Dar, Arusha na Mwanza, jiji lipi zuri kuishi

Dar, Arusha na Mwanza, jiji lipi zuri kuishi

vamda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
919
Reaction score
599
Ndugu wana JF, naomba kuuliza kati ya Dar, Arusha na Mwanza jiji lipi zuri kuishi kwa mtumishi wa serikali mwenye kipato kidogo. Naomba nijuzwe kuhusu faida na hasara za kuishi kati ya hayo majiji matatu. Karibuni jamvini wana JF.
 
mwanza ndiyo the best ata nami nipo huko huko hila makazi ni dar
 
yani ulivyosema kipato kidogo tu, MWANZA ikaja akilini
 
Itakuwa Mwanza mkuu.Sato na Sangara wa kumwaga.
 
Dar wapiga mizinga wamejaa watazimaliza hela zako, nenda Mwanza ukaanze maisha vizuri, sato za kutosha huko na free of stress...
 
Dah, wacha na mie nijipange kuikimbia Dar, hii foleni inakera kupita maelezo; pamoja na adha ya kuungua nafsi nadhani pia inaongeza umaskini tu.
 
Dar-foreni,Mza-daladala ziwahi kupaki,A.town nyumba gharama bt Mza bado ina unafuu kuliko dar&A.town
 
Kipato kidogo ni shida kuishi popote pale! Ghalama za makazi zikiwa chini Mwanza inaweza ikawa nafuu! Lakini kwa bei ya samaki na vyakula Havina tofauti sana na Dar au AR tena miji Kama Dar na AR sijawahi kusikia wanakumbwa na Majanga ya Njaa lakini kwetu huku Mza hili janga la Njaa miaka ya hivi karibuni limekua la kawaida! Vyakula viko juu sana! Tena ukiwa na familia Ndio inakua balaa! Kama ni Kipato kidogo chakula kitakua cha aina moja kila siku!
 
Back
Top Bottom