zitacheza.

Kwamba ilipotokea Yanga vs Simba ikashtukizwa mechi hali ilikuwaje kulinganisha na sasa
 
Bingwa wa league ni yanga
Bingwa wa FA ni yanga
Kwanini bungwa wa Ligi kuu asicheze na ngao ya jamii na makamu bingwa wa FA

Wanaandaa mazingira ya ligi ya ngao ya jamiu na nguvu ya waamuzi ili tu Yanga na simba zikutane
 
Wabongo mnazingua kwa Ujuaji usio na msingi.
Kuna namna nyingi za kuonesha una " akili " au " Upeo" tofauti na hii ya kukosoa kila kitu.
1. Simba na Yanga ni timu kama timu Zingine.

2. Kanuni za Ligi kuu zinafahamika.
Bingwa wa FA na Bingwa wa Ligi watacheza Mechi ya Ngao ya hisani kuashiria kuanza kwa ligi ( saiv kanuni imerekebishwa zimekuwa team nne badala ya 2).

3. Haijalishi ni team gani zimechukua kombe na kushika nafasi za juu Ngao ya jamii lazima ifanyike.

4. Uwezo wa uwanja wa mkwakwani ni Mdogo, ukiweka kiingilio Kidogo unaweza sababisha Vurugu. Weka kiingilio kikubwa kupunguza watu.
Mkuu umemaliza
 
Bingwa wa league ni yanga
Bingwa wa FA ni yanga
Kwanini bungwa wa Ligi kuu asicheze na ngao ya jamii na makamu bingwa wa FA

Wanaandaa mazingira ya ligi ya ngao ya jamiu na nguvu ya waamuzi ili tu Yanga na simba zikutane
Ni lini ilikuwa hivyo?
Hakuna kitu kinItwa makamu Bingwa.
Kama zisingekuwa team nne simba na Yanga wangekutana tu.
Kuweka timu nne kumepunguza chance ya Simba na yanga Kukutana.
 
Back
Top Bottom