Daktari ambaka mgonjwa

RayB

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
2,752
196
DAKTARI wa Hospitali ya Marie Stoppers iliyopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, Paul Andrew ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyefika hospitalini hapo kupatiwa matibabu.

Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga zimesema kuwa mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa tumbo ndipo Dk. Andrew alimwandikia kipimo cha Utra Sound.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Kamanda Kalinga alisema kwa mujibu wa mgonjwa huyo, alifika hospitalini hapo majira ya jioni na baada ya kueleza tatizo lake, Dk Andrew alimwandikia kipimo hicho.

Kamanda Kalinga alieeleza kuwa baada ya kuingia katika chumba cha kufanyiwa kipimo, ndipo daktari huyo alimpa kitu kilichomfanya alale kwa muda na nguvu ya dawa ilipokwisha alishtuka na kumkuta daktari huyo akiendelea kumbaka.

"Baada ya kumkuta daktari akimbaka, mgonjwa huyo alitoka na kukimbilia Kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama na kufungua jalada lenye namba RB/KJN/123/552/10," alieleza.

Alisema askari hao walirudi na mgonjwa huyo hospitali na kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa bado yupo eneo hilo.

Kamanda alisema mgonjwa huyo amefanyiwa vipimo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kubaini kama kweli alifanyiwa unyama huo.

Alisema mtuhumiwa bado anashikiliwa na polisi na leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo.

Source: Tanzania Daima

My take

Mimi kwa kweli hawa madaktari wa magonjwa ya akina mama aka gynecologists huwa siwaamini kabisa from my experience ya kuwa nao jirani wengi huwa wanakula wagonjwa wao
 
Uchizi mwingine bwana!? Ina maana alishindwa kumtongoza au kumhonga au kumbembeleza..? Mifadhaiko mingine bwana!?
 
Marie Stopes pameoza, kwanza ni mabingwa wa abortion wale, pili wanaojiita ma Dr wa kiume wanapenda sana kutongoza wagonjwa wa kike, nimeshuhudia mara nyingi tuu, kuna dada nafanya nae kazi hapa alikuwa anatupa issue jinsi alivyomtongoza na alivyokuwa akipokea simu yake kila dakika wanawake wakimpigia, anamwambia huyu ananiwekeaga maji ya moto nikienda kwake, huyu wa Lunch huyu wa mtoko si mchezo huyo jamaa
 
Yaani kwa kifupi hawa madaktari wa hivi vihospitali wana njaa za ajabu sana na kwa kweli sijui kwanini wanabahatika kweli manake na wanawake nao hata wakiombwa na hao wanakuwa rahisi sana kuvua sijui ni kwanini
 
Hayo ni matatizo ya madaktari mmoja-mmoja, si Marie Stopes. Hivi inawezekana kweli taasisi ikawa na madaktari fuska watupu?
 
Wapi professionalism?

Masanilo....popote ulipo unaweza toa mwongozo kidogo hapa?
 
Du! hii hatari sana. Suluhu pekee ni kuwaajiri madaktari wanawake tu. Au na wenyewe wana njaa?
 
Uchizi mwingine bwana!? Ina maana alishindwa kumtongoza au kumhonga au kumbembeleza..? Mifadhaiko mingine bwana!?

...inaonekana ndio tabia yake, '40' yake imetimia.

Yaani kwa kifupi hawa madaktari wa hivi vihospitali wana njaa za ajabu sana na kwa kweli sijui kwanini wanabahatika kweli manake na wanawake nao hata wakiombwa na hao wanakuwa rahisi sana kuvua sijui ni kwanini

...'fetish' hizo, kaugonjwa kabaya sana.

Wapi professionalism?

...100% right, wapi maadili ya taaluma?
 
Du! hii hatari sana. Suluhu pekee ni kuwaajiri madaktari wanawake tu. Au na wenyewe wana njaa?

Tujitahidi kusomesha mabinti masomo ya sayansi. Itasaidia sana kupunguza matatizo kama haya. Kwa sasa madaktari wengi bingwa wa magonjwa ya kina mama ni wanaume! Ningependa siku moja hili liwe kinyume.

Nampa pole huyo mgonjwa! Sasa kama ni mke wa mtu sijui inakuwaje hapo!
 
Hawa madktari wa marrie stopes wahuni sana hata daadangu.

Majuzi alikuwa anaangaliwa kitu tumboni anasema alikuwa akishikwa shikwa mara kwa maa kama jamaa anatafutia speed ya kuanzia.

Dada pole sana ;kuna bosi wao wa kihaya huyu ni malaya wa kuubuhu usiguse pale wale madada wa mwenge ana[/u]kula hadi wake za watu kuwadanganya na ajira
 
Hawa madktari wa marrie stopes wahuni sana hata daadangu
majuzi alikuwa anaangaliwa kitu tumboni anasema alikuwa akishikwa shikwa mara kwa maa kama jamaa anatafutia speed ya kuanzia
dada pole sana ;kuna bosi wao wa kihaya huyu ni malaya wa kuubuhu usiguse pale wale madada wa mwenge ana[/u]kula hadi wake za watu kuwadanganya na ajira

Labda swali lingine tujiulize pamoja na Marie stopes hivi vihospitali vingine hawa ni wataalamu kweli wa kuitwa madaktari? Je wizara husika huwa inafanya ukaguzi wa mara kwa mara na kupitia qualification za watumishi mbalimbali wa idara ya afya huko mahospitali? Manake nasikia hat yule jamaa aliyekamatwa pale TIP-TOP ni dentist tena ni Diploma (Habari toka kwa mtu wake wa karibu)
 
Wapi professionalism?

Masanilo....popote ulipo unaweza toa mwongozo kidogo hapa?

Hii nilikuwa sijaiona!

Dr Andrew amebaka na ameaibisha professional! Alipata mfedheheko wa ghafla maana wagonjwa wengine bwana vishawishi sana. Kupunguza uwezekano wa kupata hilo anguko angekaa na nurse pale wakati akimuhudumia....Hebu fikiria unamchojoa mgonjwa nguo zote halafu unamwambia chuchumaa! LOL Dr unajifanya kuchungulia yale maeneo hahahahaha pangumu hapo kama unaukame yanakukuta ya Dr Andrew.

Thats mental disorder huyo Dr inabidi apelekwe kwa psychiatric kwa msaada zaidi na si kufunguliwa kesi!
 
My take

Mimi kwa kweli hawa madaktari wa magonjwa ya akina mama aka gynecologists huwa siwaamini kabisa from my experience ya kuwa nao jirani wengi huwa wanakula wagonjwa wao

wapo ambao ni waadilifu na wanafata maadili ya kazi zao ..lakini huyu nae kavuka mipaka
sijui hata kama alikumbuka kutumia kinga ..naogopa!!
 
Huyu daktari aliamua kuweka weledi na kiapo chake pembeni kabisa na nafsi yake ikaanza kuongozwa na kichwa cha chini badala ya kichwa cha juu.,pole sana dada uliyepatwa na zahma hii, naamini mpumbavu huyu atapata malipo ya udhalimu wake hapa hapa diniani.
 
Hii nilikuwa sijaiona!

Dr Andrew amebaka na ameaibisha professional! Alipata mfedheheko wa ghafla maana wagonjwa wengine bwana vishawishi sana. Kupunguza uwezekano wa kupata hilo anguko angekaa na nurse pale wakati akimuhudumia....Hebu fikiria unamchojoa mgonjwa nguo zote halafu unamwambia chuchumaa! LOL Dr unajifanya kuchungulia yale maeneo hahahahaha pangumu hapo kama unaukame yanakukuta ya Dr Andrew.

Thats mental disorder huyo Dr inabidi apelekwe kwa psychiatric kwa msaada zaidi na si kufunguliwa kesi!

Hawa jamaa wanawaharibia sana professional zenu mzee......! ningekuwa mi ni mume wa huyo mama, ngejifanya PSYCHIATRIC then, na yeye na mpa nusu kaputi.......then natafuta njemba zimpumlie kisogoni........!
 
hahaaa binamu hicho kisasi balaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom