Simulizi: Mama Hadija

Detective Kipepeo

New Member
Jul 28, 2022
4
7
Sehemu ya 1.

Jakson Maiga.Koplo, kutoka kituo kikuu cha Polisi Arusha, alionekana na mawazo mengi kichwani kuhusu hatma ya maisha yake ya baadae, akiwa ndani ya gari dogo la polisi, nje ya benki ya Meridian iliyoko Clock Tower .


Koplo Maiga ni kijana mwenye miaka 27, mrefu, maji ya kunde, mwenye umbo kakamavu.mwenye malengo ya kuwa Sajenti wa polisi hapo baadae, cheo kitakachomuwezesha kufikia malengo yake ya kuoa, kuwa na watoto, na kuwa na maisha mazuri hapo baadae.Kitu ambacho hakiwezekani mpaka pale Sajenti Kimaro atakapostaafu, au kufariki.

Sajenti Kimaro, ambae ameshapita muda wake wa kustaafu wa miaka 65, pamoja na uchapakazi wake wa kiwango cha juu, ilitakiwa awe amestaafu na kumpisha Maiga kuchukua cheo chake cha Usajenti, Cheo ambacho kitampatia nafasi koplo Maiga ya kupata mshahara mkubwa utakaomuwezesha kumuoa mchumba wake anaempenda sana Hadija.

Ukiacha mawazo haya ya kupanda cheo, Koplo Maiga alikuwa na hasira za kupangwa lindo kwenye benki ya Meridian siku hii ya jumamosi jioni, muda ambao alitakiwa awe na mchumba wake Hadija, na hii ilisababishwa na taarifa ya dharura kutoka kwa Sajenti Kimaro,baada ya meneja wa benki ya Meridian ndugu Joseph Kigai, kupata ugonjwa wa mshtuko wa moyo ghafla.

"Samahani kijana wangu" Sajenti
Kimaro alimwambia Maiga," nimepata dharura kuna mambo muhimu naenda kuyashughulikia", kaa hapa ulinde benki, huwei jua, anaweza kutokea mwehu akapata wazo baya,na pia ndani ya benki yuko Janet, anamsubiri meneja mpya kutoka makao makuu ,aje kuchukua nafasi ya meneja wa sasa, ndugu Kigai ambae anaumwa, najua ulikuwa na miadi na mchumba wako Hadija,lakini hii ni dharura, utapata muda mwingine wa kukutana na mchumba wako, lakini sio leo" Sajenti Kimaro alimwambia koplo Maiga.

Koplo Maiga amekaa kwa muda wa masaa mannne sasa toka apate maagizo kutoka kwa Kimaro, na matumaini yake ya kuonana na mchumba wake yametoweka, Akaona gari dogo aina ya toyota corola taratibu inasimama kwenye parking za benki ya Meridian,akamuona kijana wa makamo, mrefu, mwenye umbo la kimazoezi anashuka kutoka ndani ya gari,na kuekea kwenye mlango mkuu wa kuingia benki, koplo Maiga kwa haraka akashuka nje ya gari.

"Wewe! ", Koplo Maiga akaita, " hebu subiri, benki imefungwa," koplo Maiga akafoka kwa hasira, Yule jamaa akasimama na kumwangalia Kolplo Maiga, alivyomuona Maiga anamkaribia, akatabasamu. " Jina langu ni Chriss Ruge," akajitambulisha kwa Koplo Maiga, " ni meneja mpya wa Meridian Benki",Koplo Maiga akamuangalia kwa makini Chriss, halafu akampa mkono,"Mimi ni Koplo Maiga, ninaweza kuona kitambulisho chako"?. Koplo Maiga akamuuliza, Chriss akaingiza mkono kwenye mfuko wake wa nyuma wa suruali, akchomoa wallet yake,na kutoa kitambulisho chake cha benki na kumpa Koplo Maiga,"hiki kitatosha"? Koplo Maiga akapokea kitambulisho cha Chriss, akakiangalia kwa makini, aliporidhika akamrudishia Chriss kitambulisho chake."Sajenti Kimaro hakutaka Janet abaki mwenyewe ndani ya benki,akaniagiza nimlinde, lakini kwa sababu umekuja,mimi naondoka", Koplo Maiga akamwambia Chriss.

"Vipi hali ya Joseph Kigai, ana unafuu"? Chriss akamuuliza koplo Maiga, "Mhh, bado hali yake sio nzuri, daktari kasema labda tumwangalie mpaka kesho, labda mambo yanaweza kubadilika",Koplo Maiga akasema."Ngoja nimuangalie Janet huku ndani ya benki,atakuwa amechoka,anataka kwenda nyumbani", Chriss akamuambia Koplo Maiga. ""Mhh kweli , maana alimkuta meneja yuko chini amedondoka, Janet atakuwa na mshtuko bado", koplo Maiga akamuambia Chrriss. Chriss na koplo Maiga wakaanza kutembea kuelekea kwenye lango la benki, mbele yao katikati ya mlango wa benki, wakamuona binti mrembo mwenye umri kati ya miaka ishirini na tano mpaka ishirini na saba amesimama."Huyu ni bwana Chriss",koplo Maiga akamuambia Janet.Janet akamuangalia Chriss kwa mshtuko, mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio" What a man!" Janet akatahayari utanashati wa Chriss. "Samahani kwa kukuchelewesha Janet", Chriss akasema."Hakuna shida"Janet akamuambia Chriss, "unaingia ndani"? Janet akauliza, Koplo Maiga akasema, Acha mimi niondoke, sina kitu kingine cha kufanya hapa", Chriss akaagana na koplo Maiga, akaanza kuongozana na Jenet kuingia ndani ya benki.Koplo Maiga akaenda kwenye gari lake na kuondoka.

Chriss akaingia ndani ya benki na kufunga mlango,akaanza kuangaza macho ndani ya benki, mbele kuna kaunta yenye nondo za chuma, nyuma ya nondo kuna dirisha la vioo, kushoto kwake kuna mlango, na mlango mwingine uko nyuma ya kaunta, pembeni kuna viti vya sofa ,na meza iliyojaa magazeti mbele ya viti. Janet akamuangalia usoni, "Pole sana kuhusu Kigai",najua bado una mshtuko, ni vizuri ukaenda nyumbani kupumzika", Chriss akamuambia Janet, "Unaweza kunipa funguo za benki, halafu uondoke"? "Hakuna kitu tunaweza kufanya sasa,mpaka Jumatatu",Chriss akamuambia Janet.

"Hutaki kukagua mahesabu"? Janet akamuuliza Chriss."Sio sasa hivi, nitakagua mahesabu Jumatatu", Chriss akasema,Chriss akafungua mlango wa ofisi ya meneja, Ofisi nzuri yenye kapeti chini, viti viwili vya kifahari vinavyoangalia meza, pamoja na kabati zuri nyuma ya kiti."Ingia na ukae kwenye kiti", Chriss akamuambia Janet, "Sigara"?, Chriss akamuuliza Janet, "Hapana, sivuti sigara", Janet akamuambia Chriss na kukaa kwenye kiti."Funguo ziko wapi"? Chriss akauliza, "Ziko kwenye droo ya juu ya kabati" Janet akajibu. Chriss akafungua droo na kuchukua funguo. "Wewe unakaa na funguo gani"?. Chriss akamuuliza Janet."Ninakaa na funguo za mlango wa mbele, pamoja na funguo za kwenye kabati la kuhifadhia fedha", Janet akamjibu Chriss,. Chriss akatabasamu na kusema,"Kwa hiyo siwezi kutoa fedha kwenye kwenye kabati, mpaka nipate ruhusa yako"?. Janet akatingisha kichwa kukubali. "Janet, mimi ndio nimefika leo kutoka Dar es Salaam ,,..sina sehemu ya kukaa, wapi ninaweza kupata nyumba nzuri ya kupanga"? Chriss akamuuliza Janet,... Mmh kwa sasa hivi ni ngumu, lakini pale ninapoishi kuna vyumba self container ni vizuri havina mpangaji.", Janet akamuambia Chriss. Chriss hakutaka kuishi karibu na Janet, lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali mapendekezo ya Janet, "Sawa, nitaenda kuviangalia,"Chriss akamuambia Janet. "Janet, kwa nini haukai na wazazi wako"? Chris akauliza, "Sina, walikufa kwenye ajali ya gari miaka mitano iliyopita", Janet akajibu. "Pole sana Janet", Chriss akamuambia. "Asante", Janet akajibu. Chriss akanyanyuka kwenye kiti na kuanza kuondoka ofisini, akamuambia Janet afunge ofisi mpaka Jumatatu watakapofungua benki, Janet akafunga mlango wa benki na kuondoka.

Chriss akawasha gari na kuelekea nyumbani kwa bwana Kigai, anaeishi kwenye nyumba ya benki, alipofika ,akaanza kuikagua nyumba, Nyumba ya kizamani ya matofali ya kuchoma, bati limechakaa na kuanza kutoa kutu, rangi ya kuta imepauka, Chriss akawaza, ", Kwa hiyo bwana Kigai asipopata nafuu mapema, mimi ndio nitakujaa kuishi kwenye hili pango"?.Chriss akawaza.Chriss akarudi kwenye gari lake, akaondoka na kuelekea Sakina Bar, alipofika, akashuka, akaingia ndani, akaenda kaunta kwenye viti virefu,akakaa na kuagiza bia.."Kwa hiyo bwana Kigai asipopata nafuu, nitakaa hapa kwenye huu mji wa wamasai kwa miezi mingi"!.. Tena inawezekana nikakaa moja kwa moja kama mambo hayatakuwa mazuri kwa bwana Kigai.."Inawezekana nikazeekea hapa benki, pamoja na Janet...tutatoka mvi pamoja na kustaafu hapa Benki.... lakini Janet hata akifikisha miaka hamsini, bado ataonekana mrembo..miaka kumi na tano jela Kisongo sio mingi."Chriss akawaza.

Chriss akaondoka Sakina Bar, akapanda gari lake na kuelekea Sekei.Akasimamisha gari mbele ya geti la nyumba nzuri, akashuka kwenye gari na kugonga geti. Baada ya muda kidogo, geti likafunguliwa na mwanamke mmoja wa makamo, mwenye umbo la namba nane. "Mimi ni Chriss Ruge", Chriss akasema, "Janet nimemkuta"?. " Oooh, karibu bwana Chriss, Janet alinitaarifu utakuja", yule mwanamke akajibu. "Asante", Chriss akajibu na kuingia ndani, Nyumba ina floor tiles kuanzia getini, Juu bati la Msouth, na milango yenye grill nzuri za rangi nyekundu iliyopauka. Chriss akamuangalia kwa makini yule mwanamke aliemkaribisha. Mwanamama mnene wastani, mweupe, mwenye hips nene, kiuono chembamba, matiti makubwa yaliyojaa na kuchongoka, shingo ya michirizi, kichwa chembamba kilichorembwa na pua ndefu na midomo minene, nywele nyingi zilizodondoka mpaka mabegani, " Bila shaka huyu ni mmeru", Chriss akawaza. "Mimi ni mama Hadija, ndio mama mwenye nyumba, ukiamua kuishi hapa, nitafurahi", Yule mwanamke akamuambia Chriss. "Na mimi pia nitafurahi kuishi hapa", Chriss akajibu. " Sijui nitakaa hapa muda gani, inategemea na muda meneja wetu bwana Kigai atapata nafuu, nimesikia yuko kwenye hali mbaya". "Ndio, Janet ameniambia, namuonea huruma mke wake", mama Hadija akajibu.

" "Najua umechoka, njoo nikuonyeshe vyumba, kuna vyumba viwili double vina vyoo ndani, unaweza kuchagua kimoja wapo", mama hadija akasema. Chriss akageuza shingo na kumuangalia mama Hadija usoni, mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda mbio, "Shilingi ngapi kwa mwezi"?. Chriss akauliza. "Laki moja kwa mwezi", mama Hadija akajibu. Chriss akaingia ndani ya chumba kimoja wapo, akaona kuna milango miwili, " Huu ni mlango wa kuelekea chooni"?. Chriss akauliza, na kunyoosha kidole kuelekea mlango mmojawapo, "Hapana, mlango huo hautumiki, unaelekea kwenye chumba changu, huo mwingine ndio unaelekea chooni,"Mama Hadija akajibu. "Nitachukua chumba hiki, kama unakubali", Chriss akajisema. "Hakuna shida", mama Hadija akasema. "Unaweza kuleta vitu vyako sasa." Mama Hadija akamuambia Chriss. "Nina begi moja tu dogo la nguo, vitu vingine nitanunua kesho", Chriss akajibu. "Sawa, naelekea jikoni kupika ," Mama Hadija akamuambia Chriss na kuanza kuondoka kuelekea jikoni, Chriss akamuangalia nyuma jinsi makalio yanavyotingishika, mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda mbio. "Mmh ,huyu mwanamke kweli ameumbika". Chriss akawaza. Chriss akaenda kwenye mlango unaounganisha chumba chake na cha mama Hadija, Akakunja kitasa kutaka kufungua, akakuta umefungwa, akatoka nje ya geti, na kuelekea kwenye gari yake, akawasha gari akaelekea mjini.

Nyumba aliyopanga Janet na Chriss, pia kuna wapangaji wengine wawili wazee wastaafu, bibi Maureen, pamoja na mzee Kijazi. Kesho yake, baada ya Chriss kununua vitu vya ndani na kuhamia rasmi, jioni akakaa na bibi Maureen , Janet, pamoja na mzee Kijazi kwenye maongezi ya kawaida ya wapangaji. Mzee Kijazi akamuambia Chriss, "Unajua bwana, Mama Hadija ni mpambanaji sana, hakuna mwanamke anaejua kupika mtaa huu zaidi yake, Mume wake, baba Hadija alikuwa mfanyakazi wa shirika la bima, mume wake alikuwa muhuni sana, alikuwa na wanawake wengi, kila siku walikuwa wanagombana, walifanikiwa kupata mtoto mmoja, mume wake alipata ajalivya gari akafariki, akimuachia mama Hadija pesa kidogo, hizo pesa ndio amejenga hii nyumba". "Binti wa Mama Hadija, na yeye anaishi hapa",? Chriss akamuuliza Mzee Kijazi, Mzee Kijazi akamjibu Chriss," Ndio, anaishi hapa, yeye pamoja na koplo Maiga ni wachumba, Hadija anafanya kazi Mount Meru Hotel, mara nyingi anaingia zamu ya usiku, ni ngumu sana kuonana nae, anarudi nyumbani saa tisa usiku, akienda kulala muda huo, kuamka ni baada ya saa tano asubuhi", Mzee Kijazi akamuambia Chriss. Baada ya muda Chriss akajisikia uchovu, akawaaga wapangaji wenzake,akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake, akajitupa kitandani, na kuanza kuwaza. "Inaonekana huu mwaka nitaupoteza hivi hivi bila kufanya chochote", Chriss aliwaza, Sasa hivi nina miaka thelathini na nane, nina akiba benki isiyofika hata milioni, nina madeni, nisipofanya kitu sasa hivi, sitaweza tena kufanya kitu chochote milele, najua mimi sio mfanyakazi hodari wa benki, kutokuwa mfanyakazi mzuri wa benki, hakunifanyi nishindwe kufanya kitu kingine.. Lazima nitafute pesa, tena pesa nyingi za kuniwezesha kuishi maisha ya kifahari kufanya biashara kubwa za maana. Hapa Arusha kuna pesa ya maana kweli nitapata"? Chriss aliwaza. Wakati anawaza hayo, mara akasikia sauti ya mama Hadija anaingia chumbani kwake.Akaamka kutoka kitandani, akaenda kwenye mlango unaounganisha chumba chake na na cha mama hadija, akainama na kuchungulia chumbani kwa mama Hadija, kupitia kwenye tundu la kwenye kitasa cha mlango,. .... akaona kitanda kikubbwa tano kwa sita, chupi, sidiria ziko juu ya kitanda, mama Hadija akavua nguo, akachukua taulo na kulizungurusha kwenye mabega, akaelekea bafuni kuoga, Chriss mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi, akahema kwa nguvu, akarudi kitandani, "Huu sio muda muafaka", Chriss akaongea mwenyewe taratibu na kupitiwa na usingizi.

Itaendelea..................................

kwa mawasiliano zaidi.
0678 85 47 50.
 
mkuu itafika mwisho? utaratibu wa kuituma hapa upoje? maana watunzi mahiri mnatupa vidonda vya tumbo fanani wenu kwa arosto
 
Sehemu ya 2:

Wiki iliyofuata ilikuwa ni kufuata ratiba ya kama kazi ilivyopangwa. Kila siku asubuhi saa moja ni muda wa kunywa chai yeye, Janet, Mzee Kijazi na bibi Maureen, Saa tatu asubuhi, saa tatu asubuhi ,anaondoka na gari pamoja na Janet kuelekea ofisini, hakukuwa na namna yoyote ya kuweza kumuacha Janet apande dala dala, wakati ana gari na wanafanya kazi ofisi moja. Kazi ya benki ni ile ile kila siku kupambana na matatizo ya kimahesabu, shoti za pesa, kukimbizana na wakopaji walioshindwa kurejesha mikopo, huku akiwaza madeni yake anayodaiwa, na tatizo la kuishiwa na pesa kila siku. Kwa muda wa siku nne aliofanya kazi na Janet, kuna kitu kikubwa alichokigundua kuhusu Janet, ni binti mchapakazi sana,sio mvivu, yuko makini na kazi, hilo jambo lilimpa faraja sana Chriss, na Chriss alishaweka ahadi ya kutokuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wanaefanya kazi sehemu moja.

Kwa muda wote wa siku nne, hakuweza kuonana na mama Hadija, kila siku anapokuwa chumbani kwake usiku, akimsikia mama Hadija ameingia chumbani kwake, lazima aende kwenye tundu la kitasa cha mlango na kuchungulia, anaaatamani kuvunja mlango lakini anasita,"Iko siku,"anaishia kujisemea taratibu.

Jumatano jioni, wakati Chriss yuko ofisini kwake anafunga mahesabu, Janet akaingia ofisini kwa Chriss, na kumuambia Chriss, "Vipi kuhusu kesho"?. "Kuna kitu gani kikubwa"? Chriss akamuuliza Janet. Janet akajibu," Ni pesa ya mshahara wa wafanyakazi inakuja". "Mshahara gani"?, Chriss akauliza. "Ni pesa ya mshahara wa wafanyakazi wa viwanda vinne, inakuja na gari ya jeshi saa kumi na moja jioni, Sajenti Kimaro na koplo Maiga watakuwepo hapa, kuhakikisha pesa inawekwa ndani ya kabati la kuhifadhia fedha." Janet akamuambia Chriss."Na siku inayofuata, wahasibu kutoka viwanda hivyo vinne, wanaakuja saa tatu asubuhi kuichukua", Janet akamuambia Chriss. " Ni kiasi gani cha pesa kinakuja", Chriss aakamuuliza Janet. Janet akajibu, " Milioni mia tisa". Chriss kusikia jibu la Janet,mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio, macho yakamtoka kodo,"Kiasi gani umesema"? Chriss akauliza tena. "Milioni mia tisa", Janet akajibu.
" Ni pesa nyingi, kwa nini wanazileta hapa benki"?. Chriss akamuuliza Janet. "Hizi pesa zinatoka benki kuu Dar es Salaam, zinakuja na ndege mpaka KIA, kwa sababu zinachelewa kufika, ndio maana zinalala hapa benki kwa ajili ya usalama, kesho yake asubuhi zinakuja kuchukuliwa na wahasibu wa kampuni husika," Janet akamuambia Chriss. " Milioni mia tisa"? Kwa kiasi hiki ninaweza kujilipua na kuzichukua, Chriss akawaza. " Ni kwa muda gani hizi pesa zimekuwa zinakuja hapa"? Chriss akamuuliza Janet. " Ni kwa muda wa miaka mitano sasa", Janet akajibu." Sasa sisi tunahusika vipi na hizo pesa"? Kuna uhakika wa usalama kwa asilimia mia moja",? Chriss akamuuliza Janet. " Majambazi wanaweza kuja hapa na kuziiba, Sidhani kama ulinzi wetu hapa ni imara sana", Chriss akamuambia Janet. "Ulinzi ni imara sana", Janet akamuambia Chriss, akaendelea, "wewe una funguo moja ya kwenye kabati la kuhifadhia pesa, nyingine ninayo mimi, na vile vile kuna kifaa maalum cha ulinzi, hakuna mtu anaweza kufungua kabati la fedha bila kujulikana", Janet akamuambia Chriss. " Hicho kifaa cha ulinzi ni cha namna gani", Chriss akamuuliza Janet. " Ni kifaa cha kieletroniki, ukikiwasha huwezi kwenda kugusa mlango wa kabati la kuhifadhia fedha, na kama ukigusa, kinapiga kengele moja kwa moja mpaka kituo cha polisi." Janet akamuambia Chriss."Mhh, hapo sawa, lakini sisi hizo pesa hazituhusu, tunawasaidia tu kuwahifadhia pesa zao", Chriss akasema. " Nadhani leo nitachelewa kurudi nyumbani , nina kazi nyingi za kufanya, wewe umemaliza kazi zako"? Chriss akamuuliza Janet. " Ndio, nimemaliza", Janet akamjibu Chriss. " Kama umemaliza kazi zako unaweza kwenda nyumbani, muambie mama Hadija muda wa chakula cha jioni nitakuwa nimesharudi nyumbani", Chriss akasema. "Sawa", Janet akajibu na kuanza kuondoka,Chriss akamsindikiza Janet mpaka kwenye mlango mkuu wa benki, wakaagana, Janet akaanza kutembea kwa madaha kuelekea kituo cha dala dala huku Chriss akimsindikiza kwa macho, Chriss akarudi ndani ya benki, na kufunga mlango. Chriss akachungulia dirisha la benki, akaona kituo kidogo cha polisi pembeni ya barabara, akaangalia ndani ya kituo cha polisi, akaaamuona Sajenti Kimaro amekaa nyuma ya meza ya kituo, akafunga dirisha na kuelekea kwenye chumba chenye kabati la kuhifadhia fedha, akaingia ndani na kuanza kulikagua kwa makini kabati la chuma la kuhifadhia fedha, akaona kufuli mbili kubwa, juu na chini ya kabat, lakini hakukiona kifaa cha kielektroniki cha ulinzi, akarudi ofisini kwake na kuanza kuwaza. "Milioni mia tisa"?, Hii ndio nafasi niliyokuwa naisubiri kwa miaka mingi, ndio nafasi yangu pekee ya kuagana na umasikini, kwa kiasi hiki, niko tayari kujilipua, liwalo na liwe, lakini niko hapa kwa muda usiopungua miezi sita, nisifanye mambo kwa pupa, nina muda mrefu wa kujiandaa na kuiba hizi pesa bila kujulikana, lazima nitafute mbinu za kufanikisha kuchukua pesa hizi bila kujulikana," Chriss aliwaza.Chriss akafunga chumba cha kuhifadhia fedha na kurudi ofisini kwake kuendelea na kazi, alipomaliza akafunga benki, akaelekea kwenye gari lake, kisha akawasha gari, na kuanza safari ya kuelekea nyumbani.

Chriss alipofika nje ya geti la nyumbani akapiga honi afunguliwe geti, baada ya muda mfupi mama Hadija akafungua geti, Chriss kumuona mama Hadija mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda mbio, damu inachemka, mama Hadija alivaa sketi fupi iliyoishia juu yu magoti, na kuacha miguu yake mizuri ikionekana vizuri, juu amevaa blauzi iliyomkaa vyema na kuonyesha umbo lake la namba nane, Chriss alivyoingiza gari ndani akashuka kwenye gari. "Karibu ndani Chriss , mimi niko jikoni napika", mama Hadija akamuambia Chriss. "Asante sana mama Hadija, nitakuja jikoni kukusaidia kupika , hata mimi ni mpishi mzuri", Chriss akasema, Mama Hadija akamuangalia Chriss kwa mshangao, kisha akasema, "sawa,ninakusubiri,nione mapishi yako", Chriss akamuangalia usoni mama Hadija,na kutabasamu, kisha akaingia chumbani kwake.

Baada ya muda mfupi, Chriss alitoka chumbani kwake, na kuelekea jikoni, kufika jikoni akamuona mama Hadija ameinama anamenya ndizi huku mapaja yake manono yenye michirizi michache yanaonekana vizuri, "Nimekuja mama Hadija", Chriss akasema, Mama Hadija akasimama ghafla na kumuangalia Chriss kwa mshangao, "kumbe ulikuwa hutanii"? mama Hadija akasema. Chriss hakujibu, akachukua kisu na kuanza kumsaidia mama Hadija kumenya ndizi, "Ni nani amekufundisha kupika"? Mama hadija akamuuliza Chriss. "Mama yangu mzazi, mama aliniambia siku nikioa mwanamke asiyejua kupika, ninaweza kupika mwenyewe", Chriss akamjibu mama Hadija huku anacheka.Mama hadija na yeye akacheka. "Lakini kwa bahati mbaya kujua kwangu kupika hakukuweza kuiokoa ndoa yangu, nikaachana na mke wangu", Chriss akamuambia mama Hadija. "Mmh, pole, mimi mume wangu alipata ajali akafa",mama Hadija akamuambia Chriss.

Mama Hadija akasimama,akaenda kabatini kuchukua nyanya, alivyogeuka nyuma akamuona Chriss yuko nyuma yake anamuangalia, Chriss akamvuta mama Hadija karibu , na kumbusu mdomoni,mama Hadija akazungusha mikono yake kichwani kwa Chriss na kumbusu Chriss kwa mahaba huku amefumba macho, wakaendelea kubusiana kama dakika moja hivi, kisha mama Hadija akamsukuma Chriss nyuma ghafla, " Sidhani kama hii ndio njia sahihi ya kupika chakula", mama Hadija akamuambia Chriss. Chriss hakujibu, akachukua ndizi akaziweka kwenye sufuria, wakaendelea kupika, huku wakitaniana na kucheka. Mama Hadija akamuangalia usoni Chriss kwa sekunde chache, kisha akasema. " Pesa!" "Sikuwa na pesa za kutosha,ndio maana nikajenga nyumba ndogo, kuanzia niko mdogo natafuta pesa, na mpaka sasa hivi zaidi ya miaka ishirini imepita, bado natafuta,na sijazipata," Chriss akamuangalia mama Hadija ,na kisha akamjibu," Nadhani tunafanana, hata mimi nataka pesa, na bado sijazipata". Chriss akaendelea kwa kusema," Unajua mama Hadija, kuna watu wameachiwa pesa nyingi sana za urithi, na hawajui kitu cha kuzifanyia, na kuna wengine wana pesa nyingi sana wamezitafuta, lakini hawajui kitu cha kuzifanyia, na kuna mimi na wewe, ambao tunataka sana kuwa na pesa, lakini hatuna na hatujui jinsi ya kuzipata, Unaona jinsi ugumu ulipo"? Mama Hadija akumuangalia usoni Chriss na kuongea huku amemkazia macho", Na kuna watu wana nafasi ya kupata pesa nyingi sana, lakini wanaogopa kuzichukua, na kuna watu kama mimi mama Hadija, hatuna nafasi ya kupata pesa nyingi, na kama tungepata hiyo nafasi, tungechukua bila kujali madhara yoyote yatakayotokea, mradi tu kiasi cha pesa kiwe kikubwa cha kueleweka".

"Madhara? aina gani ya madhara unayozungumzia"? Chriss akamuuliza mama Hadija. Mama Hadija akasema, " aina ya madhara yoyote yale yatakayotoke,sitajali, kwa mfano mimi ningekuwa ni meneja wa benki kama wewe, lazima ningeshawishika kuiba kiasi kikubwa cha pesa". Chriss damu zikamsisimuka, akamuangalia mama Hadija , kisha akamuambia,"Kama umeajiriwa na benki, ni rahisi sana kuchukua pesa , tatizo lazima utajulikana na kukamatwa, sasa kuna faida gani kuchukua pesa na kukamatwa na kuishia jela bila kuzitumia"? Mama Hadija akamuangalia Chriss na kusema, "Lakini ukiwa mjanja, na kupanga mipango yako sawa sawa, unaweza kuchukua pesa bila kujulikana". Mama Hadija alivyoona ndizi zimeiva, akazitoa jikoni na kuanza kupakua chakula, kisha Chriss akasema",Ulitakiwa uwe na friji la kuhifadhia vinywaji na chakula kisiharibike". Mama Hadija akamjibu Chriss,"Friji"? sio friji tu, nahitaji vitu vingi, tatizo sina pesa." kisha mama Hadija akasema taratibu, " Milioni mia tisa za mshahara wa wafanyakazi"! Ni kiasi kikubwa sana cha pesa"! Chriss akageuka na kumuangalia mama Hadija, kisha akasema," umejuaje kuna milioni mia tisa za mishahara ya wafanyakazi"? Mama Hadija akatabasamu, kisha akamuambia Chriss, " hakuna mtu hapa Arusha asiejua kuna milioni mia tisa za mishahara ya wafanyakazi zinakuja kila tarehe 25 ya mwisho wa mwezi jioni, zinahifadhiwa benki ya Meridian, kesho yake asubuhi wahasibu wa makampuni manne wanakuja kuzichukua". Mama Hadija akachukua chakula, na kisha kuelekea sebuleni, Chriss akamuangalia kwa nyuma mama Hadija jinsi umbile lake linavyotikisika nyuma, akasita ,kisha akaanza kutembea kuelekea sebuleni, alivyofika sebuleni akamkuta mama Hadija ameshaanza kula, Chriss akapakua chakula, wakaendelea kula bila kuongea chochote, walipomaliza mama Hadija akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake, "Usiku mwema Chriss" mama Hadija akamuambia Chriss, Kisha akafungua mlango wa chumbani kwake,na kuingia ndani.

Chriss alivyomaliza kula, akakaa kwa muda sebuleni kuangalia T.V. akaona hamna kipindi anachokipenda, akazima T.V kisha akaelekea chumbani kwake,Alivyofika chumbani kwake akajitupa kitandani kupumzika kidogo, kisha akanyanyuka na kuelekea kwenye mlango unaoelekea chumbani kwa mama Hadija, "Kama Mama Hadija aliniruhusu nimbusu, basi inawezekana amefungua mlango huu wa kuelekea chumbani kwake ili tulale wote leo", Chriss aliwaza, Alivyofika kwenye mlango ,akakiangalia kitasa, kisha akakikunjua ili kuingia ndani, akakuta mlango umefungwa. " Mmh, kumbe mama Hadija sio mrahisi kama nilivyofikiria", Chriss akawaza, Akarudi kitandani kwake na kuanza kuyatafakari maneno ya mama Hadija "Kama ningekuwa mimi ni meneja wa benki, ningeiba kiasi kikubwa cha pesa" Chriss akayatafakari maneno haya ya mama Hadija. "Je,alikuwa anatania"? au alikuwa serious?" Chriss aliwaza. " Hivi,ninaweza kumuamini mama Hadija?". "je, anaweza kunisaidia?".. Chriss akaamka kitandani kwake, akaenda kwenye swichi iliyoko ukutani, akazima taa, na kuelekea kulala.

Kesho yake asubuhi,baada ya kufika ofisini, Chriss akaenda kumuona Janet, muda huo Janet alikuwa juu ya kiti kwenye kaunta ya benki anahesabu pesa, Chriss alivyofika kwa Janet akamuambia" Janet, naomba twende kwenye chumba cha kuhifadhia pesa, unionyeshe jinsi kinavyofanya kazi, sitapenda kuonekana sijui chochote pale pesa zitakapokuja leo jioni". Janet akakubali,akanyanyuka kwenye kiti, wakaelekea kwenye chumba cha kuhifadhia fedha. Walipofika kwenye chumba cha kuhifadhia pesa, Janet akamuuliza Chriss"Unazo funguo zako"? "Ndio ,ninazo" Chriss akajibu. Ndani ya chumba cha kuhifadhia fedha, kuna makabati mawili, moja lijaa mafaili ya wateja wa benki, lingine ndilo linahifadhia pesa, " Hili kabati ni la kizamani, halina usalama wa kutosha" Chriss akamuambia Janet, huku akimuonyesha kabati lenye mafaili ya wateja, " Huko hakuna kitu cha maana zaidi ya mafaili yenye taarifa za wateja" Janet alijibu.Walipofika kwenye kabati la kuhifadhia fedha, Chriss akamuambia Janet, " Hebu nielekeze jinsi kifaa cha ulinzi cha kielektroniki kinavyofanya kazi". Janet akanyoosha kidole kuekea juu ya kabati la kuhifadhia fedha, karibu na dari, ambako kuna kidirisha kidogo kilichokaa kama kidirisha cha kuingizia hewa, kikiwa kimewekewa chuma mbele yake, "Ndani ya hicho kidirisha, ndio kuna kifaa cha kielektroniki", Janet akamuambia Chriss.

Chriss akakiangalia kile kidirisha chenye kifaa cha kielektroniki, akaona ni ngumu sana kukifikia kama kikianzaa kupiga kengele, maana kiko ndani ya grili za chuma imara zilizoungwa kwa sementi. " Utawezaje kuzuia nyaya zinazoelekea kwenye hiki kifaa zisikatwe? Mimi naona hiki kifaa hakina ulinzi wa kutosha", Chriss akamuambia Janet. " Nyaya zinazoelekea kwenye kifaa zimechimbiwa ndani ya ukuta na chini ardhini na kuezekwa kwa sementi mpaka kwenye jenereta, ni ngumu kuzifikia," Janet akasema, kisha Janet akaenda kwenye kabati la kuhifadhia pesa, kisha akafungua kufuli moja, " Fungua hilo kufuli lingine tafadhali" Janet akamumbia Chriss. Chriss akatoa funguo zake mfukoni, akafungua kufuli, akaangalia ndani ya sanduku la kuhifadhia fedha, ni sanduku kubwa usawa wa mpaka kiunoni lenye chuma imara pande zote, " Nyaya za kifaa cha kielektroniki zimeunganishwa kutoka chini ya ardhi mpaka ndani ya kabati, na nyingine ziko ndani ya ukuta mpaka kwenye kifaa" ." Kifaa hiki cha eletroniki kinafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, mtu yoyote akitaka kukata nyaya zake, kinapiga kengele ya tahadhari" Janet akamuambia Chriss. "Sasa mbona tumefungua kabati lakini hakuna kengele yoyote ya tahadhari"? Chriss akauliza.Janet akamuangalia Chriss kidogo, akasita, kisha akasema " Ngoja nikuambie ukweli, na kwa vile wewe ni meneja wa benki hakuna shida yoyote, ingawa nilikatazwa nisimuambie mtu yoyote siri hii, iko hivi, iki kifaa kinafanya kazi pale tu, taa za ndani ya benki zinapozimwa, lakini taa zinapokuwa zimewashwa ,hakifanyi kazi." Chriss akabaki kushangaa, kisha akasema, " hiyo inaleta maana kweli?". Janet akamuangalia Chriss, kisha akasema, " Hakuna shida, hata watu wa bima wamekubali, kwa sababu taa zinapokuwa zimewashwa, polisi walioko kwenye kituo hapa jirani wanaona mpaka ndani, hivyo usalama unakuwepo"! "Sawa, kama mpaka watu wa bima wamekubali, basi hakuna shida". Chriss akasema. Wakafunga kabati la kuhifadhia fedha, wakarudi ofisini na kuendelea na kazi.

Ilipofika mida ya jioni, Chriss akaona gari ya polisi inaingia kwenye parking ya benki. "Bila shaka atakuwa Sajenti Kimaro huyo anakuja", Janet akasema huku anaelekea kwenye mlango wa benki ,Chriss akamfuata nyuma yake. Ingawa Chriss alikuwa na siku kadhaa Arusha, hakuwahi kumuona Sajenti Kimaro, Sajenti Kimaro ni mrefu, ana umbo kubwa, bado anaonekana mwenye nguvu tofauti na umri wake wa miaka 68. Sajenti Kimaro akashuka kwenye gari la polisi akiwa ameongozana na koplo Maiga. " Haonekani kama ni hatari sana ,kwanza ni mzee", Chriss aliwaza wakati anamfanyia tathmini Sajenti Kimaro, huyu mwingine ni kijana mdogo,.. Hata nikiamua kuchukua pesa kwa nguvu kutoka hapa benki, hawa polisi hawataweza kunizuia", Chriss aliwaza. Janet akamtambulisha Chriss kwa Sajenti Kimaro, huku koplo Maiga akishuhudia. "Gari yenye fedha inakuja, Chriss", Sajennti Kimaro akasema, huku akimwangalia Chriss kwa wasi wasi. " Una taarifa zozote kuhusu hali ya bwana Kigai"? Sajenti Kimaro akamuuliza Chriss, "bado hali yake sio nzuri", karibu ndani Sajenti", Chriss akamwambiia Sajenti Kimaro. "Hapana, nitasubiri hapa nje ", kila kitu kiko sawasawa"? Sajenti Kimaro alimuuliza Janet," Kila kitu kiko sawa Sajenti, hakuna shida", Janet akajibu. Wakati wanaendelea kuongea,mara barabarani, wakaona gari ya jeshi iliyobeba pesa inakuja, inaongozwa na piki piki mbili za polisi. Wote wakakaa kwa tahadhari, huku wakilitazama gari kwa makini, Gari ilipofika kwenye parking za benki ikasimama, wale polisi waliokuwa kwenye piki piki, wakateremka wakiwa na silaha mkononi tayari kukabiliana na hatari yoyote, kwenye gari wakashuka tena walinzi wawili wenye silaha i. Kila kitu kinachoendelea, Chriss alikuwa, anafuatilia kwa umakini. Wale walinzi waliotoka kwenye gari, wakaenda nyuma ya lile gari la jeshi, wakafungua mlango wa nyuma, wakashusha mabegi makubwa mawili,walivyomaliza kwa haraka bila kupoteza muda wakayabeba yale mabegi na kuelekea ndani ya benki kwa mwendo wa haraka, muda wote huo Chhriss alikuwa pembeni anatazama kila hatua kwa umakini,. Wakampita Chriss moja kwa moja mpaka ndani ya benki, na kuelekea kwenye chumba cha kuhifadhia pesa. Sajenti Kimaro akafunga mlango wa benki. Janet na Chriss wakaelekea kwenye chumba cha kuhifadhia pesa, walipofika, wakakuta tayari wale walinzi wawili wameshafika na kuweka mabegi ya pesa chini, Janet akatoa funguo na kufungua kufuli moja la kabati, na Chris nae akafungua kufuli lingine, wakafungua kabati la fedha, na kuyaweka yale mabegi mawili ndani huku Sajenti Kimaro akishuhudia, walivyomaliza,wakafunga na kufuli lile kabati la fedha na kuondoka pamoja na wale walinzi wawili.

" Yah tumemaliza, hapa hakuna mtu tena atakayeweza kupora hizzi pesa, ziko sehemu salama", Sajenti Kimaro akasema,huku akitingisha kichwa kukubali jinsi operation nzima ilivyofanyika. "Chriss, utalala kwa amani sasa", Sajenti Kimaro akamuambia Chriss.Lakini Sajenti Kimaro alikuwa anajidanganya, usiku mzima Chriss hakuweza kulala, alikuwa anafikiria njia ya kuweza kupora hizi pesa bila kujulikana. Na ana uhakika, kama zikiporwa watuhumiwa wakuu watakuwa wawili, yeye, pamoja na Janet, na kutokana na uaminifu waliokuwa nao polisi kwa Janet, ni wazi kuwa. mtuhumiwa mkuu atakuwa ni yeye, Chriss," Lazima nitafute njia ya kuweza kupora hizi pesa bila kujulikana", Chriss aliweka nadhiri moyoni. Kesho yake asubuh saa tatui, lile gari la jeshi la kubebea fedha likaingia kwenye maegesho ya magari benki, wakashuka wahasibu wanne kutoka kwenye kampuni nne kwa ajili ya kuchukua pesa, wakiwa wameambatana na walinzi wanne. Wale wahasibu wanne wakatambulishwa kwa Chriss na Sajenti Kimaro. Wale wahasibu, pamoja na Janet na Chriss wakaanza kuelekea ndani ya benki, walipofika moja kwa moja wakaelekea kwenye chumba cha kuhifadhia pesa, wale walinzi waliokuja nao wakabaki nje ya benki pamoja na koplo Maiga, askari polisi wawili, na polisi wengine wawili waliokuwa kwenye pikipiki. Sajenti Kimaro akasimama kwenye mlango wa kuingilia benki. Janet na Chriss wakafungua kabati la kuhifadhia pesa, wakatoa yale mabegi mawili ya fedha na kuyaweka chini, wale wahasibu wakayafungua yale mabegi na kutoa mabunda ya noti yaliyopangwa kwa kiwango cha milioni kumi kwa kila kibunda,. Baada ya kuhesabu na kuridhika, wakabeba pesa zao na kuondoka. Siku nzima Chriss alikuwa na mawazo kuhusu zile pesa, na anajua,akijaribu kuzichukua, mshukiwa mkuu atakuwa ni yeye. Na hili ndio tatizo.

Itaendelea.................................

Kwa mawasiliano:
0678 85 47 50
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom