Dar coach hapa tuwape pongezi jamani

Ubunifu wa hali ya juu sana. Naipongeza hii kampuni kwa jinsi wanavyo boresha mahitaji ya sisi wasafiri wa mabus.

Tanzania ya viwanda bora inawezekana.
 
Shida sio kumiliki kitu kipya alafu kizuri,shida ya sisi waafrika ni kumaintain status ya kitu unapokinunua hadi baada ya muda mchache.Shida hii inatoka kwa wafanyakazi wa makampuni mpka awapokea huduma.Naomba baada ya miezi 6 unitumie picha kama hizi za leo!
 
Body inaitwa scania tanzanite......ila katika body zote walizotengeneza dar coach ,body ambayo ni nzuri sana ni body ya majinjah special CSN,CSL na BUL
 
Scania F360 opticruise hiyo. Assembled by Dar Coach. Ni ushirikiano wa Scania Tanzania na Dar Coac, Scania wanapeleka chassis Dar coach....Scania Tz wanataka kutengeneza buses hapa hapa ili kushindana na soko la basi za kichina.
 
Kiwango mkuu kiwango aka TBS
 
Waambie Serikali wapunguze kodi za kuuza bodi zilizotengenezwa Tanzania wakashusha kodi kwa mabasi ya Kutoka nje.
 
Huu ndiyo ukweli, hao jamaa wapo muda mrefu na wamefanya kazi nyingi sana.
 
CHUMA KIMESIMAMA SI MCHEZO.. THIS IS BRILLIANT, KWELI TUNAELEKEA PAZURI. I CAN ALSO RECOMMEND
 
Kwenye body tupo vizuri mkuu, kuna gari za utalii ukiambiwa body zake zinaundwa Bongo unaweza kukataa
I HOPE TUTAFIKA SEHEMU STAHIKI TU. KUNA KAMPUNI ARUSHA KAMA SIJAKOSEA YA WAHINDI WANAFUMA BODY ZA MAGARI YA TOURS AISEE NI MUSHKELI, BHALAA SANA!!
 
Yanadumu sana ila tatizo ni bei yake. Wakiweka bei kama kina Yutong na wenzake lazima atasumbua kiasi.

Je anaweza tengeneza oda ngapi kwa mapema?
Hawezi akaweka bei sawa na youtong maana magari yake ni chuma imara tofauti na mchina,, ukiuziwa Gari ya mchina m 200 na mwenzako akanunu scania ya m 400 Mwenye scania atadunda mchina akienda sana miaka m3 scania miaka 15 ni kawaida hadi 20
 
ameen ameeen ameeeen ameeeeen
 
Mkuu uko deep,inamaanisha walivua body za tsk injini nyuma wakavalisha kwenye chasisi za Scania injini mbele?
CSN na CSL ni bodi za Volvo zamani ziliitwa TSK zilikuwa engine nyuma. Hiyo BUL ni bodi ya IRIZAR hakuna mkono wa Dar coach hapo
 
Napenda sana sauti ya SCANIA hasa linaposhika kasi.
Ikiwa kwenye mwendo hua inapiga mruzi nadhani ni turbo inakua inafanya kazi hua najiskia poa balaa.
Vizuri sana Dar Coach.
 
Mimi nikilikuta stand hilo bus,sipandi lingine na siulizi bei ya nauli maana ntajisikia raha Sana kupanda Tanzanite
Kabisa mwanangu.... Nyumbani kwanza
Niwakati jamii zetu Sisi watu weusi kuanza kujitambua na kujivunia km walivyo waarabu ,wahindi na wayahudi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…