Watu 300-350 wanafika hospitali kila siku kwa matatizo ya Moyo, soma jinsi Pombe, Sigara na Mafuta zinavyochangia

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
MOYO-660x400.jpg
Kutokana na changamoto ya magonjwa ya Moyo ambayo yamekuwa yakisumbua watu wengi hasa miaka ya hivi karibuni, nimezungumza na Dkt. Pedro Pallangyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ya Dar es Salaam ambaye anafafanua kitaalam na katika lugha nyepesi changamoto mbalimbali kuhudu magonjwa ya Moyo.

Swali: Ni kwa namna gani vyakula vyenye mafuta mengi vinaweza kuathiri Moyo?
Dkt. Pallangyo:
Mafuta yanapoingia kwenye mwili wa binadamu huwa yanakwenda kuganda na sehemu kubwa ambayo yanaganda zaidi ni kwenye mishipa ambayo inasambaza damu mwilini na mishipa ya kwenye Moyo.

Picha ambayo tunaiona zaidi kwenye tafiti za Moyo, ni mishipa ya Moyo kuziba, ambayo ina hatua mbalimbali.

Hatua za awali inaweza kuwa 10% hadi 20% ambapo katika hatua hiyo mtu anaweza kutosikia dalili zozote.

Kuanzia 30% hadi 40% mtu anaweza kujisikia hali ya kuchoka ambayo haielezeki, ikizidi hapo anashindwa hata kufanya shughuli zake za kawaida, ikifika 70% na kuendelea mhusika anaweza pata vichomi au maumivu kwenye Moyo.

Inapofikia 100% ndio hapo mtu anaweza kukutwa na kifo cha ghafla, hivyo ni jambo ‘serious’

Watu ambao tumewafanyia uchunguzi kwenye taasisi yetu, mmoja kati ya wawili anakutwa na changamoto ya mishipa kuziba na wengi wao wanahitaji kuzibuliwa mishipa ili kurejea katika hali zao za awali.

Bahati mbaya mtambo unaotumika kufanya vipimo vya Moyo hapa Nchini unapatikana Dar es Salaam na Dodoma, hivyo wanaotoka mbali na maeneo hayo wakipata changamoto ya mishipa kuziba kwa 100% inakuwa ngumu kuokoa maisha yao kwa kuwa hadi wafike Dar au Dodoma wanakuwa wameshapoteza maisha.

Kutokana na hali hiyo ndio maana tunasisitiza kuzuia ili watu wasikutwe na hiyo hali kwa kuwa nchi yetu bado haina miundombinu ya kutosha kwenye la matibabu ya Moyo.

Hivyo, ndivyo matumizi ya mafuta yanavyoweza kuchangia tatizo la Moyo, inaziba mishipa, inapunguza mzunguko wa damu.
Picha no. 4.jpg

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Pedro Pallangyo

Dalili za awali kwa mtu mwenye changamoto ya Moyo ni zipi?
Dkt. Pallangyo:
Mwanzoni kabisa huwa hakuna dalili maalum, zilizopo zinafanana na za magonjwa mengine, mfano kuchoka ambayo inaweza kutokana na shughuli au umri.

Pamoja na hivyo, dalili ambayo inaweza kusema kubwa ni kichomi au maumivu ya kwenye moyo, ambayo nayo yakijitokeza inamaanisha tatizo limeanza kuwa kubwa na inawezekana mishipa imeshaziba kwa zaidi ya 50%.

Ni mafuta ya aina gani ambayo yanachangia mishipa ya kuziba?
Dkt. Pallangyo:
Ni mafuta ya aina zote, kiwango cha mafuta kikizidi kwenye damu italeta hiyo shida bila kujali ni ya aina gani, lakini yanayoweza kuwa na athari zaidi ni yanayotokana na Wanyama, ndio maana inashauriwa kutumia mafuta ya mimea kama vile Alizeti japokuwa haimaanishi yenyewe ni salama zaidi, kwani yakizidi tatizo linakuwa ni lilelile.

Nini kifanyike kuhusu mafuta kwa kuwa vyakula vingi zina mafuta?
Dkt. Pallangyo:
Ni kupunguza aina ya vyakula ambavyo vinakuwa na mafuta mengi, mazingira ya sasa yanawalazimisha watu kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

Mfano unapokuwa nyumbani na unaandaa chakula mwenyewe unaweza kuacha kutumia mafuta katika vyakula ambavyo si lazima utumie mafuta.

Kwa wanaopenda kula vyakula vya kulowekwa kwenye mafuta kama chips na vinginevyo wajitahidi kupunguza idadi ya siku za wiki ambazo wanakula milo ya aina hiyo.

Ni kweli mazoezi yanachangia kupunguza mafuta mwilini?
Dkt. Pallangyo:
Ni kweli lakini changamoto ni kuwa kiwango cha mazoezi kinachofanywa na wengi kuondoa mafuta mwilini ni kidogo kuliko uhalisia wa mafuta wanayoingiza, ni wachache wanaoweza kutimiza kiwango cha mazoezi ya kutoa mafuta ikawa zaidi ya kiwango cha mafuta wanachoingiza.

Vipi kuhusu Pombe na Sigara?
Dkt. Pallangyo:
Vyote vina aina fulani ya sumu au kemikali ambayo inaathiri mishipa ya damu na kuta za Moyo, ambapo mwisho wake inasababisha Moyo kupata shida ya kupampu vizuri na damu kutopita vizuri kwenye mishipa.

Mfano katika Pombe kuna kitu kinaitwa Alcoholic cardiomyopathy (ACM) ambapo mtu anaishia kuwa na Moyo unaotanuka na kuwa mkubwa kisha kufeli kwa sababu ya wingi wa unywaji wa pombe, hiyo ni kutokana na damu yake kuwa na kiwango kikubwa cha pombe ambacho ni sumu.
Hivyo, mtu anapokuwa na unywaji uliopitiliza anatengeneza sumu kwenye damu yake inayotokana na pombe.

Kama ilivyo katika mafuta changamoto haiwezi kusababishwa na matumizi ya mara moja bali ni mchakato ambao unafanyika kila siku na unaweza kuchukua miaka kadhaa.

Ni pombe za aina gani na kuna kiwango cha kunywa?
Dkt. Pallangyo:
Pombe za aina zote zina madhara bila kujali ni za viwandani au za kienyeji, lakini kiwango cha kunywa kitaalam kinatakiwa kuendana na aina ya pombe husika.

Mfano bia Mwanaume anashauriwa kutozidisha kunywa chupa 3 wakati Mwanamke anashauriwa kutozidisha chupa 2. Unywaji wa wine hapo siyo suala la chupa bali glasi ambapo inashauriwa kutozidisha glasi moja.

Unywaji wa pombe kali kama vile Konyagi na nyinginezo haitakiwi kuzitisha shoti moja.

Kwa ufupi ni kuwa kila pombe ina kiwango chake cha kitaalama ambacho hautakiwi kuzidisha.

POMBE KWA MJAMZITO
Dkt. Pallangyo:
Mama mjamzito anapotumia pombe inaweza kupita katika kondo linalomuunganisha mama na mtoto, kwa kuwa pombe ina sumu, ikiingia katika kwenye mfumo wa ukuaji wa mtoto inaathiri vitu vingi mfano Ubongo, Moyo, Mapafu n.k

Hivyo Mtoto anaweza kuzaliwa na changamoto kadhaa kwa kutegemea na kiwango ambacho mjamzito alikuwa anakunywa wakati kiumbe kikiwa tumboni.

SUKARI NA CHUMVI
Dkt. Pallangyo:
Matumizi mengi ya Sukari siyo kwamba itasababisha ugonjwa wa Moyo wa moja kwa moja, bali inaweza kusababisha Kisukari, ambacho kinaambatana na magonjwa mengine yanayotokana na mishipa.

Ndio maana ni kawaida kuona mgonjwa wa Sukari anakatwa kiungo fulani kwa kuwa damu haifiki kwa wakati na hayo maeneo yanakufa ndio maana yanakatwa kama vile miguu au mikono.

Hivyo, unapokuwa na Kisukari unaweza kupata ugonjwa wa Moyo unaotokana na Kisukari unaoitwa ‘diabetes heart disease’, ambao nao unaathiri mishipa ya moyo, ambapo unaathiri mzunguko wa damu kwenye moyo.

Chumvi athari yake yenyewe ni presha, kitaalamu inaongeza resistance (kizuizi) kwenye mishipa ya damu na ni kisababishi kikubwa cha Shinikizo la Damu.

Kutokana na hali hiyo ndio maana huwa tunawaambia wagonjwa wa Shinikizo la Damu na Presha kupunguza matumizi makubwa ya chumvi.

Wagonjwa wengi wanakosea na kuacha kabisa kutumia chumvi jambo ambalo ni kosa kwa kuwa miili yetu bado inahitaji chumvi katika utendaji kazi wake, usipotumia kabisa unaweza kupata ugonjwa mwingine wa tofauti.

Takwimu za wagonjwa wa moyo kwa mwaka zipoje Nchini?
Dkt. Pallangyo:
Hakuna utafiti wa moja kwa moja kujua idadi ya wagonjwa wa moyo kwa Nchi nzima, labda ninaweza kukupa takwimu za JKCI.

Kwa kila siku tunahudumia wagonjwa 300 hadi 350 wanaokuja na kuondoka, lakini tunaolaza ni wagonjwa 8 hadi 10, hivyo ukihesabu kwa mwaka unapata idadi kubwa.
agonjwa ya Moyo yapo ya aina mbalimbali na katika ukubwa tofauti kutokana na mazingira, mfano maeneo ya Manyara, Arusha na Singida magonjwa yaliyopo huko ni tofauti na maeneo mengine.

Wagonjwa wengi wanatokea Mkoa gani?
Dkt. Pallangyo:
Kwa kuwa ofisi yetu ipo Dar es Salaam ndio sehemu ambayo tunapata wagonjwa wengi lakini haimaanishi wakazi wengi wa mkoa huo ndio wenye changamoto ya Moyo, faida yao ni kuwa taasisi ipo karibu yao.

Nje ya Dar wagonjwa wengi tunawapata kutoka Morogoro, Arusha na Kilimanjaro.

Kwa nini Wagonjwa wengi wanafika hospitalini wakiwa wamechelewa?
Dkt. Pallangyo:
Kwanza ni tamaduni ya kutokuwa na kawaida ya kufanya vipimo, mtu akisikia maumivu ya moyo ananunua Panadol huku akijisikilizia bila kufanya vipimo.

Pili ni wahudumu wa afya, wengi hawana elimu kuhusu masuala ya Moyo na hata miundombinu ya vipimo siyo vingi, baadhi ya sehemu vifaa vipo lakini matumizi bado ni changamoto kwa kuwa hakuna wataalam wenye uelewa mzuri wa magonjwa hayo.

Pia umasikini unachangia kwa kuwa kama nilivyosema sehemu yenye vifaa vya uhakika na vikubwa ni Dar na Dodoma, hivyo inapotokea changamoto ya moyo kwa mazingira hayo inakuwa ngumu kufika maeneo husika.
 
View attachment 2590868

Ninaomba kuuliza kuhusu mafuta ya alizeti .research nyingi sikuizi zinaonesha kuwa mafuta ya alizeti sio mazuri kabisa
Kwasababu ratio ya omega 6 (ambayo ni proinframattory) na omega 3(ambayo ni antiinflammatory ) ni kubwa sana, na inajulikana kamba inflammation ndo inaletea zaidi kugandiana kwa mafuta kwenye damu.
Alafu pia sidhani kama mafuta tunayokula yanaenda direct kwenye mishipa ya damu maana kuna cells zinaitwa fat cells maalumu kwa kuhifadhia mafuta ni kiwango kidogo tu kinachoenda kwenye mishipa. Mimi nilidhani mafuta mabaya ni yale yanayotokana na wanga tunaokula sana ambapo ukizidi (glucose) kwenye ini unabadilishwa kuwa mafuta na mafuta ayo ndo mabaya sana kwenye mishipa.
 
1: Ni kweli mafuta ya alizeti yana omega 6 nyingi ukilinganisha na omega 3:

Cha msingi ni kuwa bado mwili unahitaji hii esential acid na mwili hauwezi kupata ndani yake bali kutoka nje. Bado mafuta ya alizeti yana uwiano mzuri zaidi kuliko yale ya wanyama ndo maana mtaalamu kule juu anasema si kuwa kwa kuwa ni salama watu watumie tu bali kiasi kizingatiwe.

2: Mafuta toka nje huvunjwa vunjwa ili kuweza kufyonzwa na.mwili kutumia material yaliyofyozya kutengeneza tena matufa/lipids.

3: Sukari hubadilishwa kuwa mafuta pale kiwango cha utunzaji wa nguvu mwilini(ini na misuli) kama glycogen kinapozidi na hivyo mwili kutengeneza mafuta kutoka kwenye sukari kwa ajili ya utunzaji wa hizo nguvu pia. Ndo maana uchukuaji wa sukari unasisitizwa kuendana na mahitaji ya nguvu ya mwili.

NB: Zote ni materials za kutengeneza fats/lipids.
 
Kwanini hawajataja matumiz holela ya Energy drinks! Energy inaweza hata kupelekea moyo kusimama ghafla bila dalili yoyote! Na ndiyo zinanyweka saba these days!
 
Back
Top Bottom