Daktari wa Upasuaji akiri kuiba machine ya kuangalia mapigo ya Moyo Hopitali ya Rufaa Simiyu na kuiuza Mkoani Mwanza

Kuiba mali ya ofisi ni maamuzi magumu sana, alitegemea hatokamatwa kwavile ofisi ina watu wengi.

Kwanza wizi wake wa kizembe.
 
Hahaha, nilipo hawacheki na nyani, hata angeiba condom wangekula kichwa!! And why uende supermarket uibe wine?? Huoni huo ni ujinga uliopitiliza....
Si wanasheria zao kuwa mwizi akiiba adhabu yake ni hii, wananchi wao wakiiba wine adhabu ikoje?
 
Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watumishi watatu wa Idara ya afya kwa wizi wa mashine ya kuangalia Mapigo ya Moyo, Upumuaji, Wingi wa hewa ya Oksijeni katika damu kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji ambapo mashine hiyo iliibiwa ikiwa ndani ya chumba cha upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Nyaumata.

Katika taarifa iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao imeeleza kuwa uchunguzi uliofanywa katika Hospitali hiyo umebaini kuwa chumba hicho cha upasuaji hakikuvunjwa.

Amesema kuwa Septemba 20.2021, Getrude Emmanuel (45), ambaye ni katibu wa hospitali ya mkoa wa Simiyu, aligundua kuibiwa kwa mashine hiyo inayojulikana kwa jina la Cadiac Monitor Accessories yenye namba za usajili EX-7C051585 yenye thamani ya shilingi .7,820,000/= iliyokuwa kwenye chumba cha kufanyia upasuaji wa macho.

Amefafanua kuwa kiini cha tukio hili ni kujipatia kipato kisicho halali, na kwamba wafanyakazi katika chumba hicho cha upasuaji waliokamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo ni Paul Igosha (37), mkazi wa Somanda, Neema Msekile (24), mkazi wa Kidinda na Edward Yirika (27), mkazi wa Somanda ambao wote ni wauguzi katika chumba cha upasuaji wa macho katika hospitali ya Nyaumata'.

Kamanda Abwao ameeleza kuwa baada ya tukio hilo kuripotiwa kituoni hapo upelelezi mkali ulianza mara moja kwa kukagua eneo la tukio na kuhoji baadhi ya mashahidi na baada ya mahojiano hayo timu hiyo ya makachero waliwakamata watumishi wa chumba cha upasuaji wa hospatali hiyo ambao ni Paul Igosha, Neema Msekile na Edward Yirika ambao walihojiwa lakini walikanakuhusika na tukio hilo.

Amesema kuwa jana Septemba 22. 2021 jeshi la polisi lilimkamata, Allen Cosmas (30), ambaye ni daktari wa usingizi, chumba cha upasuaji ambaye pia alihojiwa na makachero na hatimaye kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alieleza kuwa mashine hiyo ameuza mkoani Mwanza.

Chanzo:- Clouds Tv
Milioni Nane kasoro unaenda jera!!hizi akili hizi
 
Sidhani kama aliyekamatwa ni daktari bingwa wa usingizi, kuna vitu tunachanganya. Huyo bila shaka ni ‘Muuguzi wa kutoa dawa za Usingizi’ au Nurse anaesthetist.

Ni nadra kumkuta Anesthesiologist mikoani.
Kwanini usimkute mkoani? Ni wachache sana? Au they are highly demanded?
 
hivi hao ma Doc waliokamatwa na imebainika hawajahusika si wamesababishiwa usumbufu na fedheha,je hawawezi kuishitaki serikali ?
Polisi wetu ni wataalamu wa kukamata, uchunguzi sifuri. Washukuru hatuna mahakama huru, mashitaka ya madai yangewaandama kila leo.
 
Unasoma kazi ya "kutoa dawa za usingizi"...unalipwa MSHAHARA....unashindwaje kujiongeza "kazi za nje" kutoa "usingizi" katika hospitali za binafsi muda wako wa nyongeza?!!!Khaaa

Mwizi ni mwizi tu....huwa ni mbaya zaidi anapoliibia TAIFA....
Wa aina hii ndio huwauzia wezi dawa za usingizi ili wapulize na kuvunja majumba.
 
Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watumishi watatu wa Idara ya afya kwa wizi wa mashine ya kuangalia Mapigo ya Moyo, Upumuaji, Wingi wa hewa ya Oksijeni katika damu kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji ambapo mashine hiyo iliibiwa ikiwa ndani ya chumba cha upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Nyaumata.

Katika taarifa iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao imeeleza kuwa uchunguzi uliofanywa katika Hospitali hiyo umebaini kuwa chumba hicho cha upasuaji hakikuvunjwa.

Amesema kuwa Septemba 20.2021, Getrude Emmanuel (45), ambaye ni katibu wa hospitali ya mkoa wa Simiyu, aligundua kuibiwa kwa mashine hiyo inayojulikana kwa jina la Cadiac Monitor Accessories yenye namba za usajili EX-7C051585 yenye thamani ya shilingi .7,820,000/= iliyokuwa kwenye chumba cha kufanyia upasuaji wa macho.

Amefafanua kuwa kiini cha tukio hili ni kujipatia kipato kisicho halali, na kwamba wafanyakazi katika chumba hicho cha upasuaji waliokamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo ni Paul Igosha (37), mkazi wa Somanda, Neema Msekile (24), mkazi wa Kidinda na Edward Yirika (27), mkazi wa Somanda ambao wote ni wauguzi katika chumba cha upasuaji wa macho katika hospitali ya Nyaumata'.

Kamanda Abwao ameeleza kuwa baada ya tukio hilo kuripotiwa kituoni hapo upelelezi mkali ulianza mara moja kwa kukagua eneo la tukio na kuhoji baadhi ya mashahidi na baada ya mahojiano hayo timu hiyo ya makachero waliwakamata watumishi wa chumba cha upasuaji wa hospatali hiyo ambao ni Paul Igosha, Neema Msekile na Edward Yirika ambao walihojiwa lakini walikanakuhusika na tukio hilo.

Amesema kuwa jana Septemba 22. 2021 jeshi la polisi lilimkamata, Allen Cosmas (30), ambaye ni daktari wa usingizi, chumba cha upasuaji ambaye pia alihojiwa na makachero na hatimaye kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alieleza kuwa mashine hiyo ameuza mkoani Mwanza.

Chanzo:- Clouds Tv
Akili ndogo tamaa kubwa unaiba m7 sasa mnaigawaje
 
Ukiondoa polisi kwa kuendekeza njaa wanofuatia ni madaktari.

Hawa nao njaa kali sana, hawatosheki na mishahara yao kuendesha maisha.
Wengi wanaendesha maisha kwa pesa ya damu.

Kuna yule wa Tanga aliyefumua mishono ya mgonjwa baada ya mgonjwa kushindwa kumpatia rushwa.
 
Back
Top Bottom