Daktari wa Upasuaji akiri kuiba machine ya kuangalia mapigo ya Moyo Hopitali ya Rufaa Simiyu na kuiuza Mkoani Mwanza

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,149
12,818
Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watumishi watatu wa Idara ya afya kwa wizi wa mashine ya kuangalia Mapigo ya Moyo, Upumuaji, Wingi wa hewa ya Oksijeni katika damu kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji ambapo mashine hiyo iliibiwa ikiwa ndani ya chumba cha upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Nyaumata.

Katika taarifa iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao imeeleza kuwa uchunguzi uliofanywa katika Hospitali hiyo umebaini kuwa chumba hicho cha upasuaji hakikuvunjwa.

Amesema kuwa Septemba 20.2021, Getrude Emmanuel (45), ambaye ni katibu wa hospitali ya mkoa wa Simiyu, aligundua kuibiwa kwa mashine hiyo inayojulikana kwa jina la Cadiac Monitor Accessories yenye namba za usajili EX-7C051585 yenye thamani ya shilingi .7,820,000/= iliyokuwa kwenye chumba cha kufanyia upasuaji wa macho.

Amefafanua kuwa kiini cha tukio hili ni kujipatia kipato kisicho halali, na kwamba wafanyakazi katika chumba hicho cha upasuaji waliokamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo ni Paul Igosha (37), mkazi wa Somanda, Neema Msekile (24), mkazi wa Kidinda na Edward Yirika (27), mkazi wa Somanda ambao wote ni wauguzi katika chumba cha upasuaji wa macho katika hospitali ya Nyaumata'.

Kamanda Abwao ameeleza kuwa baada ya tukio hilo kuripotiwa kituoni hapo upelelezi mkali ulianza mara moja kwa kukagua eneo la tukio na kuhoji baadhi ya mashahidi na baada ya mahojiano hayo timu hiyo ya makachero waliwakamata watumishi wa chumba cha upasuaji wa hospatali hiyo ambao ni Paul Igosha, Neema Msekile na Edward Yirika ambao walihojiwa lakini walikanakuhusika na tukio hilo.

Amesema kuwa jana Septemba 22. 2021 jeshi la polisi lilimkamata, Allen Cosmas (30), ambaye ni daktari wa usingizi, chumba cha upasuaji ambaye pia alihojiwa na makachero na hatimaye kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alieleza kuwa mashine hiyo ameuza mkoani Mwanza.

Chanzo:- Clouds Tv
 
Ukisikia elimu kutomsaidia mtu ndio huku sasa,

Dactari mzima unajiingiza katika wizi wa kifaa cha 7M, tena ambacho utauza kwa si zaidi ya 4M, maana huwezi toa 7M kwa mashine ya Wizi na chakavu ikiwa bei hio hio unapata Mpya na Halali.

Wote damu changa, tamaa za kizembe kama za baadhi ya vijana wasio na kazi mtaani,
 
Ukisikia elim kutomsaidia mtu ndio huku sasa,

Dactari mzima unajiingiza katika wizi wa kifaa cha 7M, tena ambacho utauza kwa si zadi ya 4M, maana huwezi kuna na 7M yakuipata kihalali na mpya halafu ukaamua kuiba chakavu...

Wote dumu changa, tamaa za kizembe kama za baadhi ya vijana wasio na kazi mtaani,
Kweli wizi ni mbaya sana......huyo Dr atashtakiwa but the good thing is that hiyo mashine hata huko Mwanza ilikwenda kutibu watu sio fisi....
ni change of venue tu
Dr mzima anaibaje!!???
 
Ukisikia elim kutomsaidia mtu ndio huku sasa,

Dactari mzima unajiingiza katika wizi wa kifaa cha 7M, tena ambacho utauza kwa si zadi ya 4M, maana huwezi kuna na 7M yakuipata kihalali na mpya halafu ukaamua kuiba chakavu...

Wote dumu changa, tamaa za kizembe kama za baadhi ya vijana wasio na kazi mtaani,
Washughulikiwe haswa hao majinga!
 
Sidhani kama aliyekamatwa ni daktari bingwa wa usingizi, kuna vitu tunachanganya. Huyo bila shaka ni ‘Muuguzi wa kutoa dawa za Usingizi’ au Nurse anaesthetist.

Ni aghalabu kumkuta Anesthesiologist mikoani.
Hapo kwenye neno 'aghalabu' nafikiri usahihi wake ni neno 'nadra' kulingana na maudhui ambayo nahisi ulikusudia kuyawasilisha.
 
Ukisikia elim kutomsaidia mtu ndio huku sasa,

Dactari mzima unajiingiza katika wizi wa kifaa cha 7M, tena ambacho utauza kwa si zadi ya 4M, maana huwezi toa 7M kwa mashine ya Wizi na chakavu ikiwa bei hio hio unapata Mpya na Halali.

Wote dumu changa, tamaa za kizembe kama za baadhi ya vijana wasio na kazi mtaani,
hivi hao ma Doc waliokamatwa na imebainika hawajahusika si wamesababishiwa usumbufu na fedheha,je hawawezi kuishitaki serikali ?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom