Kwenye mwendokasi naona ndo wamefanya sheria kabisa kwamba wanawake wajawazito au waliobeba watoto wapishwe na wana siti zao maalum sasa kuna siku mimi na dada mmoja tulijichanganya tukawahi siti zao
Akaja mama kabeba mtoto wenzie wakamwambia "si uwaombe hao wadada wakupishe" akawajibu eti "kwani hawanioni hadi niwaombe ona watu wenyewe wanavyogeuka pembeni utafikiri hawanioni"
Sasa bora hata mimi yule mwenzangu alivyosikia vile ndo kabisa akainamisha kichwa kulalia pochi yake na mimi siyo kwamba nisingeweza kumpisha
Ila niseme tu ukweli siku hiyo nilikuwa najisikia vibaya hovyo yaani hata pochi yangu tu nilikuwa naiona nzito sembuse kupakata mtoto wa mtu au kusimama daah
Kuanzia siku hiyo nikasema sipandi tena mwendokasi bora nijitahidi niwe nawahi treni tena ukizingatia nilipokuwa naishi kwenda kwa treni ni moja kwa moja wakati kwa mwendokasi nazunguka
Sema tu ni vile treni kuna siku nilikuwa nachelewa naikosa na ikienda hadi ije irudi tena giza lishaingia sasa daladala ndo usiseme yaani zile unaweza ukasukumana na watu milangoni na bado ukakosa hata nafasi ya kusimama tu achilia mbali kukaa
Tena siongelei zile daladala za hiace au coaster naongelea zile eicher zenye milango miwili mbele na nyuma ila bado zinajaa hadi zinaegamia upande mmoja sasa fikiria umetoka kukanyagana na watu umechoka halafu unafika unakaa mtu anaomba umpishe akae
Inabidi tu ukubali maana ndo ubinadamu huo leo kwake kesho kwako ila aise maisha ya dar mixer lile joto kama hauna usafiri wako ni mtihani kwa kweli bora hata nilivyohamiaga mkoani