Dadangu anahitaji msaada, anaweza kujiua muda wowote!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
KIMSINGI, huu si utani na imetokea bahati mbaya tu kwamba nilipotea njia nikajikuta humu! Nimetafuta japo upenyo wa kutokea, nimeshindwa kuuona na hivyo nimeonelea niyaeleze humu humu! POINT OF NOTE, huu si utani but really my sister anahitaji msaada otheerwise anaweza kufanya maamuzi mabaya ikiwa hata pamoja na kujiondoa uhai.

Nina dada angu wa mama mkubwa; tunapendana sana na dada angu huyu kv tumekusoma wote Primary hadi O-level na tukaachana A-level ambapo yeye alienda kusoma Jangwani. Kwa wanafunzi wa Jangwani S.S 2004/2006 wataakuwa wanamfahamu dada huyu jinsi ambavyo alivyo na uzuri wa kipekee! Kimsingi, kila mmoja alimfahamu.

Tatizo linalomsumbua dadangu huyu ni ndoto zinazomfanya awe anakojoa kitandani hata mara mbili au tutu ktk usiku mmoja! Kahangaika sana, ikiwa na kwa wataalamu wa dawa za asili ili aonokane na janga hili lakini ameshindwa. Pamoja na uzuri wake, anakataa kuolewa kv anafahamu nini kitatokea (mpeni pole dadangu)!

Baada ya kuhangaika sana, akaja shangazi yetu toka kijijini. Baada ya kumsimulia mkasa wa sister; akadai hilo ni tatizo dogo sana na kwamba yupo mganga mmoja aliyekuwa anaishi kijijini zamani na sasa yupo dar! Akaahidi atamtafuta ili aondoe kabisa tatizo la dadangu mpendwa!

Baada ya kupewa matumaini hayo, dadangu ikabidi amkubalie kaka mmoja ambae kwa muda mrefu alitoa pendekezo la kutaka kumuoa! Hata hivyo, sister alikuwa anamtolea nje huyo jamaa ingawaje alikuwa akimpenda. Alikata shauri la kuumia na nafsi yake kuliko kwenda kujidhalilissha! Hivyo, baada ya kupewa matumaini kwamba tatizo lake litaisha tu; ndipo akaamua kumkubalia huyo jamaa!
Kwa bahati mbaya au mzuri, huyo jamaa anaishi Nairobi, na alikuwa amebakiwa na siku chache sana kuondoka. Kutokana na hilo na hilo, alikusudia kufunga nae ndoa mapema iwezekanavyo ili aondoke na mke wake! Kutokana na haraka hiyo, ndipo shangazi nae akaharakisha kumtafuta yule mganga; na kweli akapatikana!

Siku aliyokuja mganga ni siku ambayo ilipangwa kufungwa hiyo ndoa jambo lililomfurahisha sana dadangu! Kweli, jioni ya kufungwa kwa ndoa hiyo, mganga alikuja na kukutana na dada!

Baada ya dada kumsimulia mganga, ndipo mganga yule alipomwambia kwamba anasumbuliwa na Jini Tij! Akampa dawa na kumwambia kwamba usiku huo akiwa usingizi jini litamtokea na kumshuhudia kwa macho yake. Mganga akaendelea kumwambia dadangu kwamba, akishamuona tu huyo Jini, amkimbize hadi apotee kabisa kwenye upeo wa macho yake. Mganga akadai kwamba, akishamkimbiza hadi akapotea kabisa basi huo ndo utakuwa ndio mwisho wa jini huyo kumtokea na hatakojoa tena kitandani!

Ndoa ikafungwa! Kwavile shemeji yangu anajiweza akaamua kwenda kula Honey Moon na dadangu kwenye Hotel moja maarufu sana hapa jijini ( Kwa sababu za kibiashara, sitaitaja hotel hiyo). Baada ya maongezi yao ya hapa na pale, mara wote wakapitiwa usingizi. Kama ambavyo mganga alisema; akiwa kati kati ya usingizi mzito, mara dadangu akamuona yule Jini Ji! Hapo ndipo dadangu alipokumbuka maelekezo ya mganga wake hivyo bila kupoteza muda akaanza kumkimbiza huyo jini! Walikimbizana kwa umbali mrefu hadi wakafika mitaa ya Magomeni! Yule jini alivyoona ameshiwa na pumzi, ikabidi aingie kwenye choo kimoja pale mtaa wa Idrisa kama unaelekea kituo cha Morroco hotel.

Dadangu kwavile alikuwa na hasira sana na jini yule, nae akaingia huko huko chooni! Jini kuona amefuatwa hadi chooni akaamua kutumbukia kwenye lindi la choo! Dadangu kuona vile, akaamua hii ndio nafasi yake ya kumshikisha adabu Jini Ji hivyo bila kufikiria mara mbili akashusha underwear yake na kuanza kukata gogo huku akiamini anamnyea yule jini hasidi!

Wakati akiendelea kujikamua ili ashushe gogo lingi zaidi ili amkomeshe jini; mara akashtukia anapigwa kofi! Kushituka, akajikuta amejinyea kitandani! Kwenye kitanda cha hotel maarufu jijini! Leo nimefika pale hotelini asubuhi hii, stori zilizotawala kwa wale wahudumu ni za dadangu kujinyea kitandani!

Dadangu ikabidi atoroke usiku huo huo na sasa amejificha sehemu ni mimi tu ndie napafahamu huku akitishia heri ajiue!
Tafadhali wadau, mwenye kumsaidia dadangu, ama kwa tiba au kwa ushauri basi afanye hivyo! Nisingependa kumuona dadangu akiendelea kuwa na hali kama hii ya upweke inayohatarisha hata maisha yake!
 
Haya mambo ya kutishiana "kujiua bado yapo" hebu mpe kamba au vidonge vya fragile na glasi ya pombe tuone!
 
Hichi ni kichekesho cha zamani eti umemuweka dadako,anyway mlete tu kwangu akojoe na kunya kitandani wala hamna shida.
 
duh mpe pole sana....
mwambie amweleze mumewe tatizo lake from a to z,kama atamstahimili hivyo hivyo na ulemavu wake au atamtema ajue mapema
 
Old skuli. Imenikumbusha mbali sana. Unafaa kuwa mtunzi.
 
Kama ni kweli peleka kule jf doctor.

Kama nilivyosema, huku nilipotea njia tu na hata nilipotafuta upenyo wa kutokea, sikuuona na ikabidi nimwage mchele hapa hapa! Ahsante kwa kunionesha njia ingawaje hofu yangu ni kwamba madaktari jpili hawapo vituoni!
 
Ngoja nikutafutie namba ya shigongo...

Thanx in advance mkuu, itauwa umemsaidia sana dadangu! Kumbe Shingongo nae ni mganga?! kumbe jamaa ni mult-talented enh?! au sio shigongo wa magazeti?!
 
Back
Top Bottom