Merciana
Senior Member
- Sep 6, 2017
- 103
- 327
Leo nilipanda kosta ya kawe nikakaa siti ya kwanza kabisa pembeni ya mlango.Njiani akapanda mmama watoto wanne na binti,sasa yule mama akambwaga mtoto mmoja miguuni kwangu asiseme kitu.
Me nikanyamaza tukatembea vituo kama vitatu mtoto akaanza kucheza cheza mamaake anamuuliza una nini mtoto hasemi....mama na binti walikua wamesimama pembeni yangu mama akamnong'oneza binti na mimi nasikia.
"Huyu dada anaroho ngumu hata kumpakata mtoto kama hamuoni itakua hajazaa... sijui anashuka wapi nikae".
Sikushindwa kumpakata yule mtoto sema mama mtoto alijifanya hajielewi alishindwa kuniomba nimpakatie mtoto wake?
Kumsaidia mtu siyo lazima ila kama unahitaji msaada kwanini usiombe?nilishuka Morocco nikamuachia nafasi.