Mkuu, Kabla ya kufikia uamuzi wa kumtaka aje kukanusha ungejenga hoja mbadala kwanza ya PROCESS ambayo CCM walikuwa wanaitumia kuwapata wabunge wa viti maalum na kama ungepata upenyo wa shimo linalotumika kufanya kile ambacho unadai Juliana Shonza aliahidiwa, ndiyo ungekuja na hoja ya kumtaka akanushe.
PROCESS ambazo CCM ilikuwa inazitumia katika kuwapata wabunge wa viti maalum ziko wazi na siyo kama baadhi ya vyama vingine ambavyo wabunge wake wa viti maalum walipatikana kwa njia ambazo ni viongozi wachache wanazijua.
Hata nafasi ambazo Rais alitakiwa kikatiba kuzitoa kwa watu anaopenda bila kuulizwa sababu yake, Rais alizitoa kwa uangalifu mkubwa kwa watu ambao kila mwenye akili pevu alijua sababu za msingi za kufanya hivyo kwa maslahi ya Taifa.
Hoja yako inakosa nguvu kwa vile msingi wa hoja hauko.
Anyway, hili ni juu ya Juliana Shonza kulitolea ufafanuzi kama atapenda pamoja na kwamba hakuna basis za kufanya hivyo.