Dar es Salaam Derby au Kariakoo Derby ukipenda ilivyokuwa 1960s

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,024
2,000
Wengi wetu tumekulia Dar es Salaam na tumeuona unazi wa Simba na Yanga ulivyokuwa.

Nakumbuka siku kama ya leo ambayo sasa tunaita Dar es Salaam Derby ukipenda Kariakoo Derby ilivyokuwa.

Nakumbuka pale mnadani Mafia na Msimbazi vile vitezo vilivyokuwa vinamwaga moshi wa ubani toka asubuhi.

Wakati ule Yanga wako Sukuma na Sunderland yaani Simba wako Congo.

Vilabu viko jirani kwa mwendo na mbio zetu za kitoto dakika kumi zilitosha kufika Yanga kuangalia kuna nini na ukarejea Sunderland kutazama hali ya hewa. Uwanja ulikuwa Ilala Stadium.

Watangazaji wa TBC wana kijibanda kidogo juu tuu ya jukwaa la watazamaji.
Dar es Salaam ilikuwa ndogo sana.

Milango ya kuingia uwanjani midogo sana inaruhusu kuingia mtu mmoja mmoja na wachanaji tiketi unawaona hapo.

Wauza soda za Portelo kutoka kiwanda cha Abdulrasul wanazunguka uwanjani na Cocacola pia walikuwa wanashusha makreti kwa makreti ya mbao nyuma ya uwanja.

Kuna vijana wakiuza soda hizo kwa kamisheni. Nakumbuka gari la soda za Cocacola la Mzee Maukwe.

Navikumbuka vyumba vya wachezaji...vyumba vidogo sana.

Minazi mingi ilikuwa imezunguka uwanja na kuna waliopanda minazi hii kuangalia mpira.
Hali imebadilika sana.

Kuna maendeleo makubwa katika soka.
Unazi pia umechukua sura tofauti kabisa.

Leo sihitaji kupiga zile mbio kwenda club au kupita mnadani kupata, "mood," ya "game."

Simu yangu janja inanitosha kabisa kusikiliza na kuona watani wanavyotupiana makombora na kwa kweli inaongeza ladha ya mchezo.

Hakika tumetoka mbali toka enzi za akina Mnuwili, Ugundo (Dr. William), Ayub Kiguru, Bin Dossi, Jumanne Kisukari...Allah awarehemu...viongozi kama Shebe, Kitwana Ibrahim...muhimu sana TFA itengeneze Ukumbi wa Historia ya Mpira na historia ya Wanazi wa Simba na Yanga.

Hii ni historia ya pekee kabisa.

Leo tuko kwenye "electronic tickets," na mpira uko kwenye TV na hii imetuletea wapenzi wa soka wa kwenye makochi majumbani, Uingereza wanawaita, "arm chair supporters," na wanajaribu kuwatoa vitini kuwaleta uwanjani.

Club zinataka kuongeza ''gate collection.''

Vilabu hivi Simba na Yanga vina historia kubwa sawasawa na mji wake wa Dar es Salaam.
Timu iliyoshinda Gossage Cup 1949 picha hii walipiga Ilala Stadium.

1550335170280.png

Timu iliyoshinda Gossage Cup 1949 picha hii walipiga Ilala Stadium.
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,451
2,000
Wauza soda za Portelo kutoka kiwanda cha Abdulrasul wanazunguka uwanjani
Umenikumbusha jambo kubwa sana mzee wangu. Hii Portelo ndio soda ya kwanza kutengenezwa hapa nchini na kiwanda cha Abdurasul and Sons LTD kilichokua pale opposite na jengo la telephone House nadhani ni mtaa qa Bridge ule

Siku moja mwaka 1996 mmojawapo ya mtoto wa Abdurasul akiiitwa Turabal( amefariki miaka takriban kumi iliyopita naye akiwa mtu mzima sana) alikabiliwa na mwanaharakati za Uzawa zilizoasisiwa na Mchungaji Christopher Mtikila, jamaa wa Kingoni na akamwambia wewe Gabacholi(Muhindi) rudi kwenu India

Basi Mzee Turab kama tulivyokua tunamwita alianza kumueleza yule mwanaharakati wa sera za uzawa kua yeye Babu yake akiitwa Sachupira alikuja Tanganyika(Kilwa) mwaka 1841 kwa Jahazi akitokea Zanzibar akiwa ni survivor wa ajali ya baharini iliyouwa wazazi wake yeye akiwa mtoto wa kubebwa

Baadae walezi wake wakahamia Dar na ndipo alipokulia hadi akaoa na kumzaa Abdurasul ambae ni Baba yao kina MarehemuTurabali, Mustafa, Shuli na wengine nimewasahau

Mzee Turab akamwambia yule jamaa wa Kingoni kwamba kipindi hicho bado Wangoni hawajaja kabisa Tanganyika wapo hukoo South Afrika wakipewa msukosuko na Mfalme Shaka Zulu hadi kwenye miaka ya 1880s. Akamalizia kwa kumuuliza kati ya yeye(Turab Abdurasul) na hiyo Mngoni nani kati yao ni Mtanzania zaidi!?
 
Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,024
2,000
Hakika lilikuwa jibu mujarab kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,531
2,000
Kuna jamaa nilikutana nae Botswana na aliwahi fika Tanzania enzi hizo na kuona vimbwanga vya mechi ya Simba na Yanga, bado anafikiri sana kuhusu raha ya unazi wa mpira wa Tanzania. Na bado anashangaa ni vipi mahaba yoote katika hiyo Derby yashindwe kutafsiri mafanikio ya soka la Tanzania kimataifa? Anashangaa sana kuona Tanzania ipo chini sana kisoka wakati hamasa ya soka ilikuwa juu sana kulinganisha na mataifa mengine yaliyotuzunguka.
Sio ajabu ukienda Kampala au Nairobi na hata Bujumbura ukakuta watu wanajinasibu wao ni Simba au Yanga. Hii ni kuonyesha kama tungetumia vizuri hiyo fursa leo hii hapa Afrika Mashariki na Kati watu wangekuwa wanashabikia Simba na Yanga badala ya Man U au Barcelona. Hakika hatukuweza kuitumia fursa hii adhimu!
 
Milanzi2018

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
389
500
Umenikumbusha jambo kubwa sana mzee wangu. Hii Portelo ndio soda ya kwanza kutengenezwa hapa nchini na kiwanda cha Abdurasul and Sons LTD kilichokua pale opposite na jengo la telephone House nadhani ni mtaa qa Bridge ule

Siku moja mwaka 1996 mmojawapo ya mtoto wa Abdurasul akiiitwa Turabal( amefariki miaka takriban kumi iliyopita naye akiwa mtu mzima sana) alikabiliwa na mwanaharakati za Uzawa zilizoasisiwa na Mchungaji Christopher Mtikila, jamaa wa Kingoni na akamwambia wewe Gabacholi(Muhindi) rudi kwenu India

Basi Mzee Turab kama tulivyokua tunamwita alianza kumueleza yule mwanaharakati wa sera za uzawa kua yeye Babu yake akiitwa Sachupira alikuja Tanganyika(Kilwa) mwaka 1841 kwa Jahazi akitokea Zanzibar akiwa ni survivor wa ajali ya baharini iliyouwa wazazi wake yeye akiwa mtoto wa kubebwa

Baadae walezi wake wakahamia Dar na ndipo alipokulia hadi akaoa na kumzaa Abdurasul ambae ni Baba yao kina MarehemuTurabali, Mustafa, Shuli na wengine nimewasahau

Mzee Turab akamwambia yule jamaa wa Kingoni kwamba kipindi hicho bado Wangoni hawajaja kabisa Tanganyika wapo hukoo South Afrika wakipewa msukosuko na Mfalme Shaka Zulu hadi kwenye miaka ya 1880s. Akamalizia kwa kumuuliza kati ya yeye(Turab Abdurasul) na hiyo Mngoni nani kati yao ni Mtanzania zaidi!?
hii nimeipenda bure Kabisa
 
GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
1,564
2,000
Bandiko hili linanikumbusha siku yangu ya kwanza kwenda kuangalia mpira kwenye uwanja wa Ilala. Mimi niliwahi kuwa mcheza mpira, lakini sikuwahi kuwa na mapenzi na klabu kongwe za Yanga na Simba. Mzee wangu naweza kusema ni Simba damu damu na ndie aliyenishawishi tukaangalie mpira siku hiyo Simba ikicheza na Cosmopolitans.

Pamoja na kutokuwa mshabiki sana nilikubali mwaliko wa mzee wangu,tukaenda Ilala stadium na ilikuwa mwaka 1971 kama sikukosea. Uwanja ulizungushiwa ukuta na kuacha milango midogo ya kuingilia kwa pembeni kulikuwa na vidirisha vidogo vya kulipia kiingilio. Eneo lile lilijaa mchanga na minazi kila upande, na kila mnazi juu yake kulikuwa na watu waliokuja kuangalia mpira kwa kiingilio cha umahiri wa kupanda minazi na kuhakikisha huanguki kwa kushangilia. Nje kama kawaida walikuwepo Polisi wapanda farasi.

Ndani ya uwanja, viti vilijengwa kwa sementi na mbao na nafasi ilikuwa ni finyu sana kiasi cha kubanana. Nakumbuka alikuwepo kijana mmoja mwenye mwili mdogo sana aliyekuwa na uwezo wa kumiliki mpira atakavyo na kuwapagawisha mashabiki, huyu baadaye nikalazimika kumjua kwa nguvu kwani ndio Mzee Abdallah Kibadeni wa leo. Kuna mchezaji mmoja mrefu mwenye miguu iliyopindia kushoto, Huyu ndiye aliyenivutia zaidi siku hiyo kwa umahiri wake, kujiamini kasi ya ajabu na mbwembwe za hapa na pale... Huyu nilikuja kumjua kwa jina moja la....Lesso sikumbuki jina lake la kwanza .... Lakini tumetoka mbali sana Kwa hiyo tutembee kifua mbele shigo juu kwa kujiamini sana...tuko kwenye right track!!:D:D:D
 
ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
11,680
2,000
Wengi wetu tumekulia Dar es Salaam na tumeuona unazi wa Simba na Yanga ulivyokuwa.

Nakumbuka siku kama ya leo ambayo sasa tunaita Dar es Salaam Derby ukipenda Kariakoo Derby ilivyokuwa.

Nakumbuka pale mnadani Mafia na Msimbazi vile vitezo vilivyokuwa vinamwaga moshi wa ubani toka asubuhi.

Wakati ule Yanga wako Sukuma na Sunderland yaani Simba wako Congo.

Vilabu viko jirani kwa mwendo na mbio zetu za kitoto dakika kumi zilitosha kufika Yanga kuangalia kuna nini na ukarejea Sunderland kutazama hali ya hewa. Uwanja ulikuwa Ilala Stadium.

Watangazaji wa TBC wana kijibanda kidogo juu tuu ya jukwaa la watazamaji.
Dar es Salaam ilikuwa ndogo sana.

Milango ya kuingia uwanjani midogo sana inaruhusu kuingia mtu mmoja mmoja na wachanaji tiketi unawaona hapo.

Wauza soda za Portelo kutoka kiwanda cha Abdulrasul wanazunguka uwanjani na Cocacola pia walikuwa wanashusha makreti kwa makreti ya mbao nyuma ya uwanja.

Kuna vijana wakiuza soda hizo kwa kamisheni. Nakumbuka gari la soda za Cocacola la Mzee Maukwe.

Navikumbuka vyumba vya wachezaji...vyumba vidogo sana.

Minazi mingi ilikuwa imezunguka uwanja na kuna waliopanda minazi hii kuangalia mpira.
Hali imebadilika sana.

Kuna maendeleo makubwa katika soka.
Unazi pia umechukua sura tofauti kabisa.

Leo sihitaji kupiga zile mbio kwenda club au kupita mnadani kupata, "mood," ya "game."

Simu yangu janja inanitosha kabisa kusikiliza na kuona watani wanavyotupiana makombora na kwa kweli inaongeza ladha ya mchezo.

Hakika tumetoka mbali toka enzi za akina Mnuwili, Ugundo (Dr. William), Ayub Kiguru, Bin Dossi, Jumanne Kisukari...Allah awarehemu...viongozi kama Shebe, Kitwana Ibrahim...muhimu sana TFA itengeneze Ukumbi wa Historia ya Mpira na historia ya Wanazi wa Simba na Yanga.

Hii ni historia ya pekee kabisa.

Leo tuko kwenye "electronic tickets," na mpira uko kwenye TV na hii imetuletea wapenzi wa soka wa kwenye makochi majumbani, Uingereza wanawaita, "arm chair supporters," na wanajaribu kuwatoa vitini kuwaleta uwanjani.

Club zinataka kuongeza ''gate collection.''

Vilabu hivi Simba na Yanga vina historia kubwa sawasawa na mji wake wa Dar es Salaam.
Timu iliyoshinda Gossage Cup 1949 picha hii walipiga Ilala Stadium.

View attachment 1024269
Timu iliyoshinda Gossage Cup 1949 picha hii walipiga Ilala Stadium.
Youtube haipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom