SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,151
- 7,918
Wakati wengine wanaangalia tu matokeo ya uwanjani na timu inavyocheza, wengine tumekuwa tunaangalia mazoezi ya Simba na kuanza kuona mapungufu ya kitimu kuanzia huko.
Nakumbuka kuleta uzi nikikumbushia umuhimu wa "Rondo" katika kutengeneza wachezaji wenye uwezo wa kumiliki mpira. Hilo ni zoezi moja tu ila wachezaji wa Simba wanaonyesha mapungufu yao kuanzia mazoezini. Yanga wako serious sana kuanzia mazoezini hadi katika mechi zao. Simba kuna mizaha mingi na mambo ya hovyo hovyo yanaendekezwa katika ngazi zote.
Mapungufu na matatizo yaliyoonekana leo kwa Simba na ubora ulioonyeshwa leo na Yanga ni matokeo ya kile kilichokuwa kinafanyika kwenye uwanja wa mazoezi kwa muda sasa. Nilijua mazingira yanatengenezwa kwa Simba kuja kufungwa goli nyingi na mtani wake na si kwa sababu ya hujuma bali kuzidiwa mchezo.