Dalili za kuonesha tayari una ugonjwa wa Figo: Wanywa Pombe Kali Mnasalimiwa!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Profesa Janabi kwenye uzinduzi wa Professor Jay Foundation ametaja dalili za mtu ambaye tayari anaugonjwa wa figo.
"Ukiwa na hizi dalili sio za mwanzo tena, tayari wewe umeingia kwenye ugonjwa wa Figo

Katika kutaja dalili hizo, salamu hizo amelekeza kwa wale Wazee wa bapa, k-vant, Nyagi na wote wanaopiga vileo vikali ili kukomesha mademu na mengine kama hayo. Prof J hata kwenye interview yake alisema kwa siku alikuwa anachoma sindano za laki 8,

Dalili za ugonjwa wa Figo

1. Kuchokachoka ambako hakuelezeki.
2. Kulala siku inakuwa shida.
3. Hamu ya kula inapungua bila kujielewa.
4. Huwezi kufikiria sawa.
5. Mwili unaanza kuwasha.
6. Miguu inaanza kuvimba.
7. Ukiamka asubuhi jiangalie kwenye kioo uso wako utakuwa wa mduara na kadiri siku zitakavyokwenda inapotea.
8. Taste ya chakula inaanza kupotea
9. Kupumua hata rafiki zako wanaanza kugundua harufu yako ya kupumua inakuwa si nzuri sana.
10. Tumbo kuuma
11. Usiku kutoka mara kwa mara kwenda haja ndogo
12. Haja ndogo kuanza kuwa na povu
13. Unaanza kuona chembechembe za damu kwenye mkojo" -
P Jb
 
Duh ni hatari
a0478b9c-f6e2-4877-908e-d4822b371455.jpg
 
Pombe ipo tu, hamna mtu ataacha, imetengenezwa iwape uraibu watumiaji, ili wanunue kwa wingi na kuacha iwe ngumu...

Kuna matangazo kila mahali kuhamasisha unywaji, imeshakua utamaduni kabisa

Serikali inawapa ruzuku TBL, TBL inawapa ruzuku wasambazaji, ni sekta ya uchumi hiyo

Lazima walevi wawepo tu.
 
Pombe kali inatakiwa isindikizwe na mlo mzuri...
Tofauti na hapo ni kuchoma pafu tu
Prof alikosa chakula? Achaneni na kuitia hasara serikali.
Achaneni na pombe kali, kunywa mbege, togwa na mnazi.
Acha piwa, wanzuki, Moshi, Kaja jana kaondoka leo, hizo wanywaji ukiwaona wanakuwa na kakitambi flani mbonyeo kama mjamizot, alafu mashavu yanamwagika, alafu mtu anakuwa kama anangaa flani, ni hatari sana.
 
Ila hizi za kienyeji utanenepa kizembe sana!
 
Profesa Janabi kwenye uzinduzi wa Professor Jay Foundation ametaja dalili za mtu ambaye tayari anaugonjwa wa figo. "Ukiwa na hizi dalili sio za mwanzo tena, tayari wewe umeingia kwenye ugonjwa wa Figo

Katika kutaja dalili hizo, salamu hizo amelekeza kwa wale Wazee wa bapa, k-vant, Nyagi na wote wanaopiga vileo vikali ili kukomesha mademu na mengine kama hayo.
Prof J hata kwenye interview yake alisema kw asiku alikuwa anchoma sindano za laki 8,
1. Kuchokachoka ambako hakuelezeki.
2. Kulala siku inakuwa shida.
3. Hamu ya kula inapungua bila kujielewa.
4. Huwezi kufikiria sawa.
5. Mwili unaanza kuwasha.
6. Miguu inaanza kuvimba.
7. Ukiamka asubuhi jiangalie kwenye kioo uso wako utakuwa wa mduara na kadiri siku zitakavyokwenda inapotea.
8. Taste ya chakula inaanza kupotea
9. Kupumua hata rafiki zako wanaanza kugundua harufu yako ya kupumua inakuwa si nzuri sana.
10. Tumbo kuuma
11. Usiku kutoka mara kwa mara kwenda haja ndogo
12. Haja ndogo kuanza kuwa na povu
13. Unaanza kuona chembechembe za damu kwenye mkojo" - P Jb
Starehe isiyo na majuto kiafya, kiakili, kimwili na kiroho ni kumwabudu Mungu Muumba mbingu na nchi katika roho (imani) na kweli (vitendo).

Pombe majanga = Huharibu figo, ini, kisukari, mtikisiko kiuchumi..

Sigara majanga = Huharibu mapafu, kansa, pumzi ndogo kimazoezi.

Bangi = Maamuzi yasiyo na akili.

Uzinzi + Uasherati + Kunyaduana = Magonjwa ya zinaa, UKIMWI, UTI, tezi dume, mikosi, mtikisiko kiuchumi. Watoto wengi wa mitaani sababu ya mimba zisizotarajiwa na mivunjiko ya mahusiano/talaka za ndoa, visasi na mauaji sababu ya wivu uliopitiliza na usaliti.

"Dunia ni uwanja wa fujo, Dunia hadaa walimwengu shujaa"
 
Back
Top Bottom