Dah! wanawake mtatuua kwa mateso sana

Dah! wanawake mtatuua kwa mateso sana

Pole sana jipe moyo hayo yote yatapita mshukuru Mungu kwa kila jambo jipange upya kuna maisha baada ya kuachwa, jifunze kuandika Mungu kwa herufi kubwa, yaani Mungu na siyo mungu.
 
Hapo ndipo wanapofeli kumbe basi nimeelewa
Yeah, ni tatizo kubwa but kwangu naona hata ikitokea nitakua na amani tu (sipo kwenye hii issue though), ukifanya kitu usifanye kwa kutegemea kupata kitu!
 
Mbeya nakuja tarehe moja utakuwepo nataka tule vyukuuu
Tujipe pole kwakweli.Halafu Yule dada alirudi na anaomba msamaha mpaka kesho.

Unajua nipo wp this time? Dodoma-Chemba huku naitafuta Mbeya
 
Uzembee tu huo. .Hamna cha mzunguko wala nini --- maisha Yana endeshwa na kanuni - ukitoka nje ya kanuni husika lazima yatakuadhibu tu. ..

Let me tell you this mkuu--- Binaadamu Huwa tunapo kutana na changamoto mbali mbali zinazo tuumiza huwa tuna desturi ya kuwalaumu watu au mazingira yaliyo pelekea kutuumiza,,

Huwa hatujipi time ya kujikagua vyema ili tuweze walau kujua mistake tulizo zifanya ambazo zilipelekea kutoa chance kwa watu wabaya na mazingira mabaya ili ya weze kutuumiza. ... Tukijenga desturi ya kujifanyia, tathmini ya wapi tulipokosea ' itatupatia experience so itakuwa ni nadra next kufanya makosa Yale Yale '' pia itatusaidia kuweza kuwapa ushauri wenzetu wanao kabiliwa na changamoto ambayo sisi, tulisha wahi kuipitia
Huwa wanasahau mkuu , halafu anamlaumu mwenzie badala ya kujivhunguza yeye mwenyewe kakosea wapi tutafike tu hata tukiwa vibogoyo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahaha Akamgeuze Kuku tu
Wangerogwa wengi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa maumivu haya, itakuwa alimwacha mwingine kisa kapata kisu [emoji23][emoji23][emoji23] sasa kimemgeukia
 
Habari wakuu

Japo sio swala jipya ila hata hii ni yenyewe[emoji22]


SITOMWAMINI MWANAMKE TENA

Nimeamua kulielezea hili kuhusu wewe mwanamke tuliyedumu ktk mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja. Sio siri kwa sasa umenipa wakati mgumu sana ktk mapenzi na sikutegemea kama ungenifanyia jambo gumu hivi.

Nakumbuka tulipoanza mahusiano yetu na uliponithibitishia huna mtu kabsa kimapenzi nikajikuta nakupenda tena moyo wangu ulishafika tamati kwako ulionyesha mapenzi ya dhati kwangu sikujua kama mwenzangu ulikua unatafuta njia ya kutoka.

Nakumbuka Ulikubali kwenda kunitambulisha kwenu na nilipokelewa vzr na ndugu zako nilifurahi sana kwa kua nilijua sasa nakaribia kupata mke. Lkn nilishangaa kila ninapokwambia nataka kuleta barua ulikataa na kuniambia bado itanijulisha.

Kwakua tulishafikia muda kdg ktk mapenzi yetu lkn kilichonishangaza kingine hukutaka kabsaa tukutane bila kutumia condom. Hii ilinipa maswali kdg ila sio mbaya nilijipa moyo mpaka tutakapofunga ndoa. Kwakua nashukuru mungu hela ya mboga na kuvaa sikosi Maana nimeajiriwa kwenye kampuni moja binafsi.

Siku hiyo ulinambia nikununulie vitu vya ndani upelekeke kwenu Maana wazazi wako wanapata shida vitu ni vya zamani halafu vimechoka.nikakununulia kitanda godoro sofa TV nikamalizia na fridge tukapeleka kwenu.

Baada ya miezi miwili kupita ukaniomba nikupe milioni moja ili ufanye biashara ikabidi nichukue mkopo wa milioni mbili kazini. Nikakupa laki nane ili uanze na hiyo biashara cha kushangaza kupita wiki tu ukawa hupatikani kwenye simu nikija kwenu naambiwa umesafiri tena nashangaa bila kuniaga!!

Kuna siku nilikupigia tena simu akapokea mwanaume akanitukana sana yaani ni mtu ambaye una mahusiano nae mda mrefu kabla yangu daaah we mwanamke una roho ngumu sana. Kwanini ulinificha na kuniaminisha mimi ndo wako ili tuje kuoana!!

Ila namshukuru sana mdogo wako siku nilipoenda kwenu tena ndipo akaniita pembeni na kunieleza kila kitu. Kumbe kwangu ulifanya njia ya mafanikio tu lkn uliyempenda ulikua nae. Yaan vitu nilivyonunua mimi umeenda kupanga chumba unaishia na mwanaume uliyempenda. Pia pesa niliyokupa uliyoniomba kwa nia ya biashara umempa huyo mwanaume kaongezea kanunua bodaboda yote nimeambiwa.

Nakupigia simu unamijibu nyodo na kejeri. Ila sawa mi huu mkopo nitaulipa ila namuachia mungu kwa uliyonifanyia. Umenifanya niyachukie mapenzi na nisimuamini mwanamke yeyote sasaivi. Chozi langu namuachia mungu yeye ndo atahukumu. Najua huu ujumbe lazima ukufikie lkn nikwambie tu mi nakutakia kila la kheri

cc: joanah
Aisee!
 
Back
Top Bottom