Daktari wa Upasuaji akiri kuiba machine ya kuangalia mapigo ya Moyo Hopitali ya Rufaa Simiyu na kuiuza Mkoani Mwanza

Sidhani kama aliyekamatwa ni daktari bingwa wa usingizi, kuna vitu tunachanganya. Huyo bila shaka ni ‘Muuguzi wa kutoa dawa za Usingizi’ au Nurse anaesthetist.

Ni nadra kumkuta Anesthesiologist mikoani.
kumbuka kuna hata CO wamesoma Anaesthesia so usiconfirm kwa kusema atakua nurse Anesthetist
 
Huyo daktari wa miaka 30, tena ni bingwa!
Huyo ni nurse tu, sema tu polisi hawawajui madaktari
Sisi wagonjwa tukienda Hospitalini kila tunayemwona amevaa mavazi ya Hospitalini tunajua ni Daktari, nao Polisi ni kama sisi
 
kumbuka kuna hata CO wamesoma Anaesthesia so usiconfirm kwa kusema atakua nurse Anesthetist
Najua. Ila CO sio daktari. Hoja yangu tunachanganya ‘Daktari bingwa wa usingizi’ na ‘Paramedics in Anaesthesia’
 
dodoma,arusha,dsm,mbeya na mwanza huwezi kusema mkoani lazima useme jijini
Hata Dar es salaam, Arusha, mbeya ,Dodoma na Mwanza ni mikoani. Kwa kawaida mikoa nje ya Dar es salaam ndio huitwa mikoani. Kwa maana Dar ndio centre of all activities in Tanzania
 
Ukiondoa polisi kwa kuendekeza njaa wanofuatia ni madaktari.

Hawa nao njaa kali sana, hawatosheki na mishahara yao kuendesha maisha.
Wengi wanaendesha maisha kwa pesa ya damu.

Kuna yule wa Tanga aliyefumua mishono ya mgonjwa baada ya mgonjwa kushindwa kumpatia rushwa.
Yule ni CO,hakuwa daktari. Wananchi wengi hawajui kutofautisha kada katika afya.
 
Ukisikia elimu kutomsaidia mtu ndio huku sasa,

Dactari mzima unajiingiza katika wizi wa kifaa cha 7M, tena ambacho utauza kwa si zaidi ya 4M, maana huwezi toa 7M kwa mashine ya Wizi na chakavu ikiwa bei hio hio unapata Mpya na Halali.

Wote damu changa, tamaa za kizembe kama za baadhi ya vijana wasio na kazi mtaani,
Sasa sisi tusio na kazi huku mtaani tumeingiaje hapo maisha yatunyanyase na wewe pia???
 
Huyu mtaalamu aliyeaminiwa na kuajiriwa na Serikali anakiri kuiba kitendea kazi, baada ya kuiba angeendeleaje na kazi? Bora angejitetea aliiazima kwa ajili ya kufanyia shughuli za 'kliniki tembezi', bahati mbaya hakuomba ruhusa.

Uwekezaji unaongeza ajira, lakini Wawekezaji wanalalamika Watanzania ni wezi, wavivu, wazembe na visingizio kuomba ruhusa kila uchao. Wanaomba kuajiri wageni na kuachana na Wabongo. NDIYO HAYA
 
Back
Top Bottom