p53 pamoja na mawazo yako mazuri, umeonyesha dharau kubwa kwa wataalamu wetu. Una maana gani kuwakandya ma-Clinical Officer? Hivi unafahamu 90% ya wanaotoa huduma katika vituo vya afya, zahanati na hospitali Tanzania ni Clinical Officers? Na kwa taarifa yako kuna MD wengi mabomu na wabakaji.
Sikuonyesha dharau bali nimesema ukweli.Sasa kama kusema ukweli ni dharau basi na nihukumiwe!Vilevile sijasema kwamba MD wote wako perfect.Si ni binadamu hawa,sasa watakuwaje wakamilifu?Sema nchi zetu hizi zisizokuwa na utawala wa sheria na wananchi wasiojua haki zao.Wenzetu wako makini sana na miiko ya taaluma.Huwezi kuchezeachezea wagonjwa tu halafu ukategemea utasalimika.Vinginevyo itakutokea puani na utajuta kwanini ulienda medical school!