Damas Ndumbaro atupwa jela ya soka miaka 7

Tokea lini uvaaji wa nguo ukahitaji ruhusa ama uhakiki wa uraia?

Hivi huyu Waziri bado yupo madarakani kweli? Amekiuka Katiba ya nchi
Kachemka, wakati timu zinajitahidi kupata mashabiki nje ya nchi zao lakini yeye analeta mambo ya ajabu, issue hapo Kila timu ihakikishe mashabiki zake wanajaza uwanja ambapo automatically hata wakija watu wamevaa jezi ya mgeni wanafunikwa.

Tunataka tuondoe uhalisia wa soka letu Kwa upande mashabiki
 
Kwahiyo mtu akivaa nguo ya njano awe na paspoti ya Afrika kusini au hata ya Rwanda?

Na wanaovaa chupi nyekundu wawe wanatembea na paspoti za Misri?

Huyu mzembe wa kufikiri. Si wataingia nazo kwenye mifuko na kizivaa uwanjani
Halafu ni msomi na mwanasheria...
Nchi ina hazina ya viongozi bogus
 
Kwahiyo mtu akivaa nguo ya njano awe na paspoti ya Afrika kusini au hata ya Rwanda?

Na wanaovaa chupi nyekundu wawe wanatembea na paspoti za Misri?

Huyu mzembe wa kufikiri. Si wataingia nazo kwenye mifuko na kizivaa uwanjani
Poor reasoning.
 
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchi TFF, imemfungia wakili Damas Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha pesa. Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na rais wa TFF, Ndugu, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam Tv.

Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa Shirikisho, Malinzi.

Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu. Ndumbaro ambaye alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia, Bodi ya Ligi amekanwa hadharani na vilabu huku vikisema kuwa havikumtuma kuzungumza yale ambayo alisema mbele ya vyombo vya habari. Klabu zimesema alizungumza kwa utashi wake mwenyewe, na si wao walimtuma.

Kilichomuhuku ni yeye kutaka kubadilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF bila kuthibitishwa na wajumbe wa Bodi ya Ligi na kukubaliana. Kupingana maamuzi ya kamati ya utendaji ni kosa la kinidhamu. Ndumbaro amehukumiwa kutokana na makosa hayo na kama angezungumza kwa niaba ya klabu basi adhabu hiyo ingekwenda kwa kwao, lakini yeye alijizungumzia tu kama vile alivyotaka iwe.

ShaffihDauda

View attachment 192911View attachment 192912View attachment 192913View attachment 192915
Ndo maana walimfungia zero brain.
 
Back
Top Bottom