Daniel Sillo, Kiongozi anayejitengeneza historia katika siasa za Tanzania

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mbunge wa Babati Vijijini, Ndugu Daniel Baran Sillo, ameendelea kuandika historia katika medani ya siasa nchini, hususan mkoani Manyara.

Safari yake ya kisiasa ilianza kwa uthubutu na ujasiri mwaka 2015, alipojitosa kwa mara ya kwanza kuwania ubunge, ingawa hakufanikiwa.

Hata hivyo, hakurudi nyuma. Mwaka 2020 alirejea tena kwa nguvu mpya na kuibuka na ushindi, hatua iliyompa nafasi ya kuwa mwakilishi wa wananchi wa Babati Vijijini.

Katika muda mfupi wa uongozi wake, Sillo amekuwa miongoni mwa wanasiasa waliopanda ngazi kwa kasi, jambo ambalo halijazoeleka kwa wengi mkoani Manyara.

Historia hiyo inamuweka sambamba na viongozi wakubwa waliotoka Manyara kama Frederick Sumaye aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Dkt. Mary Nagu, Mateo Qaresi, Balozi Philip Marmo pamoja na Paulina Gekul waliowahi kushika nafasi muhimu za kitaifa.

Mara baada ya kuingia bungeni, Sillo alichaguliwa kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Bunge, nafasi aliyochukua baada ya Mussa Zungu kuteuliwa kuwa Naibu Spika. Uongozi wake ulionekana na wabunge wengi kama wa kuaminiwa na wenye weledi.

Baadaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mwaka 2025-2030, baada ya kuendelea kuaminiwa na wananchi na kuchaguliwa tena kuwa Mbunge, jina lake limeibuka kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, hatua inayodhihirisha imani kubwa aliyonayo kwa wananchi na viongozi wenzake.

Sillo ndiye mgombea Naibu spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.
 
Wabunge wote walioshinda Kwa wizi hawawwzi kuweka historia yoyote ya maana zaidi USHIRIKI wao kipindi Cha umwagikaji wa damu

Atakayeweka historia Kwa kujiuzulu na kujutia damu zilizomwagika
 
Back
Top Bottom