Dar: Basi la shule la St. Florence Academy (hiace) lapata ajali maeneo ya Interchick Mbezi Beach

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Ajali hii imetokea asubuhi hii, basi hilo likionekana kutumbukia kwenye mtaro likiwa na wanafunzi kama 10 hivi. Kwa kuwaangilia watoto hawaonekani kuwa wameumia sana, zaidi ya michubuko na hofu kwa kilichotokea. Basi jingine kubwa la shue hiyolilipita eneo hilo na kuwachukua watoto hao.

IMG_0501.jpeg
IMG_0502.jpeg

IMG_0503.jpeg


Habari zaidizitakujia kadri zitakavyopatikana.
 
Limepita kuwachukua linawapeleka shule au linawapeleka hospitali, kuwapa taarifa wazazi na kuwasubiri wawasili hospitali ili warudi na watoto nyumbani?
Dereva wa basi hilo alitaka kuwapeleka shule, ila wananchi waliofika kusaidia wakasema hawawezi kwenda hivyo shule kutokana na tukio hilo, kwanza wawapeleke hospitali…. sijui nini kilifuata
 
Sijui kama wenzangu huwa mnawafuatilia hawa madereva wa gari za shule huwa wapo rough sana.

Nadhani ni kwasababu sheria inawaruhusu kutembea kama gari la zima moto au embulance, hawakai katika foleni na kuna sehemu wanaruhusiwa kupita kama dharula.

Ila bado hata huku mitaani huwa wanatembea na hizi gari bila adabu kabisa as if hawajabeba watoto kabisa.
 
Inafanya barabara kuwa sehemu hatari sana.
Kama hii mandela road kutokea kule Riverside hadi tazara kule yaani mamotaro gari ikiteleza lazima ile mueleka.

Aisee kuna wahandisi ni wapumbavu sana aisee. Sijui wakipita pale wanaonaje sasa na wanahisi wamefanya maamuzi sahihi kabisa. Mamitaro ni makubwa na mapana kiasi kwamba yakifunikwa na ile mifuniko ya zege unapata lane ya kupita gari ndogo na bajaji bila shida.
 
Kuna watu wasio kuwa na akili huko manispaa ndio wanaona mamitaro makubwa ni suluhu ya kupitisha maji taka bila kukwama.

Yaani ni ukosefu wa akili kiwango cha lami mzee.
Boss, Mitaro kuwa mikubwa ni sahihi, mitaro mikubwa kuachwa wazi sio sahihi na ni hatari.
 
Gari zote zinazotumika kubeba watoto wa shule zinapaswa kuwa na speacial inspection kutoka kwa mamlaka ili ziwe salama, nyingi kwa uzoefu wangu ni mbovumbovu.
 
Kumbe
Sijui kama wenzangu huwa mnawafuatilia hawa madereva wa gari za shule huwa wapo rough sana.

Nadhani ni kwasababu sheria inawaruhusu kutembea kama gari la zima moto au embulance, hawakai katika foleni na kuna sehemu wanaruhusiwa kupita kama dharula.

Ila bado hata huku mitaani huwa wanatembea na hizi gari bila adabu kabisa as if hawajabeba watoto kabisa.
Ndivyo Sheria inawaruhusu nilikuwa sijui Kabisa!
 
Wadau Wa Jamii, Habari naomba Nijulishe Msicho kitambua . Hiki kitabia Cha madereva wa school bus kuamka saa Tisa Usiku na kuanza Root saa kumi kumfata mwanafunz wa mbali , ndio kinafanya Dereva Kuanza Kusinzia Jua linapotoka ,unakuta dereva ananza taratibu Kusinzia taratibu chuma inahama
 
Back
Top Bottom