Daktari wa Upasuaji akiri kuiba machine ya kuangalia mapigo ya Moyo Hopitali ya Rufaa Simiyu na kuiuza Mkoani Mwanza

Ina wezekana,mbona Chato inaitwa mkoa ikiwa nda ya mkoa wa Geita,
Mkoa wa Kinondoni,mkoa wa Temeke,mkoa wa Tarime.
Tarime ni wilaya Boss,na Chato ni wilaya bado haijawa Mkoa na pia sina hakika kama Kinondoni na Temeke ni mikoa maana ingekua na mkuu wa mkoa
 
Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watumishi watatu wa Idara ya afya kwa wizi wa mashine ya kuangalia Mapigo ya Moyo, Upumuaji, Wingi wa hewa ya Oksijeni katika damu kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji ambapo mashine hiyo iliibiwa ikiwa ndani ya chumba cha upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Nyaumata.

Katika taarifa iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao imeeleza kuwa uchunguzi uliofanywa katika Hospitali hiyo umebaini kuwa chumba hicho cha upasuaji hakikuvunjwa.

Amesema kuwa Septemba 20.2021, Getrude Emmanuel (45), ambaye ni katibu wa hospitali ya mkoa wa Simiyu, aligundua kuibiwa kwa mashine hiyo inayojulikana kwa jina la Cadiac Monitor Accessories yenye namba za usajili EX-7C051585 yenye thamani ya shilingi .7,820,000/= iliyokuwa kwenye chumba cha kufanyia upasuaji wa macho.

Amefafanua kuwa kiini cha tukio hili ni kujipatia kipato kisicho halali, na kwamba wafanyakazi katika chumba hicho cha upasuaji waliokamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo ni Paul Igosha (37), mkazi wa Somanda, Neema Msekile (24), mkazi wa Kidinda na Edward Yirika (27), mkazi wa Somanda ambao wote ni wauguzi katika chumba cha upasuaji wa macho katika hospitali ya Nyaumata'.

Kamanda Abwao ameeleza kuwa baada ya tukio hilo kuripotiwa kituoni hapo upelelezi mkali ulianza mara moja kwa kukagua eneo la tukio na kuhoji baadhi ya mashahidi na baada ya mahojiano hayo timu hiyo ya makachero waliwakamata watumishi wa chumba cha upasuaji wa hospatali hiyo ambao ni Paul Igosha, Neema Msekile na Edward Yirika ambao walihojiwa lakini walikanakuhusika na tukio hilo.

Amesema kuwa jana Septemba 22. 2021 jeshi la polisi lilimkamata, Allen Cosmas (30), ambaye ni daktari wa usingizi, chumba cha upasuaji ambaye pia alihojiwa na makachero na hatimaye kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alieleza kuwa mashine hiyo ameuza mkoani Mwanza.

Chanzo:- Clouds Tv
Unasoma kazi ya "kutoa dawa za usingizi"...unalipwa MSHAHARA....unashindwaje kujiongeza "kazi za nje" kutoa "usingizi" katika hospitali za binafsi muda wako wa nyongeza?!!!Khaaa😲😲

Mwizi ni mwizi tu....huwa ni mbaya zaidi anapoliibia TAIFA....
 
Polisi wa bongo wanaweza kukupa kibano hadi ukakiri kosa wakati sio kweli.

Yule dereva tax alipewa kibano hadi akakiri kumteka Mo Dewji.
 
Mbona dokta kaiba mashine kidogo afu maneno Kama yote. Mnayajua watu wanajenga majengo ya serikali kwa kiwango kidogo.
Mwalimu anafundisha kishingo upande anatoa watalaamu wachanga.
 
Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watumishi watatu wa Idara ya afya kwa wizi wa mashine ya kuangalia Mapigo ya Moyo, Upumuaji, Wingi wa hewa ya Oksijeni katika damu kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji ambapo mashine hiyo iliibiwa ikiwa ndani ya chumba cha upasuaji mkubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Nyaumata.

Katika taarifa iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao imeeleza kuwa uchunguzi uliofanywa katika Hospitali hiyo umebaini kuwa chumba hicho cha upasuaji hakikuvunjwa.

Amesema kuwa Septemba 20.2021, Getrude Emmanuel (45), ambaye ni katibu wa hospitali ya mkoa wa Simiyu, aligundua kuibiwa kwa mashine hiyo inayojulikana kwa jina la Cadiac Monitor Accessories yenye namba za usajili EX-7C051585 yenye thamani ya shilingi .7,820,000/= iliyokuwa kwenye chumba cha kufanyia upasuaji wa macho.

Amefafanua kuwa kiini cha tukio hili ni kujipatia kipato kisicho halali, na kwamba wafanyakazi katika chumba hicho cha upasuaji waliokamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo ni Paul Igosha (37), mkazi wa Somanda, Neema Msekile (24), mkazi wa Kidinda na Edward Yirika (27), mkazi wa Somanda ambao wote ni wauguzi katika chumba cha upasuaji wa macho katika hospitali ya Nyaumata'.

Kamanda Abwao ameeleza kuwa baada ya tukio hilo kuripotiwa kituoni hapo upelelezi mkali ulianza mara moja kwa kukagua eneo la tukio na kuhoji baadhi ya mashahidi na baada ya mahojiano hayo timu hiyo ya makachero waliwakamata watumishi wa chumba cha upasuaji wa hospatali hiyo ambao ni Paul Igosha, Neema Msekile na Edward Yirika ambao walihojiwa lakini walikanakuhusika na tukio hilo.

Amesema kuwa jana Septemba 22. 2021 jeshi la polisi lilimkamata, Allen Cosmas (30), ambaye ni daktari wa usingizi, chumba cha upasuaji ambaye pia alihojiwa na makachero na hatimaye kukiri kuhusika na tukio hilo, ambapo alieleza kuwa mashine hiyo ameuza mkoani Mwanza.

Chanzo:- Clouds Tv
Mishahara ni midogo Sana, chuoni nakosoma unakuta lecturer mwenye PhD yake anahangaika na kuku, wengine vihostel, wengine Hadi ruhuma maisha wanayoishi. Ndo maana efficiency inapungua na mtu anakua sio productive. Stress na maisha. Kuna doctor mmoja rafiki yangu nafuga nae nguruwe. Binafsi Hilo tukio siwez shangaa hata kidogo.
 
Inaonesha bado hujapevuka
 
Back
Top Bottom